Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,681
239,222
Nimeangalia game ya France na Romania mpaka dk hii ya 88 na nusu ambapo France inaongoza 2-1 , kiukweli huyu mchezaji anasifiwa bure tu .

Baada ya yeye kutolewa ndio timu ikapata uhai , kwa ufupi ni kwamba alikuwa mzigo kwa timu .

Sasa zile sifa zake zote za kule juventus ilikuwa za uongo ?
 
Nimemkubali sana Payet kwa goli alofunga japo kwenye mpira mimi si kivileee ila nimebet
 
Pogba ni bonge la mchezaji ila kocha anakosea namna ya kuwachezesha maana wachezaji watatu wanaocheza no 10 wote anawaanzisha kwa pamoja hivyo kila mmoja anacheza kwa kushindwa kucheza kwa uhuru! Pogba na Payet wanacheza no moja huku Matuid akikosa uhuru wa midfield

Mtu mmoja aliyewekwa nafasi yake ni Kante na ndo maana anaonekana sana lazima kocha aamue kati ya Payet na Pogba nani aanze
 
Jambo moja kuu, nimegundua wewe si mpenzi wa mpira, hata levo ya ushabiki hujafkia, labda shabiki maandazi mkuu.. Kuna jambo moja usilolijua, yule binadam kuna siku anakuwa katika form kuna siku anapotea, afadhali ungekuwa umemshuhudia kwa mechi hata 5 sasa moja tu unamsimanga, mkuu boli haliendi hvyo...

Jambo la ufaransa kutokucheza vizuri si tatzo lake, mfumo wa 4-3-3 hauko poa kwao unawanyima, muone hata fundi matuidi, mtizame griezman hilo ni tatzo.. Angalia alipoingiza winga kati akabaki matuid na kante ndicho kilichobadili mchezo mkuu tena japo si kwa kiwango kivile. Ni hayo tu mkuu
 
Kaka inaonekana umepata futari yako vzuri
Very good comment
 
Hivi kuna fundi wa penalti?
Hakuna mkuu.. Jambo baya ni kuwaona wachezaji kama malaika, nao wanakosea tu mbona, kuna kauli mtu anakwambia angekuwa messi au cr7pale hakukosi wakat wao wenyewe wanakosea, utofaut ni % ya ukoseaji wengine asilimia chache wengine asilimia kubwa so sitaki kumlaumu sana samata.. Socrates fundi wa penalt kakosa, zidane kakosa, huyo andunje messi na robot ronaldo wamekosa, mchawi gaucho kakosa.. Fundi kichogo henry kakosa, riquelme etc wamekosa.. Kukosea kupo..
 
Back
Top Bottom