Kwanini ndege haiwezi kurudi nyuma mpaka isukumwe?

bbc

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
3,836
4,145
WanaJF,

Mara zote nimeona ndege ikitaka kurudi nyuma mpaka isukumwe, haiwezi kurudi kinyumenyume, hivi kwanini ilitengenezwa hivyo kwamba isiweze kurudi kama yafanyavyo magari?
 
ndege inatumia injini zake kujipeleka mbele kwa kukusanya hewa mbele na kuleta nyuma ili yenyewe ipate force ya kwenda mbele.. sasa ukitaka irudi nyuma inamaa injini ziangalie nyuma! ambapo hata ww unaona kbs jambo hilo si jepesi nafikiri wameonelea vyema kufanya hivyo kutokana na muundo wa ndege zilivyo
 
Baadhi zina uwezo wa kurudi. Kuna wakati nilipanda Flightlink kwenda Mgololo airstrip Iringa, ilirudi reverse, Ni kitu ambacho nilikua sijawahi kuona maishani mwangu!
 
ndege inatumia injini zake kujipeleka mbele kwa kukusanya hewa mbele na kuleta nyuma ili yenyewe ipate force ya kwenda mbele.. sasa ukitaka irudi nyuma inamaa injini ziangalie nyuma! ambapo hata ww unaona kbs jambo hilo si jepesi nafikiri wameonelea vyema kufanya hivyo kutokana na muundo wa ndege zilivyo

Ilitengenezwa isirudi nyuma kwakuwa hata dunia nayo hairudi nyuma bali siku zote inakwenda mbele.
 
WanaJF,

Mara zote nimeona ndege ikitaka kurudi nyuma mpaka isukumwe, haiwezi kurudi kinyumenyume, hivi kwanini ilitengenezwa hivyo kwamba isiweze kurudi kama yafanyavyo magari?
Siyo zote mkuu
 
  • Thanks
Reactions: bbc
Ona hii
Na zingine zipo pia. Labda wataalamu wa aviation waeleze

angalia vizuri huyo mwenye kamera yupo kwenye gari ambayo ilikuwa inaisukuma hiyo ndege kurudi nyuma angalia mpk mwisho
 
Suali zito mno lakini utapata majibu mujarabu..!

Ngoja nimwite mtaalamu sasa hivi..!
 
Back
Top Bottom