Kwanini Odinga atashindwa mahakamani na hili liwe fundi kwa UKAWA!

Kwanini Odinga atashindwa mahakamani na hili liwe fundi kwa UKAWA!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,254
Mimi ni CCM asilia lakini kwa masilahi mapana ya kitaifa ninawapa ushauri wa bwerere UKAWA na washirika wao.

Raila na NASA wanamburuza Rais wao Uhuru Kenyatta na tume ya uchaguzi IEBC Mahakama ya kileleni ya Kenya na huu ni ufupisho wa msingi wa kesi yao:-

1)Uchaguzi haukuwa huru, haki, shirikishi na hakikishwa

2) Uhesabuji wa kura, ujumlishaji hadi kumtangaza Uhuru Kenyatta uligubikwa na uchakachuaji wa matokeo ya urais

3) Kifo cha Meneja wa teknohama wa IEBC Chris Musando kilichangia uvurugaji wa mawasiliano ya usafirishaji wa matokeo ya urais kutoka majimboni

4) Mitambo ya kielektronikia ya IEBC ilikuwa dhaifu kutokana na aliyepewa zabuni hakuwa na sifa na udhaifu huo ulisababisha udukuzi wa matokeo ya urais kutoka majimboni kufanyika makao makuu ya IEBC

5) Kura zilizokataliwa chini ya 3% ya kura xilizopigwa hazikupaswa kuondolewa kwenye jumla kuu ya matokeo ya urais

Kama nilivyosema awali, Raila na NASA wataangukia pua na UKAWA wajifunze siyo kuendelea kuzubaa zubaa tu.

Na ufuatao ni uchambuzi wangu binafsi.

USHAHIDI HAWANA

Raila na NASA wamekuwa wakitamba kuwa wana " a very tight case" lakini ushahidi wao unathibitisha uchaguzi ulikuwa huru, haki, shirikishi na hakikiwa au " the Kenyan election was free, fair, credible and verifiable. "

Raila na NASA wamekuwa wakiwadobosha mashabiki wao kuwa ushahidi walioupeleka Mahakama ya Kileleni ni zaidi ya kurasa 25, 000! Lakini pia wanakiri ushahidi huo zaidi ya 90% walipewa na IEBC. Tatizo liko wapi?

Tatizo hapa lina sura nne.

Moja hakuna hata fomu moja ya mawakala wa NASA walioiweka kama sehemu ya ushahidi. Hii inamaanisha fomu namba 34A ya IEBC haina mushkeli na madai yote tajwa hapo juu ni ya uongo mtupu. Ili kupinga matokeo yaliyotangazwa na IEBC Raila na NASA walipaswa watumie fomu zao wenyewe kutoka kwa mawakala wao. Hili halikufanyika na Raila na NASA hawawezi kuhoji uhalali wa kuhesabu matokeo ya vituoni kwa sababu hakuna mahali mawakala wao walipinga uhesabuji wa kura vituoni na kujaza malalamiko hayo kwenye fomu 34A.

Mbili, Raila na NASA wanadai mawakala wao hawakuzisaini fomu 34A za vituo vya kupigia kura takribani 14,000. Lakini sheria iko wazi wakala asiposaini fomu ya uchaguzi au kutoorodhesha malalamiko yake kwenye fomu husika ni kuwa anahesabika siku ya uchaguzi hakuwepo kwenye kituo cha uchaguzi na mahakama haiwezi kuyafanyia kazi malalamiko ya mawakala ambao hawakufuata sheria ya uchaguzi.

Tatu, Raila na Kalonzo Musyoka wao ndiyo vinara wa kutoa ushahidi kwa kuwakilisha nakala za hati za viapo. Tatizo liko wapi? Ushahidi wao ni kuwasimuliwa "hearsay evidence" na haukubaliki na wala hauwezi kufanyia kazi kuhoji yaliyomo kwenye fomu na. 34A. Penye ushahidi wa maandishi ni dhahiri blah blah za vinara hawa hazikubaliki. Fomu na. 34A zinajitosheleza na isitoshe si Raila au Kalonzo walikuwepo kwenye vituo vyote vya uchaguzi siku husika kwa muda wote hadi zoezi la kupiga kura kukamilika na kuhesabiwa.

Nne, majumuisho ya kura za vituoni hufanywa na wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi kutoka fomu na. 34A hadi fomu na. 34B na kutumwa IEBC. Majumuisho ya matokeo ya fomu na. 34B hufanywa makao makuu ya IEBC na kuwekwa kwenye fomu na. 34C. La ajabu wakala mkuu wa Raila na NASA Bw. Musalia Mudavadi aligoma kuisaini fomu na. 34C au kuandika malalamiko tajwa kwenye fomu hii. Ni dhahiri, Bw. Musalia Mudavadi alipewa nafasi ya kuhoji matokeo na hakufanya hivyo sasa mahakamani Raila na NASA wanaenda kufanya nini? Mbaya zaidi kwa Raila na NASA, Bw. Musalia Mudavadi hajawakilisha hati ya kiapo mahakamani kutoa sababu zilizomzuia asifuate sheria ya uchaguzi wa Kenya. Mahakama ya Kileleni haiwezi kufanyia kazi malalamiko ambayo hata IEBC haikupewa nafasi yake ya kisheria kupitia fomu 34C kuyafanyia kazi.

Madai ya udukuzi ya kimfumo Raila na NASA wanategemea ushahidi wa mwendazake Chris Musando. Tatizo ni nini? Tatizo ni kuwa Taasisi ya kikatiba kama IEBC siyo mtu bali ni nguvu ya kisheria. Waajiriwa hawezi kuipa Taasisi uhalali bali ni sheria na jinsi sheria inavyotekelezwa na Taasisi husika. Hivyo, haya majitaka yatamwagwa kwa kukosa uhimili wa kisheria

Madai ya kura zilizoharibika kujumuishwa kwenye jumla kuu ya matokeo ya urais hili ni swala la kisheria ambalo mahakama hiihii ya kileleni ilikwisha kuliamua mwaka 2013 katika kesi ya Raila Amolo Odinga dhidi ya IEBC na Uhuru Muigai Kenyatta. Mahakama ilisema kura batili ni batili na kuzijumlisha kwenye jumuisho kuu ni kuyabatilisha matokeo halali. Sasa Raila na NASA sijui wamemeza maharagwe ya Chunya kudhani kura batili zaweza kuruhusiwa kujumlishwa kwenye jumla kuu? Ili iweje? Kubatilisha matokeo halali ya ushindi wa Rais Kenyatta?

MAFUNZO KWA UKAWA

1) Kabla ya kuhoji matokeo ya urais hakikisheni fomu zote za vituoni mnazo na mawakala wenu wamehoji uhalali wa matokeo kwenye fomu husika

2) Kwenye website zenu muwe mnabandika fomu zote za vituoni mlizozikusanya na majumuisho yake kuthibitisha tume ya uchaguzi haikuwatendea haki

3) Acheni Kuitumia katiba kama kivuli cha kutokwenda mahakama kuu kuhoji uhalali wa matokeo ya uchaguzi wa Urais. Upo uamuzi wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa unaoonyesha wazi kama tume ya uchaguzi haikufuata sheria na ushahidi upo mahakama ikiombwa kuchunguza na kutolea maamuzi

4) Katiba yetu inaitaka tume ya uchaguzi kufuata sheria ya uchaguzi kabla ya kumtangaza mshindi wa urais. Matokeo yoyote yale ya urais yanayokiuka sheria ya uchaguzi hakuna ibara yoyote kwenye katiba inayoizuia mahakama isiyachunguze na kuyatolea maamuzi.

5) Mkome kuwapotosha wapigakura kuwa mlishinda uchaguzi wa Urais wa 2015 huku si kwenye websites zenu au mahali popote pale mmethibitisha ni fomu zipi za vituo vya kupigia kura zimewaongoza hata kuhitimisha hivyo.

Mwisho CCM hoyee!
 
MAFUNZO KWA UKAWA

1) Kabla ya kuhoji matokeo ya urais hakikisheni fomu zote za vituoni mnazo na mawakala wenu wamehoji uhalali wa matokeo kwenye fomu husika

2) Kwenye website zenu muwe mnabandika fomu zote za vituoni mlizozikusanya na majumuisho yake kuthibitisha tume ya uchaguzi haikuwatendea haki

Mwisho CCM hoyee!

1. Mpaka leo kuna majimbo yapo mjini Ukawa hata fomuz amatokeo za uraisi hawajazipata.
na hapa ndipo kwenye jipu kuu, lazima uwe na mawakala wa uwakika wataosimamia mpaka mwisho, either umeshinda au umeshindwa laizma uwepo mpaka dakika ya mwisho upewe fimu yako na uilinde.

kule kote walikoshinda ukawa arusha, dar na mbeya mbinu hii wanaijua na wanitekeleza sawasawa. ndio maaana mdee na mtulia walipo taka kuchakachuliwa walikomaa maana fomu hizi zote walikuwa nazo, ila yule muhindi wa ilala aliliwa kwa sababu alikosa hizi fomu, inasemekana mawakala wake walinunuliwa na kukimbia nahizi fomu, mwisho wa siku akajikuta anafomu zilizochakachuliw ana zungu na zote zimesainiwa na wakala mmoja. akazikana kataka masanduku yahesabiwe upya kitu ambacho sheria hairuhusu.

2. hii ni ngumu kumbuka tally center zilivyovyamiwa.

All in all UKAWA waandae pesa ya kutosha kulipa wamawakala na watoe elimu ya kutosha na waandae mawakaala kila kituo wawili au watatu wa vyama tofauti.

NB:
Uchakuzi mkubwa ulifanyika halmashahuri wakati wa majumuisho nakutuma matokeo tume, na muda huu mara nyingi wapinzani wameshindwa au wameshinda na wameondoka kushangilia, mkurugenzi anabaki peke yake anafanya atakavyo.

mfano mzuri, mdee na mnyika pamoja na kushinda hawakuondoka walikomaa wakisubiri kura za uraisi zitangazwe na zitumwe kituoni ndio waondoke.
 
Nakala za fomu 34A hupewa nakala kwenye vituo vya uchaguzi baada ya kura kupigwa na kuhesabiwa, kujazwa kwenye fomu na mawakala kuzisaini
 
Back
Top Bottom