Kwanini mvua hainyeshi vizuri?

Lendomz

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
446
381
Kuna watu wa hovyo kabisa nimekuwa nikisoma humu JF wanahusisha baadhi ya watu kuwa ndio wanaosababisha mvua isinyeshe.

Wanasahau haya hapa chini;
1.Kuna uharibifu wa mazingira tena wa makusudi. Unaambiwa usilime karibu na chanzo cha Maji wewe unalima eneo hilo halafu eti rais kasababisha mvua isinyeshe hovyo kabisa.

2.Unaambiwa usikate miti hovyo wewe unakata miti hovyo.

3.Kazi ya viongozi wa dini ni kumwomba Mungu atutendee mema ikiwemo kutupa mvua ya vuli na masika! Sasa viongozi wetu ( siyo wote) wanajihusisha na madawa ya kulevya, wameingia kwenye siasa ambayo ni mchezo mchafu,wanapokea rushwa, wengine wanakesi za ubakaji, mashoga wamejaa humo makanisani, waumini wanatoa mimba na kufanya mambo ya hovyo, albino wameuwawa hovyo kipindi cha nyuma, Mungu asikasirike kweli na kutunyima mvua? Halafu lofa linakuja eti rais kasabisha mvua isinyeshe! Hovyo kabisa!

4.Taifa limejaa wanasiasa uchwara wasioheshimu mamlaka iliyowekwa na wengine kujifanya wanaota ndoto za hovyo kabisa wakati wana ajenda asili ya kumdhuru rais wetu halafu eti Mungu akupe mvua ya vuli na masika?

5.Shetani daima hawatakii mema wanadamu! Anaweza kuzuia mvua isinyeshe.

Sasa basi tujichunguze na kuacha maovu. Waombaji tutubu na kuanza kumwomba Mungu, yeye ni wa Rehema ataturehemu na kutupa mvua, tutii mamlaka iliyowekwa, tuwaombee viongozi wetu rais, serikali, mawaziri, wabunge, madiwani, RCna ma DC ili Mungu awape hekima na maarifa katika kuliongoza taifa letu na kutuletea maendeleo kwa ajiri yetu na watoto wetu na watoto wa watoto wetu!

Amina
 
Kuna maeneo yanapewa mvua ila sehemu ambazo kuna wapinzani ni bajeti ya mvua hakuna ( ) akili yangu imefika mwisho.

Usikurupuke lakini.
 
Kuna watu wa hovyo kabisa nimekuwa nikisoma humu JF wanamsingizia rais wetu Mpendwa eti ndiye anayesababisha mvua isinyeshe!!! Wanasahau haya hapa chini
1.kuna uharibifu wa mazingira tena wa makusudi!! Unaambiwa usilime karibu na chanzo cha Maji wewe unalima eneo hilo halafu eti rais kasababisha mvua isinyeshe!! Hovyo kabisa!!

2.unaambiwa usikate miti hovyo wewe unakata miti hovyo halafu unasema eti rais amesababisha mvua isinyeshe!!! Una akili kweli?

3.Kazi ya viongozi wa dini ni kumwomba Mungu atutendee mema ikiwemo kutupa mvua ya vuli na masika!! Sasa viongozi wetu ( siyo wote) wanajihusisha na madawa ya kulevya, wameingia kwenye siasa ambayo ni mchezo mchafu,wanapokea rushwa ,wengine wanakesi za ubakaji, mashoga wamejaa humo makanisani,wwaumini wanatoa mimba na kufanya mambo ya hovyo,albino wameuwawa hovyo kipindi cha nyuma,........Mungu asikasirike kweli na kutunyima mvua??? Halafu lofa linakuja eti rais kasabisha mvua isinyeshe!! Hovyo kabisa!!

4.Taifa limejaa wanasiasa uchwara wasioheshimu mamlaka iliyowekwa na wengine kujifanya wanaota ndoto za hovyo kabisa wakati wana ajenda asili ya kumdhuru rais wetu halafu eti Mungu akupe mvua ya vuli na masika??

5.Shetani daima hawatakii mema wanadamu!! Anaweza kuzuia mvua isinyeshe!!!



Sasa basi tujichunguze na kuacha maovu !! Waombaji tutubu na kuanza kumwomba Mungu !! Yeye ni wa Rehema ataturehemu na kutupa mvua!! Tutii mamlaka iliyiwekwa!! Tuwaombee viongozi wetu rais,serikali ,mawaziri,wabunge,madiwani,RCna ma DC ili Mungu awape hekima na maarifa katika kuliongoza taifa letu na kutuletea maendeleo kwa ajiri yetu na watoto wetu na watoto wa watoto wetu!!!Amina

By the way...hapo namba tano!! Je yule aliyesema anata matajiri waishi kama mashetani na yeye ni shetani??? Maana hawatakii mema wanadamu wenzake pia!!
 
umesahau kauli mbiu yake "hapa kazi tu" akimaanisha kazi za ofisini tu, akasahau kuna kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara.
 
By the way...hapo namba tano!! Je yule aliyesema anata matajiri waishi kama mashetani na yeye ni shetani??? Maana hawatakii mema wanadamu wenzake pia!!
Hapo ndipo alipomaliza maombi yake,
Sasa maombi yanafanya kazi no mvua no what sote tutaishi kama mashetani.
Mdomo huumba
 
hii ni application ya uteuzi sioni sababu ya kutunga huu ...., kama siyo kum-lure mteuaji
 
..nyie mnaoleta thread hizi ndio mna lenu...sasa ngoja muambiwe....juzi amerudi mvua imekata...wakati ilishaanza kunyesha aliposafiri nje briefly...dhambi hii tumejichumia wenyewe kwenye uchaguzi wa 2015...na kukosa mvua ni sehemu ya Mungu kutuonyesha....at least ushahidi wa kimazingira unaonyesha hivyo...hata sala zetu nyingi huko makanisani ni za kinafiki...
 
We should ask the sky spirits, may be they need some kind of sacrifice
 
Back
Top Bottom