Kwanini movie za kikorea zimekamata Tanzania?

Ally maganga

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,433
909
Hili swala huwa linanisumbua sana, hivi bongo movie walikosea wapi mpaka hawa wakorea wameteka soko.
Kuanzia Nyumbani, kwenye usafiri, vibanda umiza kote ni Korean drama. Popote kwenye Tv na deki lazima pembeni utakuta movie ya kikorea.
Wabongo mpo wapi?
 
Umeanza vizuriiii hapo mwisho tu ndyo Umeboa kumkashifu wema japo ni kweli kuwa huwa anaachia makalio yake.

Bongo movie ikianza ikifika katikati mtu unajua kabisa itaishaje, nani atamuoa nan ndani ya move tofauti na za kikorea huwezi kutabiri na ukitabil au ufikiriacho kitakuwa kinakuwa tofauti.
 
Niliwahi dokezwa Rais wao mmoja aliyepita aliamua na kuhamasisha kuwekeza kwenye uiguzaji wa filamu ili wa export nje ya nchi .
Na ukiangalia baadhi ya stori nyengine tulizisoma kwenye vile vitabu vyetu vya zamani vya primary.
 
Hili swala huwa linanisumbua sana,
hivi bongo movie walikosea wapi mpaka hawa wakorea wameteka soko.
Kuanzia Nyumbani, kwenye usafiri, vibanda umiza kote ni Korean drama.
Popote kwenye Tv na deki lazima pembeni utakuta movie ya kikorea.
Wabongo mpo wapi?
Dada Wema kabaki kuchezesha matako tu!
Korea wamejipanga sana kuanzia waigizaji wako vizuri na vipaji vyao pamoja na teknolojia wanaenda nayo katika sanaa, bongo muvi ubunifu uko chini hivyo muvi zao kukosa ubora
 
Sijui kwanini wapenzi wengi Wa hizo muvi huwa ni akili ndgo hvi....
Tena unakuta zimetafsiriwa kwa kiswahili.
Nina library ya muvi ipo uswahilini, nina muvi seasons zilizotafsriwa na zisizotafsiriwa.

Huku uswahilini ni watu wachache sana watatazama zisizotafsriwa (binafsi pia siangalii zilizotafsiriwa) lakini kuna maeneo wana hizo ambazo hazijatafsriwa mfano Sinza kwa jamaa anajiita Torrent na Mkwajuni.

Kila jumatatu muendelezo wa hizi seasons unatoka. Kwa maeneo ambayo wanauziwa elfu mbili na kukodishiwa kwa elfu moja mfano Mbagala na Koma Koma mtu wa eneo hilo ana uhakika wa kutengeneza elfu themanini mpaka laki moja kwa siku hiyo.

Maeneo mengine haitatengenezwa chini ya elfu hamsini, katika siku nyingine za kawaida, kuna uhakika wa kuitengeneza kuanzia elfu thelathini mpaka hamsini.

Kuna wanafunzi wa IFM nahisi Masters sikuwauliza vizuri wamejiajiri kwenye kutafsiri hizi seasons, akitafsri ile moja master ya hiyo season anaiuza laki mbili mpaka tatu, sasa wazia ametafsri season nne na kila jumatatu anamuuzia master mmiliki wa duka.

Graduates tunasurvive kwa mchezo huo tafadhali usiwaite wateja wetu wana akili ndogo.
 
Kuna matangazo ya action movies za kibongo nimeyaona kuna moja inaitwa Ulingo wa Moto nyingine inaitwa Ajenti Bava au Bavo kama sikosei, wakuu action za mule ndani Boyka huyu hapa.

Zikitoka lazima nizicheki, nahisi sasa ndiyo tunabadilika pole pole.
 
Nina library ya muvi ipo uswahilini, nina muvi seasons zilizotafsriwa na zisizotafsiriwa.

Huku uswahilini ni watu wachache sana watatazama zisizotafsriwa (binafsi pia siangalii zilizotafsiriwa) lakini kuna maeneo wana hizo ambazo hazijatafsriwa mfano Sinza kwa jamaa anajiita Torrent na Mkwajuni.

Kila jumatatu muendelezo wa hizi seasons unatoka. Kwa maeneo ambayo wanauziwa elfu mbili na kukodishiwa kwa elfu moja mfano Mbagala na Koma Koma mtu wa eneo hilo ana uhakika wa kutengeneza elfu themanini mpaka laki moja kwa siku hiyo.

Maeneo mengine haitatengenezwa chini ya elfu hamsini, katika siku nyingine za kawaida, kuna uhakika wa kuitengeneza kuanzia elfu thelathini mpaka hamsini.

Kuna wanafunzi wa IFM nahisi Masters sikuwauliza vizuri wamejiajiri kwenye kutafsiri hizi seasons, akitafsri ile moja master ya hiyo season anaiuza laki mbili mpaka tatu, sasa wazia ametafsri season nne na kila jumatatu anamuuzia master mmiliki wa duka.

Graduates tunasurvive kwa mchezo huo tafadhali usiwaite wateja wetu wana akili ndogo.
Utaisaidia polisi si mda.. Huo ni ujambaxi na wizi uliotukuka.
 
Sijui kwanini wapenzi wengi Wa hizo muvi huwa ni akili ndgo hvi....
Tena unakuta zimetafsiriwa kwa kiswahili.
Huo ni mtazamo wako mkuu.
Ila ukweli utabaki pale pale movie za kikorea ni bora pia unaweza kuangalia Hata na familia pia yaani baba, mama, watoto hadi wajukuu kwa pamoja tofauti na movie za kimarekani au kibongo.
 
Kutoka moyoni mwangu, ukinunua series/muvi za kikorea kamwe hautajuta kutoa hela yako na utaona kama umepewa bure.

Kazi zao nzuri sana na zinamvuto plus zinaridhisha kuziangalia.

Ila pongezi ziende kwa ITV -TANZANIA maana wao ndio walikuwa watu wa kwanza kutuonesha utamu wa muvi/series za kikorea kupitia siries pendwa kuliko zote za JUMONG.
 
Wakorea wanawwza bana..unaangalia series hauishi hamu

Kuna tamthilia ya kibongo nlifanikiwa kuiangalia nilichoka tu pale mwanafunzi wa chuo alipopata mimba akafukuzwa..kilichofuata ni kuzima Tv na kulala
 
Back
Top Bottom