Kwanini mkoa wa Mbeya?

Kwanini mkoa wa Mbeya?

Nikajua utataja at least wahubiri wakubwa 15 na waimbaji wa nyimbo za injili at least 40 kutoka Mbeya!! Kumbe una taarifa robo tu!
Halafu hapo uliposema sijui sheikh Mazinde aliuliza sijui kuna nabii mnyakyusa sijui nini nini thread yako ulitaka kuipeleka kwenye mlengo gani? Nahisi unahitaji kukanyaga mafuta kwa Mwamposa wewe na unywe maji ya upako!! Karibu Mbeya
 
Ungekuwa unajua kitu kinaitwa neema usingeuliza ,kiufupi neema ni upendeleo anaoutoa Mungu mwenyewe kwa kusudi lake ni kama vile alivyoamua kuchagua taifa la Israel litumike kupeleka injili duniani
 
Mkoa wa mbeya wa arabu nadhani awakufika kabisa tofauti na mikoa mingine kidogo ina balance katika mambo ya dini.

Mbeya nadhani ndo mkoa wa kwanza kwa Tanzania kufikiwa na wazungu na kuwakuta bado awajajua mambo ya dini tofauti na sehemu zingine ndo maana unaweza kwenda mbeya vijijini usione msikiti hata mmoja.
 
Naulizia hii ya waimba nyimbo za injili, Wachungaji wa makanisa ya kilokole kwanini wengi wanatoka mkoa wa Mbeya?

Hawa wachungaji wa Mbeya wametapakaa nchi nzima wakihubiri injili na wokovu, Huwa najiuliza maeneo ya Dar es Salaam mengi mpaka mitaani wachungaji wa haya makanisa wengi wao wanatoka mkoa wa Mbeya

Je nini kipo nyuma ya huu mkoa wa Mbeya?

Je huko Mbeya kuna shule nyingi za biblia kuliko maeneo mengine?

Je Mbeya hii imani ya Kuhubiri na kueneza ulokole ina Misingi kutoka nchi gani?

Mfano hawa ni baadhi ya wachungaji wenye asili ya Mbeya na wenye majina makubwa na kuna wachungaji wengi wapo mkoani na hata maeneo mengi ya miji mikubwa

1.Mtume Mwamposa,Na kuna shehe (Ustadh Mazinde) aliwahi uliza hivi kweli Mtume anaweza kuwa mnyakyusa na akotokea Mbeya?

Shehe Mazinde aliumia baada ya kuona waislamu wanatoka Zanzibar na Tanga kwenda kuombewa na Mwamposa

2.Mwalimu Mwakasege.Huyu kwa wale wasiofungamana na upande wowote wengi wanamfahamu sana na anafuatiliwa na malaki ya watanzania kwa mafundisho yake

Inasemekana baada ya Lagos Nigeria kwa Afrika mkoa wa Mbeya ni wa pili Afrika kwa kuwa na makanisa mengi

Inasemekana kila baada ya hatua kadhaa mkoa wa Mbeya utakutana na makelele watu wakiimba na kusifu huku wachungaji wakitoa injili na maombi ya nguvu

Turudi kwenye waimba kwaya na Gospel kwa ujumla, Nadhani hapa ndio mwisho wa kazi yenyewe, Watu wa mkoa huu ukiwakuta wanaimba kwaya, wanaimba kwa hisia sana na unaweza Fikiria Leo ndio mwisho wa hii dunia

Maajabu wanaimba na kulia sana lakini mkoa wa Mbeya hauishi matukio ya vituko na maajabu kila wakati

Mwaka huu kuna mlima hapo Mbeya umesababisha ajali mfululizo haijawahi kutokea na ukamfanya Makamu wa Rais Philip Mpango kwenda kutazama eneo husika linalosababisha ajali, Cha kushangaza baada ya siku kadhaa wachungaji wakaenda kupiga maombi hapo Mlimani
Mbeya ina matapeli wengi kwa sasa utapeli umehamia kwenye dini na gospel pale hakuna cha Mungu wala nini
 
NIMEZALIWA MBEYA NIMEKULIA MBEYA

Ni Hakika Mbeya Inamakanisa Mengi Sana Yani Hadi Uchochoroni Tena Yapo Ya Kutosha Watu NI Kumsifu Yesu Tu Mpaka Mda Mwingine Mimi Mwenyewe Licha Ya Kuzaliwa Huku Huwa Sielewi Kuna Nini HILI NI JIJI LA KRISTO

MBEYA NA ULOKOLE NI KAMA SAMAKI NA MAJI

Uhalifu Ulikuwa Zamani Sana Tena Sana Wageni Karibuni HUKU NI INJILI TU NA MISOSI YA BEI CHEE.
 
Kuna sehemu inaitwa Simike Nigeria ipo Mbeya kwa mujibu wa wenyeji wa eneo hilo wanasema waliita ivo kwakufananisha na Nigeria kutokana na uwingi wa makanisa
 
NIMEZALIWA MBEYA NIMEKULIA MBEYA

Ni Hakika Mbeya Inamakanisa Mengi Sana Yani Hadi Uchochoroni Tena Yapo Ya Kutosha Watu NI Kumsifu Yesu Tu Mpaka Mda Mwingine Mimi Mwenyewe Licha Ya Kuzaliwa Huku Huwa Sielewi Kuna Nini HILI NI JIJI LA KRISTO

MBEYA NA ULOKOLE NI KAMA SAMAKI NA MAJI

Uhalifu Ulikuwa Zamani Sana Tena Sana Wageni Karibuni HUKU NI INJILI TU NA MISOSI YA BEI CHEE.
Uhalifu upo mkuu nimekabwa zaidi ya mara tatu maeneo ya Sterio,Fine na Mafiati pale vibaka ni wengi mnoo aisee
 
Umesahau na wachuna ngozi, wapiga nondo za kichogoni, waganga wa kienyeji wote wanatokea Mbeya,
 
Uhalifu upo mkuu nimekabwa zaidi ya mara tatu maeneo ya Sterio,Fine na Mafiati pale vibaka ni wengi mnoo aisee
SEHEMU AMBAYO HAINA UHALIFU NI MBINGUNI TU AMBAKO YUKO BWANA WETU YESU KRISTO.

Ninacho Kanusha Ni Huyo Mleta Uzi Kuzungumzia Uhalifu Wa Zamani Sana Na Kuuelezea Nyakati Hizi Kana Kwamba Upo Mpaka Sasa Mfano Alipo Sema Kupigwa Watu Nondo Na Kuchunwa Watu Ngozi Huo Ni Uhalifu Wa Kizamani Ambao Sasa Hivi Sijawahi Sikia Tangu Miaka Hiyooo Zamani Sana.
 
Back
Top Bottom