Kwanini Mungu Ibariki Afrika kwanza na Si Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Mungu Ibariki Afrika kwanza na Si Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichankuli, Mar 27, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Wandau wa JF, mara nyingi huwa tunasisitizana kutanguliza uzalendo mbele katika mambo mbalimbali tunayoyatenda. Mojawapo ya vitambulisho vya uzalendo na utaifa wa mtu ni wimbo wa Taifa lake. Hoja yangu kwa wadau, kwa nini sisi Watanzania wimbo wetu wa Taifa uendelee kuanza na Mungu Ibariki Afrika badala ya Mungu Ibariki Tanzania. Wengine watasema kwamba, ni namna moja wapo ya kumuenzi Mwalimu JK ambaye wakati ule, pamoja na wenzake akina kwame Nkuruma, walikuwa na fikra za kuwa na Afrika moja. Imeshapita zaidi ya miaka arobaini sasa tangu nchi za Kiafrika zianze kujipatia uhuru, na Afrika moja imekuwa ni njozi, badala yake kuna Taasisi ambazo zinaundwa na kutuongezea gharama zisizo za lazima, kama hili Bunge la Afrika, au Afrika Mashariki.

  Nadhani kuna haja ya kubadili mpangilio wa wimbo wetu wa Taifa ili uanze na Mungu Ibariki Tanzania halafu ndo ifuate Mungu Ibariki Afrika.

  Natoa hoja kwa Mjadala
   
 2. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Mwalimu JK alikuwa na upeo wa mbali sana. Na itafika siku moja wazo lake la kuiweka Africa mbele ikaonekana. Ndio sababu katika kutengeneza wimbo wa taifa akaagiza iwe Mungu Ibariki Afrika kabla Mubgu Ibariki Tanzania.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Afrika ni mama yangu, asili yangu na nchi yangu.
  Tanzania ni gereza langu
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mzee kwani kuna ubaya gani ikitangulia Afrika?labda ungeeleza madhara ya kuanza kwa Frika katika wimbo huo kwani kwa maoni yangu huwa nashangaa kwanini iliongezwa sehemu ya Tanzania kwa sababu sehemu ya kwanza ya Afrika ina cover na Tanzania pia. Yaani Mungu akiibariki Afrika ndi atakuwa ameibariki na Tanzania pia. Kwa maoni yangu sehemu ya Tanzania haina maana ni marudio yasiyo ya lazima.

  Mzee historia ya wimbo huu haikuanzia Tanzania, sababu ya Tanzania kutumia wimbo huu ni fikra zilizokuwepo wakati huo za kuwa na nchi moja ya Afrika na wimbo huo(Nkhosi Sikeleli) uwe ni wimbo wa taifa la Afrika. Hii ndio sababu nchi kadhaa za Afrika zinatumia wimbo huu mfano, Zambia, SA.
  Nadhani katika hali hii ya leo ambapo bara letu linasakamwa na majanga makubwa kama vita, njaa, umasiki, matatizo ya utawala mbovu na uongozi, tunahitaji kufikiria ni jinsi gani tunaweza kuunganisha juhudi zetu kujimboa badala ya kufikiria nchi zetu kwanza.
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kiukweli Nyerere Ni Nuru ya bara la afrika. Na aitabakai ahivyo!!

  Tanzania ni chimbuko la Nuru hiyo.

  Kwenye sala tunaanza na kwa kuwa General na tunamalizia na kuwa sepecific.

  Mara nyingi tunajieleza hivyo pia kwenye maandishi , mihadhara nk.
   
Loading...