Kwanini NECTA hakuna vyeti vya kughushi wala 'Incomplete'?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,858
Naomba mwanzo mwanzoni kusahihishwa kama ninachokijua hakiko sahihi. Nimefuatilia orodha mbalimbali zilizotolewa Utumishi juu ya uhakiki wa vyeti. Nikiri nami kuwa nimefanyiwa uhakiki kwakuwa ni mtumishi wa umma. Namshukuru Mungu, hadi sasa, sipo kwenye orodha yoyote iliyotolewa na Utumishi.

Hadi sasa zimetolewa Orodha za watumishi wa umma waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi. Kwa jinsi nilivyoisoma Orodha hiyo, sikuwaona watumishi wa Baraza la Mitihani la Taifa almaarufu kama NECTA. Imetolewa tena Orodha ya watumishi wa umma ambao taarifa zao hazijakamilia yaani 'Incomplete'. Namo humo NECTA hawamo.

Ndiyo maana najiuliza kuwa kwanini NECTA hakuna vyeti vya kughushi wala 'incomplete'? Are they perfect to that extent?
 
Zoezi la kuhakiki Vyeti feki lilifanyika kipindi kile Ndalichako ndio Mnene wa NECTA lakin kwa kuwa kilikuwa kipindi cha JK, Prof Ndalichako alishauri wanaojihisi Vyeti Vina utata basi ni bora waandike Barua ya kuacha kazi.

Watu Takriban 6 nakumbuka waliacha kazi kabla ya zoezi na zoezi likafanyika likaisha.

Ilikuwa kipindi kile kuna wimbi la Wizi wa Mitihani ya Kidato cha nne na Sita!
 
Hapa unaamini kabisa umejibu swali lililoulizwa?
 
Hapa unaamini kabisa umejibu swali lililoulizwa?

Kwani kuna Marking scheme humu? Weka basi Jibu sahihi!

Kama zoezi la uhakiki walishafanya na kujiweka sawa kabla ya zoezi hili la Kitaifa bado ulitegemea wangekutwa wenye Vyeti feki?
 
Kwani kuna Marking scheme humu? Weka basi Jibu sahihi!

Kama zoezi la uhakiki walishafanya na kujiweka sawa kabla ya zoezi hili la Kitaifa bado ulitegemea wangekutwa wenye Vyeti feki?
Hakuna ubaya vikihakikiwa tena na matokeo ya uhakiki wa vyeti vyao kuwekwa bayana.Hii itaondoa manung'uniko, na isitoshe kama vya kwao viko sawa hakuna haja ya kuwa na hofu.
 
Hakuna ubaya vikihakikiwa tena na matokeo ya uhakiki wa vyeti vyao kuwekwa bayana.Hii itaondoa manung'uniko, na isitoshe kama vya kwao viko sawa hakuna haja ya kuwa na hofu.

Orodha inayoendelea kutoka ni ya walioghushi, Wewe unashauri wafanyeje Kama Hakuna aliekutwa kaghushi?

Itawezekanaje watoe orodha ya walioghushi Kama Hakuna aliekutwa kaghushi?
 
Khaaa!!! Yaani mimi ndio nasahihisha mitihani (najijua ni kilaza ila nimepewa hiyo nafasi kama muujiza) ningali bado ni mmoja wa watahiniwa, najaza alama za wengine. Unategemea hadi karatasi zinagawiwa kwa wenye nazo nitakua sijafanya yangu?? Wao ndio wanakaa na database ya matokeo na vyeti vyote vilivyokwisha tolewa, so ni ngumu sana kujiachia wakamatwe
 
Orodha inayoendelea kutoka ni ya walioghushi, Wewe unashauri wafanyeje Kama Hakuna aliekutwa kaghushi?

Itawezekanaje watoe orodha ya walioghushi Kama Hakuna aliekutwa kaghushi?
Kuna uwezekano mkubwa tu kwamba hata huko NACTE/TCU bado wapo walioghushi na ili kuwabaini ni wakati huu unapofanyika uhakiki kitaifa vyeti vyao vihakikiwe kwanza kabla ya kuhakiki vingine.
 
Kwani ni lazima kila taasisi iwe na vyeti feki?
Mbona taasisi nyingi tu hazijaorodheshwa wahanga wake Mf. Pale blue house, kwa wajeda wa rangi na majina yote hata kulee kwa mzee wa kazi a.k.a makiliiiikriliiii hawajaweka academic certificates similiraty index zao?
Guys, this is time to concur with notion that all Tanzanians are the same but not equal!!
 
Sakata la vyeti ni kizungumkuti, kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wangepunguzwa sifa zao,mfano wewe ulitakiwa urudishwe kwenye sifa ya astashahda badala ya stashahada.
Nakumbuka mwaka fulani nilikuwa Songea,na kulikuwa na afisa mmoja wa polisi akiwa na wadhifa mkubwa kule CCP na zilipotoka nafasi za upolisi alisomba wafanyakazi wake wa ndani kama saba hivi,kuanzia walisha mifugo,wapishi,watunza bustani na mashmba wote wakaingia upolisi kwa kutumia vyeti vya kidato cha nne vya watu wengine!!!
Sasa hawa najua zoezi la uhakiki litawaacha salama maana vyeti vyao ni halali,ila kiuhalisia hata elimu kamili ya msingi hawana.!!!!
Mmoja aliyetoa cheti chake nasikia alilalamika baada ya kusikia jina lake linatumiwa na polisi huko Mpanda lakini alishindwa namna ya kufika huko maana yeye hana kazi.
 
Back
Top Bottom