Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Habari ndugu zangu,
Kuna swali limekuwa likinitatiza kwa kipindi kirefu sasa. Mwanzoni nilidhani labda 'itifaki' haziruhusu kwa kiongozi wa juu wa nchi (Rais), kufanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini, mfano Televisheni / Radio / Magazeti.. Lakini hili nimepingana nalo baada ya kuona akialikwa mara kwa mara nchi za ugenini na kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali na Media za huko.
Kwa mfano, Nishawahi kumsikia Mheshimiwa Rais akihojiwa mara kwa mara na vyombo vikubwa vya habari kama vile BBC, Deutsche Welle, na vinginevyo.. Lakini kwa vyombo vya habari vya hapa nyumbani si jambo lililozoeleka, Kwanini?
SIJAWAHI kuona Rais akialikwa let's say ITV / TBC / Channel 10 kufanyiwa mahojiano kuhusu masuala yanayoendelea au jambo lolote kwa manufaa ya wananchi. Kama ishawahi kutokea basi ningependa kujuzwa kwanini imekuwa ni nadra kwa kiwango hicho?!
Je, ni sheria za nchi haziruhusu? Au ni utaratibu usiozoeleka na hivyo umeridhiwa uendelee hivyo hivyo tu? Kwanini iwe hapa kwetu tu na akienda nchi za nje afanyiwe Interview?
Nimeshashuhudia mara kwa mara Rais wa Kenya akihojiwa na vyombo vya habari vya huko mfano KTN (Sio ile Press Conf.), yaani namaanisha yale Mahojiano yaliyoratibiwa na Channel husika!
Juzi juzi nilimuona Mhe. Rais JK akiwa kwenye uzinduzi wa Kituo cha Azam TV International na kufanyiwa TEST INTERVIEW na Tido Mhando - Nilivutiwa sana na kujiuliza kwanini hili suala halifanyiki kabisa kiuhalisia na vyombo vyetu!?
Nimejaribu kuandika kwa kirefu ili nieleweke na kupata majibu ya kina kutoka kwenu wadau!
Nawasilisha kwenu nyote Wakuu wote wa JF tujadili, wakiwemo;
RUCCI Chachu Ombara Msamiati Pasco FaizaFoxy Watu8 figganigga Mag3 Donatila Mapengo 17

Last edited by a moderator: