Kwanini nakala ya vyeti vya ndoa ni mbili?

Kwanini nakala ya vyeti vya ndoa ni mbili?

Bahati yangu

Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
30
Reaction score
7
Kama kufunga ndoa ni kuwa mwili mmoja?kwanini nakala ya vyeti hapa kwetu hutolewa mbili,nimefuatilia kwa wenzetu Kenya hutoa nakala moja,pia Nigeria hutoa nakala moja.Kwanini hapa kwetu hutoa mbili,mwenye uelewa mpana naomba anisaidie.
 
kimoja cha wife...kingine cha mume...hata mume/ke ikitokea mkwaruzano na mmoja wapo akaharibu cha kwake na kubatilisha uwepo wa ndoa, mwingine bado anao ushahidi wa uwepo wa ndoa hiyo
 
Swali zuri! Ngoja wataalamu wa sheria za ndoa wafike watakujibu wanakula sahii!!
 
Mbona jibu la swali lako rahisi sana ntakujibu kwa kukuuliza swali, kwani wanapofunga ndoa wanafunga wangapi??
 
Mbona jibu la swali lako rahisi sana ntakujibu kwa kukuuliza swali, kwani wanapofunga ndoa wanafunga wangapi??

ningekuwa mimi ndo Bahati yangu ningekuchapa swali la nyongeza: kwani huko kenya na kwingineko wanafunga ndoa wangapi wangapi!
 
Last edited by a moderator:
Usijali wanakuja kukupa majibu na mimi nawasubiri hao hao,kama kweli umefanya utafiti huko kote wanatoa cheti kimoja lazima kuna sababu tu kwanini hapa kwetu wanatoa viwili!
 
Kama kufunga ndoa ni kuwa mwili mmoja?kwanini nakala ya vyeti hapa kwetu hutolewa mbili,nimefuatilia kwa wenzetu Kenya hutoa nakala moja,pia Nigeria hutoa nakala moja.Kwanini hapa kwetu hutoa mbili,mwenye uelewa mpana naomba anisaidie.

Huko kenya na kwengineko ndio wanaokosea na hapa kwetu tz ndo tunao patia kwa kutoa nakala mbili kwakua wahusika ni wawili
 
Nakala moja ya Mr. nakala nyingine ya Mrs. na book copy inabaki kwa mfungisha ndoa. Katika maisha lolote linaweza kutokea. Wafunga ndoa wanakuwa mwili mmoja lakini ukweli ni vichwa viwili tofauti ndio maana kunakuwepo kusalitiana.
 
Back
Top Bottom