Kwanini ndoa za aina hii hazidumu kwa muda mrefu?

Kwanini ndoa za aina hii hazidumu kwa muda mrefu?

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Wakuu salute kwenu.

Sina mengi ya kueleza ila nataka kusikia machache toka kwenu kuhusiana na hiki kitu kinachoitwa ndoa.

Mara nyingi watu hupenda kufanya sherehe au harusi baada ya kufunga ndoa, kitu ambacho ni kizuri kwa kujiwekea kumbukumbu ya kihistoria katika maisha yao. Nawapongeza sana kwa hilo

Kinacho nisikitisha kama siyo kunishangaza ni kwanini asilimia kubwa ya ndoa hizi zinazofanyiwa sherehe hazidumu kwa muda mrefu ukilinganisha na zile ambazo watu huoleana kienyeji?

Chukulia mfano ndoa ya Dogo Janja na Uwoya, ndoa ya Stamina, ndoa ya Roma Mkatoliki, ndoa ya Naseeb Abdul na Zari na wengineo wengi wasio maarufu, ndoa zao zimevunjika miezi/miaka michache baada ya kuoana na kufanya sherehe.

Je, kipi hupelekea ndoa za aina hiyo kuvunjika mapema?

Je, ni nguvu ya shetani hutumika kuzivunja kwa sababu ya kuoneana wivu kwa wale waliopo nje ya ndoa au ambao hawakufanya sherehe kwenye ndoa zao?

Najua sababu zipo nyingi kwahiyo kupitia kwenu nitapata kitu cha kujifunza kuhusiana na kufanya sherehe wakati wa kufunga ndoa.

images%20(5).jpeg
images%20(3).jpeg
images%20(1).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataalam wanasema mkusanyiko wa watu wengi kwenye harusi haina baraka vijicho utapata vingi.
 
Jiwe alipaswa kuchukua namba 1 alafu lemutuz umtoe man uyo ni njaa ndo inamsumbua ...umuweke...Polepole..alafu Muigulu mtoe muweke spika wote wawili wanafungana. Mzee Magu lzm achukue no 1
Mkuu umeelewa mada Lakini?
 
Back
Top Bottom