Tized
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 4,025
- 5,955
Ila inakera sana. Bora mtu kutokuoa. Kama wewe hujaoa, mpe exam mkeo ya kuwazoea dada zako.
Mkuu Kama alivyosema Kaunga hii kitu ni ya pande mbili. Na mara nyingi huanzishwa na dada wa kaka kwa kutaka mkeo aishi kutokana na matakwa yao wao. na wakati mwingine huanzishwa na Mkeo asipokuwa na uelewa wa kutosha kwa namna ya kuishi na jamii ya watu wengine tofauti na familia alioizoea.
Mkuu kwa habari ya hii mambo huwa ni ngumu sana kuamua au kusuluhisha usipojitahidi kuwa ''independent'' nikimaanisha usichukue maneno ya upande mmoja na kuyafanyia kazi, jipe muda, chunguza na atakayekuwa ameenda kinyume na mwingine umuonye mbele ya wengine kwa HAKI, Kama ni dada zako unawakemee kwa haki na kama ni mkeo unamkemea kwa haki, hapo utaanza kujenga uhusiano na heshima kwa kila mmoja.
Mwisho jitahidi sana kuwa na msimamo wako kama Mwanaume na kama kichwa cha nyumba yako.
usiache dada zako na mama yako wamue namna ya wewe na nyumba yako muishi. You are the head so they under your terms.
Maneno ya hekima yanasema katika kitabu cha mwanzo kuwa ''Mtu mume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na Mkewe nao watakuwa mwili mmoja'' so kuna matatizo mengine inaweza pia kuwa wewe mwanaume ni chanzo pasipo kujua. so jitahidi kuangalia kama role yako kama mwanume una-play fairly
''nani alikuambia wanawake wanapendana kiasi hicho hata waishi pamoja kwa amani na uelewano? ni wachache sana kaka wa namna hiyo''