Kwanini mnafunga watoto wenu hirizi?

Kwanini mnafunga watoto wenu hirizi?

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,402
Reaction score
1,618
MCHUNGUZI HURU nawasilisha kwenu uchunguzi niliyoufanya kwa zaidi ya miezi sita.

Unakuta mtoto mdogo sana lakini ashavalishwa zile kamba nyeusi mkononi.

Wengi wanawavalisha hizo hirizi watoto kwa lengo la kuwatibu magonjwa kama degedege n.k sambamba na kuwawekea kile wanachodai ni ulinzi dhidi ya wabaya.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa si wale tu wasio na elimu bali hata wasomi hufunga watoto wao hizo hirizi. ISIPOKUWA wasomi wengi huvalisha watoto wao kiunoni ili watu wasione tofauti na wale wanaowavalisha watoto wao mikononi.

RAI YA MCHUNGUZI HURU : Watoto ni malaika wanaolindwa na Mungu na ndio maana mtoto mdogo ana uwezo wa kumuona mchawi na akawa analia tu, mtoto halindwi kwa HIRIZI.

WAZAZI BADILIKENI.

MCHUNGUZI HURU
 
Last edited by a moderator:
Leo kidogo umesema la maana,binafsi huwa sielewi maana ya hilo jambo!japokuwa kuna wengine wanasema wanafunga vitovu pale kulinda maisha ya mtoto!!
 
Yaani huwa vinanikera sana vile vidude mtu hadi kumbeba huyo mtoto unajishauri!
 
kweli kabisa hiyo kitu inakera sana mtoto mdogo amefungwa likamba leusi halafu limeshachafuka yaani inakera mno kwa kweli. siku hizi kuna chanjo nyingi za kuzuia watoto wasipate magonjwa mbali mbali tuwapeleke clinic kwa wakati sio kuwafunga makamba kama vibwengo
 
mbona huku kwetu hamna mambo hayo.... usipo mfunga ndo inakuaje
 
hizi ni mila na tamaduni zutu jamani? mbona mnapenda kudharau kila kitu? we kama humfungi mwanao acha wengine wafunge watoto wao.
 
ni kaaina kaushirkina tu, hili la hata wasomi sina hakika nalo sana, ila wakazi wengi wanaoishi maeneo yenye msongamano-uswahilini hili linausika zaidi kwao, kwa hapo haijalishi unajua kusoma au hujui...
 
hizi ni mila na tamaduni zutu jamani? mbona mnapenda kudharau kila kitu? we kama humfungi mwanao acha wengine wafunge watoto wao.

Huko Ntwara ndo zenu ila wakati ufike tuache mila potofu zisizokuwa na faida yeyote! Kumfunga mtoto hayo madude unafikiri ndo kumlinda?Mtoto mlinde kwa kumpatia chanjo na kumpa chakula bora tu hayo mengine tena tunasema ulozi/uchawi!Hebu badilika VOICE OF MTWARA
 
Back
Top Bottom