Ndata
JF-Expert Member
- Mar 2, 2017
- 226
- 321
Kumeibuka kundi kubwa la wazalendo wa nchi hii kutaka ukomo wa madaraka uondolewe kwenye katiba yetu ili kuruhusu Magufuli aongoze kwa awamu tatu au nne zaidi.
Hili sio jambo geni duniani. Hata Marekani wamewahi kufanya hivi mwaka 1940 Roosevelt alipochaguliwa kuongoza kwa awamu ya tatu na 1944 aliporuhusiwa kugombea kwa awamu ya nne bahati mbaya akafariki. Baada yake mfumo huo uliondolewa.
Sababu za kuongezewa muda ni zilezile tunazoziongelea Tanzania, Magufuli ni mfano wa viongozi aina ya Mao wa China, Nyerere wa Tanzania na Roosevelt wa Marekani. Hawa ni wajenga nchi.
Viongozi aina hii huchukua Muda kupatikana, ndio maana baada ya Mao wa China kiongozi mwingine wa aina yake ni huyu kapatikana kizazi chetu hichi na tunaona wachina wamemuondolea kabisa ukomo wa uongozi.
Tanzania baada ya Nyerere wamepita viongozi watatu hadi kuja kumpata mwingine mwenye mawazo, malengo na itakadi kama ya Nyerere, kwanini tusimuongezee muda ilihali Nyerere aliongoza kwa awamu zaidi ya nne kama tukihesabu miaka mitano mitano.
Mfumo wa uchaguzi ubaki kama ulivyo kila baada ya miaka mitano na pale Magufuli atakapochoka au kufariki katiba ibadilishwe kurudi kwenye mfumo tuliozoea hadi pale atakapopatikana mjenga nchi mwingine.
Shauri lililopo mahakamani lililofunguliwa na Mkulima ni shauri la kizalendo na lenye maana kubwa kuliko hoja za wanaompinga.
Wakati hoja kuu ya wapinzani ni Rais kubadilika pale anapogundua kaondolewa ukomo suala la uchaguzi kila baada ya miaka mitano nadhani linaweza imaliza hoja yao kabisa. Kama hawana imani na tume ya uchaguzi hio ni issue tofauti sana na kilio chetu wazalendo cha Magufuli kuondolewa term limit kwa faida ya nchi hii.
Ombi kwa wazalendo wengine wengi huu ni muda wa kuungana na Mkulima kimawazo, ushauri na kumuwezesha pale anapikwama ili asije akashindwa kwa vitu vidogo ambavyo tungeweza kuchangia.
Cwu.