Kwanini ni vigumu sana wananchi kujikomboa kutoka kwa 'wakoloni weusi?' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ni vigumu sana wananchi kujikomboa kutoka kwa 'wakoloni weusi?'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 20, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Jamani nauliza: Inakuwaje inakuwa vigumu kwa wananchi kujikomboa kutoka makucha ya 'wakoloni weusi' kuliko kutoka kwa 'wakoloni weupe?'

  Nakumbuka ilichukuwa miaka michache tu kwa wananchi kuikomboa nchi hii kutoka kwa wakoloni wa kiingereza, lakini sasa hivi ni vigumu sana kujikomboa kutoka kwa hawa 'weusi' ambao miaka 50 baada ya uhuru, wamegeuka kuwa ni sawasawa tu na wale 'weupe' au hata wabaya zaidi.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ni kweli kabisa! nchi zote tu, Ukombozi II huwa ni tabu sana, lakini hili bara la Afrika limezidi. Viongozi waliopo wako hata tayari kuuwa. Lakini kwa kiasi fulani Ocampo anajaribu kusaidia -- mfano ni Kenya.
   
 3. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Waafrika na hasa watz ni waoga sana,wanaogopa kutekwa,ukianzisha tutakukuta msitu wa pande umepumzika baada ya kichapo.
   
 4. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sijui niseme nini hasa!, lakini kuna watu wanakesha wakiomba, wakiamini hawa ni ndugu zetu tu, shetani kawaingia, wanakesha kuwaombea wabadilike, wakati wao bila huruma wanatumaliza, wanaifilisi nchi, wao, wanatuona sisi mafala tu, kwa kweli watu wachukue hatua nyingine, hawa watu kwa sala, hawabadiliki, lazima wapatiwe physical action ya kuwashtua kuwa Wananchi si mafala, hawajalala na wamewachoka, I think hata kwenye Bible kuna issue za war zilizozungumziwa, sometimes ni kuomba power za design nyingine kwa God ili kudeal nao, wana kiburi sana hawa watu, yaani wanamuomba mpaka Mungu kabla ya kuanza Bunge, halafu baada ya kuanza wanaishia kufanya unafiki, uongo kwa kwenda mbele
   
 5. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi ambayo ilipaswa kuwa na amani sana, kama tungeendelea kuishi kwa kuheshimiana na kujaliana, ni sehemu tulivu but viongozi hawa wababe, madicteta, wasiokubali ukweli na kukosolewa, wanaoifilisi nchi na kutumia rasilimali za Taifa kwa faida zao zaidi, wataifanya nchi itikisike kwa kiasi kikubwa kwa muda so soon, kabla haijakaa tena sawa, kama mapinduzi yanavyotokea sehemu mbalimbali Duniani
   
Loading...