Kwanini Russia hataki kuwekeza kwenye Aircraft Carrier kama USA?

Ndiyo! Upelelezi ni jukumu mojawapo linalofanywa na F-35 kama jukumu la ziada. Lakini, F-35 ni ndege maalumu inayofahamika kama multirole combat aircraft. Yaani ina uwezo wa kutekeleza jukumu zaidi ya moja la kivita (combat) pale inapohitajika ndio maana ikapewa uwezo wa kuifanya itekeleze majukumu yote yaliyokusudiwa.

F-35 inapofanya mission ya upelelezi pekee, huwa si lazima kuingia katika anga la adui. Kwa wakati huo, inafanya kazi kama surveillance aircraft. Lakini, inapotumika kufanya mission za mashambulizi ya juu kwa juu ama ya kuelekea moja kwa moja ardhini kama bomber, hapo ndipo inapolazimu kupenya katika anga la adui. Kwa sababu hiyo, inabidi iwe katika stealth mode kupitia uwezo wake wa stealth.

Isitoshe, uwezo wa kutekeleza jukumu hilo la upelelezi unatofautiana kati ya ndege moja na nyingine. Ndege ambazo ni kwa ajili ya upelelezi kama jukumu kuu na pekee kama ilivyo kwa Global Hawk huwezeshwa zaidi kutekeleza jukumu hilo katika viwango vya juu zaidi (maximum capabilities) bila kuathiriwa na mifumo mingine ya majukumu mengine.

Sanjari na bombers pia. Kuna heavy bombers ambazo hutekeleza majukumu ya bomber pekee. Hizi huweza kufanya mashambulizi kwa kiwango kikubwa zaidi na yenye athari kubwa zaidi kwa adui kutokana na muundo wake na uwezo wake wa kubeba shehena kubwa ya mabomu (payload) ukilinganisha na multirole combat aircraft kama hiyo F-35 pale inapofanya kazi kama bomber (fighter-bomber).
F-117 ambayo ni stealth kule Serbia ilionekana mwaka 1999 na ikadunguliwa na S-125.
RQ Sentinel stealth aircraft iliteremshwa na Iran.
F-35 kule Syria ilionekana kwenye radar.
Ubora wa hizo ndege ni katika majaribio ya maabara, radar ya mwaka 1942 ina uwezo wa kuona stealth aircraft.

Silaha ni bidhaa na ili iuzwe lazima ipigiwe debe na kupewa sifa tofauti, its business.
Stealth F-35 is scam.
 
Back
Top Bottom