Ngurubhe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,840
- 1,048
Habari waungwana!!...
Najua wapo wasanii ambao walishaamua kuwa upande fulani,na hata anaefuata kazi zake atakuwa tayari anajua kuwa wewe ni chama fulani,nitolee mfano wa marehemu Komba,(mwenyezi Mungu airehemu roho yake) huyu aliamua kukitumikia chama,na hata alichokipata aliridhika nacho kwa sababu alijua kinatokana na kodi za wanachama na wanaompenda yeye na uimbaji wake.
Wasanii wa film,bongo-flavour nk wa kibongo wamekuwa hawaeleweki,mara leo huku kesho kule.
Msanii kama Kanumba(Mungu airehemu roho yake),hakuwahi kuonesha mapenzi na chama chochote cha siasa.HIVYO ALIWAUNGANISHA WATU...na kazi zake ziliuza sana..
Mbongo movie ukiachilia watu kutonunua kazi zao kwa sababu kadhaa lakini mimi NAAMINI KUJIHUSISHA NA SIASA NI MOJA YA SABABU tena kubwa tu.NYIE NI KIOO CHA JAMII..HAMTAKIWI KUWAGAWA MASHABIKI WENU..
MKUMUMBUKE KUANGALIA MOVIE kunahitaji,muda,mood,hisia na mapenzi juu ya muigizaji vilivile...sasa wewe uko busy na mambo ya vyama nani atanunua kazi yako? ,kama unataka kuwa busy na mambo ya chama mambo yataenda tu
USHAURI: JIEPUSHENI NA SIASA ,MASIRAHI YA MUDA MFUPI YANAKUPA SHIDA ZA MUDA MREFU.MTAHANGAIKA SANA NA FILM ZA NJE tatizo sio film za nje tatizo lipo kwenu wenyewe.
Mbona watu wanampenda kuku wa kienyeji pamoja na kuwa ni wa ndani? Na kuku wa kisasa hapendwi na bei rahisi pamoja na kuwa asili yake ni nje? .."ushauri tu"...