Kwanini middleman wa Richmond, Dowans na Symbion hakamatwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini middleman wa Richmond, Dowans na Symbion hakamatwi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muuza Samaki, Aug 24, 2011.

 1. M

  Muuza Samaki New Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu, miezi michache iliyopita, ndugu yangu ambaye ni mbunge alinipa taarifa kuwa kuna baadhi ya wabunge waliokuwa wameongwa pesa nyingi kuitetea Dowans na kusaidia kufanikisha uuzwaji wake. mmoja wapo ya wamiliki alikuwa akisafiri kwenda Dodoma na sanduku lililojaa pesa na kuwagawia wahusika mbalimbali. Aliniambia pia kuwa huyu jamaa alikuwa kati ya watu wa kwanza kufanikisha uanzishwaji wa kampuni ya Richmond Tanzania lakini wakati huo hakuna aliyemtaja.

  Richmond ilipowauzia mkataba Dowans, na yeye pia akaenda Dowans kama Mkurugenzi wa fedha na jana nilikuwa Tanesco nikasikia eti yeye ndiye Mkurugenzi Maya. Huyu jamaa nasikia anatokea Kenya ana biashara nyingi hapa nchini zikiwemo za madini ya Tanzanite. Pia amekuwa middleman wa makampuni ya Kenya amabayo yanakuja kuwekeza hapa nchini.
  Swali langu na msingi ni kwamba kwanini watu kama hawa hawajakamatwa na sheria ikachukua mkondo wake? Je, kama baadhi wa watuhumiwa wa Richmond kama Naeem Gire wamefikishwa mahakamani, kwanini yeye hajafikishwa mahakamani? Je, ni kwanini ameshiriki kwa karibu katika makampuni yote matatu? Mwenye taarifa zaidi atupashe.
   
Loading...