Kwanini ni ngumu kwa biashara na miradi ya Waafrika kufikisha muda mrefu kuliko wenzetu?

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,721
Ni bara pekee tu ambalo ni Afrika, kama kichwa cha habari hapo juu.

• Kwa nini huwa vina kwama au kufa mfano mmiliki akifa tu ndo kila kitu kimekufa mifano hipo mingi.

• Kwa nini biashara za waafrika zina kuwa na umimi wewe ndio mwanzo na mwisho.

• Kwa nini miradi au biashara inaanza kuwa na wanatamaa, mandugu, kukosa uongozi.

Ni mengi tu
Je, hawa wenzetu wahindi, wazungu wanafanyeje mpaka leo unasikia kampuni hipo, biashara hipo, mashamba yapo na n.k

Maana kuna kampuni mmoja inapoelekea ndio kushindwa
 
Kwanza inabidi unyumbulishe Waafrika gani. Kuna kina Aliko Dangote wamerithi biashara za familia kipindi kirefu na wanaziendeleza.

Kwa hiyo si kweli kwamba Waafrika hawawezi kuendeleza biashara zao.

Ila, ni kweli pia kwamba, kwa kila Aliko Dangote mmoja, kuna wengine wengi wanashindwa.

Tatizo kubwa ni kutopendana, kukosa
inclusivity.

Kwa mfano, rais anapoingia madarakani na kusema wazi kwamba hahitaji hata senti moja ya mfanyabiashara yeyote kwenye kampeni yake, wakati wafanyabiashara ni sehemu ya jamii, tafsiri ni kwamba huyu rais katika mawazo yake anaona wafanyabiashara wote ni wezi na pesa zao ni chafu.

Na kuanzia hapo mkakati wake ni kuwanyanyasa na kuwasumbua wafanyabiashara tu nchini kwake.

Sasa hapo watu wakishindwa kuendeleza biashara utashangaa?
 
Nidhamu ya pesa na kumbukumbu. wengi wetu tuna dhana ya kutokutumia sana maandishi tukiamini tutakumbuka tu baadae ikitokea shida. pesa ni kitabu, pesa ni maandishi.
 
Mapenzi na njaa ambayo inapelekea wizi hamna kongine.
 
Back
Top Bottom