Kwanini msafara wa gari za CHADEMA huamsha watu sana?

Kwanini msafara wa gari za CHADEMA huamsha watu sana?

Kwanza umeandika kwa mapenzi wawea kuwa mfuasi wa CDM lakin pamoja na hiyo CHADEMA hupaswi kuibeza ina wafuasi zaidi ya milion 3 nchi nzima hivyo lazima iwe tofauti na ACT CUF NLD na vyama vingine, ila bado haijawa na wafuasi kama CCM chama chenye wafuai kila kona ya nchi kila upande wa wilaya kila upande wa kata na kijiji,

Lakini pia maeneo uliyoyataja ya wafuasi ulipouliza au uliposikia wakisema wanawasubiri CDM ni wale wasiokuwa na kazi waliokata tamaa na CCM wanaosubiria mabadiliko kutoka kwenye vyama bila wao kujishughulisha kufanya kazi,
Hujui wasio kua na kazi ndio wengi tz,hata hao wenye kazi sio kwamba zinawatosheleza ni unga unga tu kwa gundi mjini,usiwabeze!...
 
Leo nimepita mitaa fulani nimepishana na fordranger M4C mbili, na dinga 4 nyingine ikiwemo ya KUB. Hakika nikaona watu wanaulizana na kushangaaa. nikamsikia mkaka anasema hawa jamaa hatari sana. nikamuuliza kivipi, kajibu tunawakubali sana na tunawasubiri.

Nimepita soko kuu nakuta bodaboda wanazungumzia kuwamiss chadema sana. naamini wataporuhusu siasa za majukwaani.

Naomba mwenye picha ya zile gari M4C atuwekee hapa, hupendeza kuziona tu.
Yani nilikuwa katikati ya jiji Fulani wiki ilopita ikapita M4C na bendera nyuma watu ni full miluzi wanashangilia."weka silaha chini tubishane Kwa hoja"

TUME HURU, TUME HURU
 
Chadema inapofanya operation zake, inaamshaamsha, hapo serikali inapata nafasi ya kuona wapi inakosea. Lakini kutowapa jukwaa la kisiasa kunarudisha nyuma harakati za maendeleo. Nitakupa mfano mdogo, kama Chadema wangekuwa jukwaani kwa muda mrefu, vijana wengi wangepata ajira na stahiki za watumishi zingelipwa kwa asilimia kubwa.
 
Jibu ni rahisi sana tu
Ni Kwa sababu CHADEMA ni chama kinacho wajali wananchi
Leo nimepita mitaa fulani nimepishana na fordranger M4C mbili, na dinga 4 nyingine ikiwemo ya KUB. Hakika nikaona watu wanaulizana na kushangaaa. nikamsikia mkaka anasema hawa jamaa hatari sana. nikamuuliza kivipi, kajibu tunawakubali sana na tunawasubiri.

Nimepita soko kuu nakuta bodaboda wanazungumzia kuwamiss chadema sana. naamini wataporuhusu siasa za majukwaani.

Naomba mwenye picha ya zile gari M4C atuwekee hapa, hupendeza kuziona tu.
 
Saccos ni CCM
Chadema Ni Chama au Saccos???[emoji3][emoji3][emoji3]
FB_IMG_1555773311437.jpeg
 
Yaani lile katazo la kuonyesha bunge laivu limeokoa maisha ya watu wengi. Kulikuwa na hatari ya kugongwa na magari maana kila wakisikia mbunge wa CHADEMA anachangia hoja kila mtu anakimbilia kwenye TV ambazo nyingi ziponkwenye maduka na sehemu za biashara.

Itokee achangie Mh Lissu ndo ilikuwa patashika.

Kwa kweli CHADEMA tumewamiss sana. Haswa majukwaani.
 
Back
Top Bottom