Kwanini mourinho aliondoka chelsea!!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini mourinho aliondoka chelsea!!?

Discussion in 'Sports' started by K007, Feb 28, 2011.

 1. K

  K007 Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamii! Mimi hadi leo nashindwa kuelewa sababu za uhakika zilizopelekea Jose Mourinho kuondoka katika klabu ya Chelsea.

  Nasikia wengine wakisema bilionea Roman hakupenda sera za kung`ang`aniza ushindi badala ya kucheza soka safi kama Arsenal, wengine wakisema kocha huyo alikuwa akipangiwa kikosi, sasa nashindwa kuelewa sababu hasa ni nini.

  Kiukweli mimi ni shabiki mkubwa wa Chelsea na hadi sasa naona Mourinho ndiye aliyeweza kuipa mafanikio klabu hiyo,na hadi sasa mwenendo wa Chelsea sio mzuri kabisa.

  Mwenye kumbukumbu nzuri kuhusu kilichomuondoa kocha huyo anisaidie kujua hilo
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,834
  Likes Received: 2,306
  Trophy Points: 280
  Alishindwa kuelewana na owner wa Club hasa kwenye mambo yafuatayo:-

  - Alishindwa kuweka intertaining football - alisema huwezi ku implement intertaining football ukiwa na wachezaji kama Essien, Lampard na wakati huo Ballack akitoa sababu eti hao ni pysical players yaani usitegemee kupata omlet nzuri wakati una mayai mabovu. Kauli hii ndiyo ilimtoa straight forwad siku ile wachezaji wakiangalia sinema ya blues revolution huku kocha wao akitimuliwa usiku huo huo.

  - Aliifanya Chelsea kutopendwa - ikawa inaitwa Boring chelsea. hii ni matokeo yake ya kucheza mpira usiovutia
  - Alishindwa kupata best combination from players
  - Alijiona yeye ni juu zaidi na hawezi kuwa replaced.

  Mpira unaotakiwa sasa duniani ni mpira wa Kasi, pass fupi fupi na ambao unafurahisha - hakuna owner wa club anayependa kuona mpira wa kukimbizana, pass ndefu na ushindi - NO.

  Angalia timu kama Barca na Arsenal hasa ndiyo vinara wa mpira huo. na jaribu kufuatilia mpira wa Madrid ya Morinho uone tofauti ya uchezaji wake tangu aanze kuifundisha.

  Kifupi Jose M ni kocha mshindi tu kwa njia yoyote lakini kama unataka future ya Club usimpe kazi, Club si ushindi tu kuna mambo mengi.
   
 3. K

  K007 Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekubali FUSO niliwahi kusikia hilo lakini nilikuwa sina uhakika, nashukuru sana mkuu, pamoja!
   
Loading...