Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Si kila mcha Mungu lazima awe Mtakatifu kwa kutangazwa. Wengine tunajua fika kwa walivyokuwa na mambo waliyo ya dhihirisha wana sifa ya kuwa watakatifu mbinguni lakini hawakutangazwa Duniani.
Ukifatilia historia ya Kanisa Katoliki, wapo wengi tu ni watakatifu. Wapo Mapdre na Masista walifanya mengi sana yana udhihirisho lakini hakuna aliyetangazwa Mtakatifu hapa Duniani. Ingelikuwa ni hivyo hata Hayati Kadinari Rugambwa angetangazwa Mtakatifu, lakini sio hivyo.
Sio kila anayekuwa Mtawala akiwa ni mcha Mungu au MTU WA ibada basi akifa amepata sifa ya kuwa Mtakatifu? Hakuna kitu kama hicho. Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia.
Kwanza kuna hatua za mapitio ya maisha yako, pili ukabili WA changamoto kabla hujawa mtawala na baada ya kuwa mtawala, taarifa za Kimungu na uchaji wako, utumishi WA Mungu rohoni mwako yaani sio lazima uwe Padre ndio uwe mtumishi. Je ulitumiaje Urais wako kama Mtumishi wa Mungu(kasisi wa Nchi rohoni)? Je katika utawala wako hakuna watu uliowaonea? Au kama ulisamehe, Je hakuna watu uliowaacha katika mazingira magumu ndani ya utawala wako tena wakiwa hawana makosa na wakaendelea kuumia kwa shinikizo lako katika utawala mwingine? Mfano unamuweka MTU Vizuizini kisa kaongea Ukweli halafu unaachia madaraka unakuwa mcha Mungu na huyo MTU au hao watu bado wako Vizuizini kwasababu yako. Hapo hakuna Mtakatifu ni maigizo tu.
Wakati mwingine sheria za nchi za Vizuizi zinaweza kuathiri utakatifu wa MTU kama yeye mwenyewe hakufanya bila kufikiria. Je, katika utawala wako umenyonga wangapi? Na umetubu hadharani Mara ngapi jamii ikajua kuwa ulisaini kunyonga? Umeagiza Mara ngapi watu wawekwe gerezani bila hatia, wale wenye hatia hawahesabiki.
Kusali Rozari au Kufunga sio Sifa ya kuwa Mtakatifu kwakuwa kama binadamu tunajua kuna mahali unaweza kujikwaa.
Na ndio maana ukifa kama mtawala na tunajua ulikuwa mcha Mungu, tunaangalia yote uliyoyafanya kwanza katika mabaya na Yale mema, na pale ulipoamua kumcha Mungu sawa sawa. Ndipo ili tuhakikishe tunahitaji kupata miujiza ama kwenye kaburi lako au kwenye mwili wako au picha zako au mabaki yako au imani ya watu kwako itakayowapa uponyaji wa mwili au roho. Matukio kama haya ndio yanaweza kukupa Utakatifu.
Padre Pio pamoja na kutenda miujiza mingi akiwa hai, pamoja na kupata madonda Matakatifu ya Yesu lakini hakutangazwa Mtakatifu kwa ghafla. Ililazimika tena kuhakikisha kama kweli ana faa kuwa Mtakatifu kwa kutumia mabaki yake, picha zake, kaburi lake n.k ili kuona kama kuna uponyaji unaweza kutokea, wengi walipata uponyaji nikiwemo Mimi Deogratius Kisandu ambaye nimekuwa natembea na picha yake tangu mwaka 1998 akiwa bado hatua za mbarikiwa na mpaka anatangazwa mwenye heri na kuwa Mtakatifu.
Tunapopitia mapitio ya kutaka Julius Kabarage Nyerere kuwa Mtakatifu lazima tukubali akosolewe yote ya nyuma mabaya na mazuri, na mapito yake yalimsaidiaje kumbadilisha na kuwa kiumbe safi cha Mungu, tatizo letu watu hawataki Nyerer e akosolewe wanataka atangazwe Mtakatifu tu? Tutahakikishaje kama hatuna taarifa zake za kiroho? Nani kapata uponyaji kutokana na maombezi yake au kaburi lake au mwili wake au picha zake?
Kuna miujiza mikuu inayosadifu kiongozi kutangazwa Mtakatifu na sio sifa za kujitakia. Wapo Mapapa ndani ya kanisa mpaka Leo hawajawahi kutangazwa watakatifu, hapo ndio ujue swala la kiroho linahitaji ushuhuda mkuu na sio kupachikana utakatifu.
Leo ukiambiwa Padre Ricardo Maria wa ndugu wadogo wa Afrika Morogoro Mr. Pekupeku kwa kazi na matendo yake kwa jamii na maisha anayoishi ya kifukara lakini watu ukiwauliza wanakuambia huyu atakuwa mtakatifu, ni kweli kabisa lakini bado swala la uchunguzi wa kiroho litafata kama litaleta ushuhuda ili aweze kutangazwa mtakatifu Duniani.
Nyerere ni lazima akosolewe na historia yake ya Utumishi wa Mungu kama kiongozi lazima ijulikane hadharani ili hata wengine waweze kuiga na kufata nyayo zake. Mnapozuia kumkosoa Mapito yake munazuia pia miujiza kutendeka ili kupata udhihirisho wake wa kuwa Mtakatifu.
Kila binadamu ana Mapito yake. Wengine wanamapito mabovu sana lakini yamesaidia kuwakomaza wengine na kuwa wauumini wazuri au watawa wazuri au wacha Mungu wazuri.
Tunaweza kuungana Kumuombea kwa Mungu ili atangazwe mtakatifu hapa Duniani lakini lazima mazuri na mabaya aliyoyafanya yajulikane hadharani na jinsi alivyomgeukia Mungu, na sio kimya kimya. Swala la Mungu halifichiki hata uwe Rais lazima ufate njia zake na ukweli lazima ujulikane ili watu wawe huru kumuombea, na hata miujiza unaweza kutokea.
Kipindi ambacho watu ndio wanahoji sana ndipo miujiza hutokea ili kuwanyamazisha. Na ndivyo kazi ya Mungu inavyotaka ili kuwaumbua maadui.
Kwa kuwa Tanzania hatujawahi kupata Mtakatifu wa kutangazwa basi tusilazimishe ili tupate sifa ya kuwa na Mtakatifu. Watakatifu wapo wengi tu hapa Tanzania sema hatuna tabia za ufatiliaji. Wapo watakatifu wafiadini ndani ya makanisa lakini wamefichwa.
Hivyo tujipange upya na tukubali changamoto za Nyerere kuwa mtakatifu zitusaidie katika kupata ushuhuda sahihi.
Tuanze mwaka mpya kwa matendo mema.
Ndimi:
Deogratius Nalimi Kisandu
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
6 Januari 2017.