Kwanini Magufuli hampongezi Makonda?

Kwanini Magufuli hampongezi Makonda?

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Pamoja na jitihada anazofanya Makonda kuonyesha anaendana na kasi ya Magufuli, kwa kuwaweka ndani mara kwa mara viongozi wa wananchi wakiwemo wafanyakazi wa Ardhi Kinondoni na mbunge wa Ubungo, kuupa deadline utawala wa Urafiki na jitihada zingine, lakini sijaona wala kumsikia rais akimpongeza tofauti na Kikwete aliyekuwa akimpongeza mara kwa mara hadi kufikia hatua ya kumteua kuwa mkuu wa wilaya baada ya kuonyesha uwezo wa kumdhibiti mzee Warioba.

Ina maana rais Magufuli hazioni juhudi za Makonda au anazipuuza?
 
Atazipongeza tu wakati akipitia uteuzi wa wakuu wa wilaya wote, huyo jamaa anamtia aibu
 
unafuatilia mazungumzo yao?
 
Kama yale maneno magufuli aliyowaambia mawaziri wake yalitoka moyoni basi huyu hatampongeza atamfukuza...alisema nendeni mkafanye kazi bila kuwabagua watanzania kupitia chama chao au rangi wala kabila..
 
Labda nae anamuona kama kubenea alivyomwita makonda.
 
Ni fedhea kwa utu wake na fedhea kwa serekali safi ya JPM
 
Kama yale maneno magufuli aliyowaambia mawaziri wake yalitoka moyoni basi huyu hatampongeza atamfukuza...alisema nendeni mkafanye kazi bila kuwabagua watanzania kupitia chama chao au rangi wala kabila..
Hilo neno
 
Tatizo anayafanya haya kipindi hiki, kwanini hakuyafanya haya kipindi kilichopita cha Mh. JK
 
Mzee Magufuli alikuwa mjumbe wa Bunge la Katiba. Sio ajabu hata yeye aliwahi kulizwa simu Smartphone yake na bado anakumbuka muhusika mkuu wa wizi wa simu wakati ule alikuwa nani.
 
Back
Top Bottom