Kwanini biashara nyingi hufa baada ya Mwanzilishi Kufariki?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,621
Anaandika Sadick Tusia huko 'X' zamani Twitter

...........


Biashara nyingi sana huwa zinakufa baada ya wamiliki wake kufariki na uchunguzi wangu mdogo nilioufanya asilimia kubwa ya biashara ambazo hufa baada ya muanzilishi kufariki ni zile zinazomilikiwa mtu mmoja yaani solopreneur.

Sio Tanzania tu hata nchi nyingine nyingi duniani biashara nyingi hufa baada ya muanzilishi wa awali kufariki.

Kwa takwimu za nchi ya Marekani ni kwamba asilimia 67 ya biashara za familia( family business) hufa katika kizazi cha pili (second generation) na asilimia 90 ya zilitoboa hufia kizazi cha tatu (third generation).

Kwanini biashara zinakufa?

1.Wamiliki wengi wengi wa biashara kutokuweka msingi mzuri wa biashara zao kiasi kwamba hata akifa au akiugua muda mrefu ziendelee kuwepo,

2.Kwa wamiliki mmoja mmoja kuto kuandaa warithi mapema sana na hapa ndo kuna shida kubwa sana.

Bahati mbaya zaidi mwanzilishi wa biashara ndiyo anakuwa mmiliki wa kila kitu hivyo hata ikitokea akafariki bila kuacha mirathi maana yake kikao cha mirathi ndicho kitakacho amua nani asimamie biashara ya marehemu bila kuangalia uwezo wa huyo aliyeteuliwa katika biashara.

Muanzilishi wa biashara kutowandaa wala kuwaendeleza watoto wake/mke/ndugu katika elimu ya biashara ili kuwajengea uwezo wa kibiashara wa kusimamia baishara na hivyo kuacha wasimamie kimazoea tu mwisho wa siku biashara hufa.

Kiufupi waanzilishi wengi wa biashara huwa hawawezi kuandaa succession plan ambayo ndiyo hutoa muongozo wa kuendelezea biashara na nani wa kuiendeleza hata ikitokea yeye akafariki dunia.

SULUHISHO NI NINI?

1.Tujitahidi kuwa na makampuni na si kuendesha kama biashara ya mtu mmoja na hii inaweza kuwa suluhisho kwa sababu kampuni hujengwa katiki misingi imara zana.

Moja ya msingi imara wa kampuni ni: MEMORANDUM & ARTICLE OF ASSOCIATION.Huu ndo Msahafu au Biblia ya kampuni kiasi kwamba haijalishi Mkurugenzi au muanzilishi yuko hai au amekufa kampuni kama kampuni itaendelea kuishi vizazi na vizazi.

2. Kuwajengea uwezo wasimamizi wa biashara yako tangia mwanzo na kuwaelimisha mambo mbalimbali yahusuyo biashara yako.

Watoto wengi hawaandaliwi kuongoza biashara za familia.Labda ni ukosefu wa kuaminiana kwenye familia.

Ni muhimu sana kuwaandaa watoto kwenye biashara za familia.Wazazi wanatakiwa wajue siku itafika umri utakataa kuendana na pirika za kuendesha biashara kwahiyo ni muhimu kuwapa muongozo mapema hili wakikosea warekebishwe kuliko kuwaachia peke yao hapo mbeleni bila maandalizi.

3. Kuandaa succession plan mapema sana ya nani atasimamia hii biashara pindi nikifa, na huyo aliyeko kwenye huo mpango aandaliwe mapema kielimu na si mtu aliendaliwa aachwe akasomee kozi zingine tofauti na za biashara.Hapa mmiliki ahakikishe mtoto wake atakaye mrithi anakua na mwelekeo wa masomo ya biashara sana na si mtoto anatazamiwa kurithi biashara za baba au mama huku yeye achukua shahada ya historia au kitu kingine kisichoendana na biashara.

4.Kuwapa warithi wa biashara yako mazoezi ya vitendo yaani wawe wasimamizi kuanzia ukiwa bado hai na uwe mshauri wao tu.Mfano wahindi huwajengea watoto wao uwezo wa kibiashara kwa vitendo tangu wakiwa watoto wadogo.

Bilionea namba moja Afrika Mashariki na kati Bwana Mohammed Dewji maarufu Mo (mmiliki wa makampuni ya METL ambapo anamiliki zaidi ya asilimia 70 ya hisa zote) katika moja ya mahojiano yake aliyowahi kufanya alisema kwamba wakati yupo mdogo alikuwa anashinda na baba yake dukani baada ya kutoka shule na kuna wakati mwingine alizuiliwa kwenda kucheza na wenzake ili abaki katika biashara na baba yake kitu ambacho kimsingi kimemsaidia kumemjengea uwezo mkubwa katika biashara ambapo hata elimu yake ya juu alisoma masomo ya biashara.

Leo sina mengi ila tu nakuombea mshale wa mafanikio ukayachome maisha yako.

Wasalaam

#Tuendelee_kujifunza.

Regards,
Jeff Bezos
 
Wenye akili tu ndio watakaoelewa ulichoandikwa ukweli ni kwamba wengi ni maskini ndio maana hata wakifa hakuna cha kurithi kwa ajili ya vizazi mpaka vizazi wengi tunamiliki perishable assets.
 
Kusomesha watoto masomo ya biashara sio solution kwani mfano uhasibu au ujasiliamili Bali ni kujua aina ya biashara na mahitaji yake baadae.
Mfano watoto wanaweza kusoma Sheria hasa business law na hii Bora zaidi kuliko kitu kama general MBA.
Kitu kingine ni engineering ambayo haijakaa kibiashara lakini kama kizazi kijacho kitaandaliwa ktk upande huo basi Kuna uwezekano wa kusurvive baadae kwani ugunduzi ndio moyo ya biashara yeyote.

Mwisho ni kuzaa hao watoto na kuwaelisha kivitendo zaidi na sio lazima English medium.
 
Hizo biashara ukichunguza ni biashara za kiafrica

Baba akifa unaambiwa Kila mtu afe na chake
Ni.kweli abadilishe kichwa cha habari kilometers kwa nini biashara za waafrika hufa muanzilishi akifa

Za wahindi,waarabu ,wapemba na wazungu huwa hazifi.muanzilishi akifa
 
Ni.kweli abadilishe kichwa cha habari kilometers kwa nini biashara za waafrika hufa muanzilishi akifa

Za wahindi,waarabu ,wapemba na wazungu huwa hazifi.muanzilishi akifa
biashara za kiafrica hazina succession plan, period, nyingine ni ngonjera tu.
 
Baba unakuwa na jini la kazi, pia mswalihina kweli kweli swala 5, mtoto unampeleka madrasa huko anafundishwa majini ni shirki ni haramu hayafai, sasa utamrithishaje maana ameshajengeka kivingine, kwamba maimuna (jini) ni usheitani 😁😁😁
 
Kwa kifupi hii kauli "utajiri ni siri na siri ndio utajiri" ndicho kikwazo kikubwa. Ukiona biashara iliyoendelea baada ya mmiliki kufa ujue hiyo biashara haikuwa na siri. Hata kama ilikuwa na siri, kuna mmoja aliyemuamini na kumpa hiyo siri.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nadhani tatizo kubwa ni kuwa matajiri wanajisahau. Ukiishapata hela unaongeza vimada. Na hao vimada wanachukiana.Wanawajaza sumu watoto wako wote pamoja na mkeo. Ukifa hauachi team bali unaacha watoto wabinafsi kila mmoja anataka chake asepe.
 
Back
Top Bottom