Kwanini Mods mmefuta maandiko yangu?

Status
Not open for further replies.

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2021
Posts
413
Reaction score
726
Mara kadhaa huwa naandika na kushauri juu ta tiba za mitishamba.Kwa maana ni jambo lililo damuni kwangu na ninapenda hata wengine wajifunze na waelewe.

Ajabu ni kuwa kuna wakati moderator mnaondoa maandiko hayo kama mlivyofanya kwa sasa.

Ninatoa malalamiko yangu kwenu kuwa,kama mwanachama wa jukwaa huru la JF ninaandika kwa kuzingatia kanuni,sheria na masharti mliyoweka/tuliyojiwekea humu.

Ninasikitika sana!
 
Kama wanafuta tena bila maelezo na wewe umefuata Kanuni basi wamekukosea sana (Au yalikuwa ni katika Mfumo wa Matangazo) wakati hayapo jukwaa la Matangazo..., Au unatumia mbinu / tiba ambazo hazijathibitishwa au zinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji ?

Vinginevyo kama unafuata kanuni watakuwa wamekukosea sana...,

Nashauri liletwe Jukwaa la Mahakama humu hili sisi kama watumiaji tuwe tuna-judge iwapo mods wanafanya Haki au Udikteta (Ikibidi kuwapiga BAN accordingly hata ya Sekunde)
 
Wameondoa bandiko gani?
Lini?

Kuwa muwazi usaidiwe.
 
Yaani uje humu kuhimiza watu watumie majani ambayo haijulikani ni sumu au ni tiba halafu Mods wakuangalie tu?
 
Maanduko yangu hayako katika mfumo wa matangazo na ninaelewa ni kuvunja kanuni,isipokuwa huwa ni maandiko yanayoelezea aina ya ugonjwa na mbadala wake kwa tiba za mitishamba..na mara nyingi huwa tunajadili na kubadilishana mawazo kulingana na uelewa wa kila mtu katika mambo hayo.

Maandiko haya yaliyofutwa yamedumu muda mrefu tu katika jukwaa la afya,na wao mods ndio huwa wanalocate huko,ajabu leo wameamua kuyafuta yote.

Kama ni kanuni kuvunja ivunjwe leo na andiko lina miezi 3-5 na wao ndio wamelielekez kwenda jukwaa la afya??

Wakati wanalocate kwenye jukwaa la afya muda wote huo hawakuona kama kumevunja kanuni?? Maana andiko linapokiuka kanuni hufutwa wakati huohuo.

Ndugu zangu kila mtu ana kitu apendacho maishani mwake,wengine siasa,mpira,mapenzi ,mambo ya tiba n.k.Kwa hiyo kila mtu hapa huandika apendacho kwa kuzingatia kanuni na sheria.

Tafadhali naomba mods mrudishe maandiko yangu kwa wale wapendao kujifunza wajifunze nami nijifunze kwao.

Mlichofanya ni uonevu,mimi ni mwanachama halali kama walivyo wengine wanaoandika habari za siasa na vita na wakati mwingine zisizo na uhakika.
 
Kama hivyo ndivyo basi wamekosea...,

Naomba sana warudishe bandiko lako nadhani watakuwa wamekosea kufuta kwa bahati mbaya..., au kama kuna mtu ameshitaki / ameomba lifutwe aje hapa aeleze ni kanuni zipi umevunja....

Wasipofanya hivyo mimi kama Mwanajamii mpenda haki nitakutetea bila gharama yoyote ili kuondokana na huu uporaji wa haki...., natumai ndani ya masaa machache watakuwa wamerudisha uzi wako na kukuomba msamaha....
 
Tatizo ni hilo jina lako, vikwazo kila mahali
 
Labda wameona kuna hitilafu sehemu
 
Soma mojawapo ya andiko langu la leo ambalo halijafutwa,then uone kama kuna hitilafu kwa mjibu wa kanuni!! Maandiko yangu mkuu ni aina ya maandiko hayo,nimeshangaa sana leo kufutwa yote.Hizi kanuni zote ninazisoma na kuzifuata.

Hata hivyo maandiko hayo yamekuwepo hapa JF kwa muda mrefu katika jukwaa la afya,iweje leo yafutwe yote??

Wamenionea sana!!
 
Huenda Machapisho yalikaa kimatangazo (sina uhakika na hilo) au uzi ulio leta unafanana na uzi ulio kuwepo kabla.

Hivyo kama kosa ni lakwanza uzi wako hufutwa ila kama kosa ni lapili uzi wako uliunganishwa.

Zaidi ya hapo labda Mhariri Moderator Active waje watupe mwongozo.
 
Salaam Mkuu.

Threads zako zinafutwa sababu Serikali hairuhusu matangazo ya Miti shamba na tiba Mbadala. Hivyo JamiiForums tunafuata Sheria na kanuni za Nchi.

Tunatumia nafasi hii kukutaka usirudie kuweka mabandiko ya Miti shamba na tiba mbadala bila kuonesha kibali kinachokuwezesha kufanya hivyo.

Asante.

Zaidi, soma:

1). Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili na tiba mbadala
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…