Kwanini ni wachagga tu na Krismas? Vipi makabila mengine?

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Nimejiuliza ni kwa nini watu wa kaskazini, hususani Wachagga hupenda kwenda kusherekea krismas kwao? Lakini ukitizama makabila mengine hayana utamaduni huo. Pale Ubungo ukienda huwezi kuta ulanguzi wa tiketi kwa gari za Dodoma, Moro n.k.

Hii ikimanisha wazi watu wa pande hizo hawaendi kwao kwa sikukuu. Ni ipi sababu kubwa inayopelekea Mchagga kufanya hivyo? Makabila mengine hayana ndugu, wazazi na jamaa huko watokako?

Ebu tutafakari hili!
 
wengine hatuendi coz ukitangaza tu waenda utapigwa vibomu ushindwe hata nauli ya kurudi mujini...plus hukawii kuambiwa huyu mtoto wa mjombako nenda naye ukamsomeshe amemaliza primary...hapana kwa kweli nitawapigia tu simu niwape heri ya kirisimasi
 
Hujasikia ulanguzi wa ticket za Dar-Mza? Au kwa vile ume concentrate na Dar-Ar tu?
 
wengine hatuendi coz ukitangaza tu waenda utapigwa vibomu ushindwe hata nauli ya kurudi mujini...plus hukawii kuambiwa huyu mtoto wa mjombako nenda naye ukamsomeshe amemaliza primary...hapana kwa kweli nitawapigia tu simu niwape heri ya kirisimasi


Mkuu kama uwezo upo kwanini usimchukue tu huyo mtoto wa Mjomba asome? Huwezi jua pengine ndio huyo atakae kuja kukufaa mbeleni.
 
Kihistoria, wakati Yesu anazaliwa zamani za Biblia ilitoka amri kutoka kwa mfalme (Kaisari) kuwa WATU WOTE waende kule kwenye asili yao ili wakahesabiwe. Ndio maana hata Yesu alizaliwa na Mariam wakiwa ndio wamefika kwenye asili ya Yusufu. Kutokana na kile kitendo cha kila mtu kwenda kwenye asili yake yaani alikozaliwa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismas Wachaga na baadhi ya watu wa mataifa mbalimbali wanadumisha huo utamaduni wa kurudi makwao wakati huo JAPOKUWA hakuna amri iliyotolewa ya kwenda kuhesabiwa. Nimeona Wazungu wanaofanya kazi katika maofisi mbalimbali wakienda kwao Ulaya wakati huu wa Krismas. Au jaribu kuulizia sasa hivi nauli za ndege kwenda Ulaya nchi yoyote utakuta bei ni kubwa mno kulinganisha na ilivyokuwa Septemba au Oktoba kwa sababu wazungu wengi wanatoka Tanzania na Afrika kwa ujumla kwenda kwao majira haya ya Krismas ikiwa ni desturi iliyoanzishwa majira ya wakati Yesu anazaliwa.

Nimejiuliza ni kwa nini watu wa kasikazini hususani wachaga hupenda kwenda kusherekea krismas kwao?
Lakini ukitizama makabila mengine hayana utamaduni huo.Pale ubungo ukienda huwezi kuta ulanguzi wa tiketi kwa gari za dodoma,Moro n.k.
Hii ikimanisha wazi watu wa pande hizo hawaendi kwao kwa sikukuu.Ni ipi sababu kubwa inayopelekea mchaga kufanya hivyo?
Makabila mengine hayana ndugu,Wazazi na jamaa huko watokako?
Ebu tutafakari hili!!!
 
Wanaenda kupiga ramli! Teh Teh..

nyie mnajulikana kwa sifa za kipuuzi, mnakujaa kwenye miji ya watu mkiwa wazima na kusahau kurudi kwenu ,
mwisho mnarudishwa mkiwa kwenye jeneza

Jengeni utamaduni wa kwenda kutembelea kwenu mara kwa mara na si kusubiri misiba au matatizo ndo mwende..
 
Back
Top Bottom