Habari wakuu naomb kujuzwa kuhusu hili jambo kwa wenye ujuzi wa masuala haya ya genetics ....(lengo kujuzwa sio ubaguzi kama Kuna jina lingine sahihi zaidi nilipaswa nitumie mtanisamehe)
Kwanini hawa jamaa wanafanana sana hasa wa kiume ?
Nishapishana nao kama Sita hivi maeneo tofauti ajabu wanafanana fanana sana.......wajuzi
Aisee Hilo swala ni kweli huwa wanafanana sana hata wazungu Kwa Africa sura zinafanana unaweza kukuta mbilikimo wa kizungu na mbilikimo wa ki Africa sura kama mapacha nashindwa kuvielewa hivi viumbe
Mambo kama hayo ni ya kijenetiki. Hivyo unakuta labda wenye jeni hizo wote wana pua ya namna fulani. Kwa hiyo ukimuona huyu au yule utaona wanafanana kwa kuwa tu wameshea sifa fulani.
Ni sawa na useme watu wenye 'trisomy' wanafanana wote kutokana na namna wanavyoweka ulimi na midomo.
Si ushasikiaga kata pua uunge wajihi, ndo mambo kama hayo sasa. Kitu kidooooogo kikifanana basi utasema wote wanafanana.
Kwenye dwarfism head is not affected kichwa huwa kinaendelea kukua especially eneo la ubongo kwakuwa ana upungufu wa growth hormone lile eneo hutanuka ili kukidhi space ya ubongo ndio maana wengi wao wana vichogo na makomwe ..mbilikimo wachache sana wana vichwa vidogo.
Kwa sababu ya condition inayoitwa achondroplasia hii hutokea kwa aina ya kwanza ya dwarfism (Disproportionate dwarfism), ambayo ni hali ya kijenetiki inayosababisha ufupi wa miguu na mikono, kichwa kikubwa na uso kuwa na muonekano unaoendana...