Kwanini ndoa nyingi za vijana huvunjika baada ya muda mfupi?

Msanumbi

Member
Sep 15, 2018
43
36
Hi wana JF

Naomba tuanze kulizungumzia swala hili leo ....

Wakati tathmini zinaonyesha kuanzia mika ya 80 kurudi nyuma ndoa 15% tu ndio zilionekana kuwa mmoja ya wanandoa alibaki pekeyake kwa kufiwa na mweza wake ,lkn 80-95 iliongezeka mpk kufikia 27% ambapo kuna ambao walidai talaka na wengine kufiwa na wenzi wao,

Ilipofikia mwaka 96- mambo yalizidi kubadilika na mpk kufika 31% ,

Mwaka wa 2000 mambo yamefikia 42% vijana wakiingia kwenye ndoa hawachukui round wanaachana ,hv Tatizo ni nini haswa au nani ana kua na shida? Nani anakua na shida kati ya hawa wawili ?


*Jibu*

Vijana tumekua tunaishi kwa mazoea au wazazi upande wa kikeni hawawafundishi watt wao wa kike kuishi na ndoa au mahusiano yao au kinyume chake,

a)Wasichana hawajui chakufanya na wameendekeza usasa hata wakiwa penuni (6x6)

b)Vijana wameishiwa mbinu ya matunzo na matulizo wa wenza wao wanaowapata (pumzi ndogo 6x6 ) so hatuwarudhishi ipasavyo..

c)au tukiingia kwenye mahusiano tunachukuliana kawaida na tunakua tumezoeana..

-Acha niwape siri vijana -

Kutokana na lindi na utandawazi lililopo bora ukipata msichana/mvulana na ukagundua kuna baadhi ya mambo hawezi ,bora ukamfunza km unayajua (ila tu uwe unampenda kweli)

Na wewe utakaefundishwa wala usijiskie vbaya coz hakuna aliezaliwa anajua mambo yote so vumilia tu mpk utakapojua kufanya hayo ambayo anataka mwenza wako ,hayo ndo huitwa mapenz hata babu na bibi zetu walikua wanafanya hvyo na ndo maana ndoa zao zilikua zinakaa mda mrefu pia,
Na nyie waschana punguzeni midomo na usasa mwingi mtakuja kujikuta mnafeli kwenye kila jambo...



Mfano: unakuta mchana kweli mzuri na karembeka sio haba,kafunga kucha au kabandika kucha mikono yote na ni ndefu "hebu nambie anajisafisha vip huyu sehem zake za siri?"

Kingine kujichubua -sawa hatukatai unakua mzuri kwa sura na umbo hata ukilitia mchina sawa lkn je "uliwah kujipeleka miaka 15 mbele na ukajiona utakuaje ?" Hata huyo mwanaume utakaekua nae unadhani atavutiwa na wewe baada ya kuwa nasura iliyochakaa au kuharibika ...


Ni mtazamo tu jmn -



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyakati hizi ndoa zikidumu basi ni Mungu kaweka mkono wake tu, Maana ushindani umekua mkubwa siku hizi hakuna mtu wakusubiri nyumbani mwingine akatafute ugali, kila mmoja analeta pesa nyumbani sasa usitegemee kusiwe na migogoro, ubishani majigambo na dharau nk kaza buti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa zinazokufa ukiangalia back-ground yake utagundua nyingi zilikuwa na "mihemko"..Upendo haukua pamoja nao ndio maana hawachukui muda utakuta wamebwagana tena vibaya vagalanti'

Vijana tunatakiwa kutuliza akili saaana na kufanya maamuzi ya busara kwenye mambo nyeti kama haya,.
Unadhani mfumo wa kuchaguliwa mke/mume na wazazi uendelee kwasababu hatujui tabia za familia ambazo tunakwenda kutoa/kuolewa nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa nini? Kwa nini unataka kuolewa/kwa nini unataka kuoa.
Ndoa ime_contain vitu vingi mno

Mahaba
Uvimilivu
Ujali
Ustahimilivu
Masikilizano
Undungu wa wawili
Utimilivu wa haja kwa wakat
Urafiki
N.k

Wengi huoa au kuolewa kwasababu km hizi

a)fulan kaolewa na mm pia nataka
b)umri umefika so hakuna namna lazma niolewe/nioe
C)au unaoa ama kuolewa ili umkomoe fulan au umuonyeshe jinsi sherehe yako itavyokua
D) kuoa/kuolewa kwa kufuata Mali
Na mengineyo mengi mno.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanaachana kwa sababu wanapendana! kwenye ndoa anayetakiwa kuwa na upendo ni mmoja tu sio wote
wanaachana kwa sababu hawajui kutofautisha mahaba sirini na upendo hadharani
 
Back
Top Bottom