BioPsychologist
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 724
- 1,019
Haina ubishi kuwa kuna watu wako single hadi wanajiogopa wenyewe, karibia kila siku wanaweza kujiuliza hili swali zaidi ya Mara tano na huwa pengine wana kosa majibu, au wana pata njia za ku solve wanachodhani kuwa single ni kama ugonjwa furani hivi, la! hasha!.
Moja kati ya matatizo ya kawaida katika hisia za mwanadamu ni kuwaza kwa nini yuko single, mfano. Kwanini mimi niko single nina shida gani? Mbona furani na marafiki zangu wana wapenzi?, Nina kasoro gani ambayo watu wanaiona? Kwanini mimi?
Sababu mbili kubwa zinazofanya watu kuwa single;
1. Aliingia katika mahusiano akapenda na akatendwa kiasi cha kuumizwa na hisia za mapenzi na baada ya kutoka akaamua kuacha.
2. Hajawahi kufanya au kuwa na makubaliano ya kimapenzi na mtu yeyote bali hisia za mapenzi na maumivu anayoyashuhudia kutoka kwa jamii yanampa hofu na woga wa kuingia.
Kutokana na tatizo hili moja kati ya machapisho yaliyofanywa na Alexandria-Egypt 2006-2017,(2knowmyself.com) watafiti wanasema kuwa single hakuna athari yeyote ikiwa kweli huna yeyote unaemuwaza wala kumpenda na kitendo au hali ya kuwa single huomgeza uwezo wa mtu katika kutathimini mambo hasa mahusiano yenyewe.
Kupitia hii makala unaweza kupata majibu sahihi ya kujibu kwa watu wanaokuuliza maswali kama "kwa nini upo single?" Ambatana nami hadi mwisho wa makala hii.
ZIFUATAZO NI SABABU KWA NINI BAADHI YA WATU WAKO SINGLE, EITHER KWA KUJUA AU PASIPO KUJUA SABABU MOJAWAPO AU ZOTE, HUJIONA KAMA HAWAKO SAWA, YAANI WANA TATIZO LA KISAIKOLOJIA KUMBE SIO KWELI.
Wewe ni single kwa sababu unajua na kutambua nini unakitaka, unataka mpenzi wa aina gani, pengine nia yako haijatimia kuwa katika mahusiano, tofauti na hapo utawaona wengi wako katika mahusiano ambayo sio yao, bali wameingia kwa sababu tu wanataka wawe kwenye mahusiano, na sio uchaguzi zao sahihi.
Wewe ni single kwa sababu huenda unajiamini, kwa mfano. Mategemeo yako mwenyewe na imani yako unaona sio mda mwafaka na unaowaona sio kwamba ni wabaya bali mguso wa mapenzi bado haujafika kulingana na mipango na maisha, wanaamini kuwa anaweza kuishi bila mpenzi maana haimuathiri.
Upo single kwa sababu unaridhika na mvuto,tabasamu na bashasha nyingi toka kwa marafiki zako, huna hisia za sex maana huenda uliumizwa na mpenzi au hujawahi kabisa kufanya ngono, kumbe umeamuwa tu na kudhani mda bado.
Upo single kwa sababu unaamini kuwa utakuwa mzuri ukiingia kwenye mahusiano na umri furani, hata kama ni miaka 30-40 sababu zako sio mbaya maana dunia unaiona wewe kwenye maono yako, ni maamuzi sahihi wala usiingie kwenye mahusiano kwa sanabu ya mshindo na kelele za watu au kwa kigezo cha umri.
Upo single kwa sababu hujapata mpenzi unaempenda wewe, kutongozwa na kuwaona wazuri sio sababu ya kufanya uingie kwenye mahusiano, ni kwa sababu hujapenda tu, yeyote anaependa huingia kwenye mahusiano.
Wewe ni single kwa sababu uliekuwa nae hujamfukuza bali kajitoa mwenyewe kwenye mahusiano, hujalazimisha uwe single bali ni hali imetokrea maana mahusiano ni ya wawili, huenda unampenda sana lakini kakufanya wewe uwe single, hujataka bali umekubaliana na matokeo.
Upo single kwa sababu unajiaminisha kupita kiasi (over confidence) unajuwa unadhani kwamba kila unaempata ni bora na anakufaa zaidi bila kuangalia wala kujari kuwa yeye ni mwanadamu na ipo siku atakosea, sasa inapotokea kosa lolote maana yake umnapoteza imani kwake maana alikuwa uanamini kupita kiasi, hii inawatokea zaidi wanawake.
Upo single kwa sababu hutaki au huna mazingira ya kujivutisha mwenyewe kwa watu wakuone na kukupenda, huenda uko bize sana na kazi ratiba yako ya siku haikufanyi ukutane na watu mbalimali zaidi ni walewale wa kila siku, hapo ni lazima uwe single.
Hujawa na mahusiano kwa sababu hutaki mtu ambae anakupata au unampata kirahisi rahisi tu, inaweza kuwa sababu ya sifa zako za kupata mtu wa kiuingia nae kwenye mahusiano, hupendi utongozwe kwa mda mfupi au kwa mwanaume hapendi mwanamke anaemkubalia haraka haraka, bahati mbaya unakutana nao sana wa aina hiyo,furaha yako ni kukutana na mume au mke ambae atakupa changamoto (msoto) kumpata.
Kuwa single sio UGONJWA wala MAPUNGUFU, bali ni maamuzi ya mhusika mwenyewe, kubali na kuamini kuwa sababu inayokufanya uwe single ni sahihi kwako bila kujari changamoto unazokutana nazo.
BADILI MTAZAMO,
Ahsanteni sana!