Kwanini Mkoa wa Kilimanjaro unazidi kuporomoka?

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,057
Reaction score
10,731
Pengine unaweza kuukataa ukweli huu hasa kwa kutazama maisha na biashara za wana Kilimanjaro hasa wa jamii ya Wachaga waliotapakaa karibu kila eneo la nchi hii.

Lakini ukweli ni kuwa Mkoa huu uliosifika sana kwa uchumi wa zao la kahawa na shughuli za ujasilia mali, umeporomoka sana kiuzalishaji.

Huku nguvu kazi yake kubwa ikitapakaa na kujenga uchumi wa maeneo mengine, kule nyumbani wameachwa wazee na waangalizi wa nyumba na mifugo.

Vijana wachache waliobaki huko wamezeeka kwa ulevi wa pombe ya gongo, dadii na busa.
Wamebaki kusubiria ndugu zao warudipo safari kuwaomba hela (Chamecha lukombe kyandu), yaani (POLE TUKULAMBE KIATU).

Kinachotokea sasa ni kutuma matumizi na matunzo kwa wazee na au wategemezi hao pamoja na kwenda kuwajulia hali hasa kipindi cha Krismas, na hivyo Mkoa umegeuka kuwa wa CONSUMERS badala ya PRODUCERS.

Shime Wachaga, Embu Krimas hii tujadili namna ya kufufua uzalishaji katika mkoa huu.
 
Hahahhaa mtahangaika sana.....huu ndo muda tutapaaaaa...!!!!
 
Hovyo kabisa
 
Hawatakuelewa subiri waje watajitapa sana huku wakikupa matusi na sifa za uongo
 
Hizo kahawa wanatakiwa wazile kama karanga au wanapaswa kuuza kwenye viwanda vipi??
 
Back
Top Bottom