Waache mihemko wakati wenzao wanapiga noti
Ni kweli wanasimamia kila kitu ila tusiuze utu wetu, fikra zetu, na wanapokosea tusione haya kuwakosoa kisa tuko upande wao.Ndugu umepiga nondo zilizosimama hata mimi nakupa bigup. Sasa hebu tuambie nini kifanyike maana hakuna chochote utakakachofanya nchi hii bila ruhusa ya mwanasiasa. Hakuna uwezekano wa wewe kufanya mradi mkubwa bila mwanasiasa kutia baraka zake. Kila kitengo cha maamuzi katika nchi hii kinapata uamuzi wa mwanasiasa penda usipende. Unapoona wengi wanaamini wanasiasa, sio kweli kwamba wanawaamini bali wengi wanatarajia mwanasiasa fulani akipata madaraka na yeye atatoka kimaisha. Wananchi wengine wao hawana wajualo zaidi ya kuuziwa matangazo ya maisha bora, ni kabila langu, ni dini yangu nk na wanasiasa hapo wanageuza siasa kuwa mechi ya simba na yanga. Hebu tuambie tufuate mfumo gani maana hata kodi zetu zikikusanywa wanasiasa ndio wanapanga vipaombele.
Ni kweli wanasimamia kila kitu ila tusiuze utu wetu, fikra zetu, na wanapokosea tusione haya kuwakosoa kisa tuko upande wao.
Na pia tusijigawe kisa wao, tusipigane, kuuwana na hata kutukanana kisa tuna itikadi tofauti za vyama.
Tunaowapigania hawana nia ya kutupigania kwa dhati zaidi ya kutufanya mtaji wa kufanikiwa wao.
Umekwenda vizuri, hao wenye itikadi moja ndio ninao waongelea.....mpira hawakusanyi kodi zetu wala kugawana ruzuku.Ndugu yangu naona kama unakosea, kwanza kumbuka kila mtu ana uwezo wake wa kufikiri. Hilo la kuuna sioni kama kwenye nchi yetu linatokea japo huko mbeleni inawezekana. Kuwakosoa tunawakosoa sana, labda wanaoogopa kukosoana ni wale wenye itikadi moja. Kutukanana hili litakuwa gumu sana kwani tayari ushabiki umekuwa kama wa timu za mpira, kwani huko kwenye timu za mpira watu wanavyotukanana na kupigana vijembe unadhani wachezaji wanawagaia washabiki wao hela? Hilo la wanasiasa la kuwafanya wananchi ndio mtaji wao haliepukiki maana ndio nature ilivyo, ili mwanasiasa apate nafasi lazima apate wanaomuunga mkono. Ila kwamba watatukomboa ama la hilo wanye ushabiki hawana muda wa kuliangalia kwani kipendacho roho....