Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,314
- 72,740
Jana kwa ghafla Waziri wa sheria katoa tamko, waziri wa habari naye pia na huko Bungeni Zungu naye kachachamaa kuhusu kutajwa kwa marais wastaafu katika kadhia mbalimbali.
Lakini ukiwasikiliza vizuri ni kama maagizo hayo yameratibiwa na mtu/ofisi moja.
Nani karatibu vitisho hivyo ambavyo havina nguvu kisheria? Na kwa nini sasa wakati ambapo mjadala mkali kuhusu kufuta kinga umeshika kasi ndio vitisho vitokee?
Au aliyeko madarakani anaona akiruhusu mjadala na kinga ikatolewa na yeye atakuwa kajirahisishia kushtakiwa atakapotoka madarakani 2020?