Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya sana

Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya sana

Entim

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
4,024
Reaction score
2,273
Wakuu,
Umofia kwenu.
Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya isioweza kusomeka vizuri?
1. Je wanafundishwa chuoni?
2. Wanakuwa na haraka ili kuwahi wagonjwa?
Madaktari karibuni
 
Wakuu,
Umofia kwenu.
Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya isioweza kusomeka vizuri?
1. Je wanafundishwa chuoni?
2. Wanakuwa na haraka ili kuwahi wagonjwa?
Madaktari karibuni
Siyo wote lakini kuna wanaoandika vizuri. Nadhani sababu ni haraka waliyonayo.
 
Ni kwakuwa wamesomea mambo mengi sana, imepelekea kuharibu hata kuandika kwao.
 
Nahisi kama imekuwa sehemu ya kawaida sasa madaktari kuandika vibaya,kwahiyo imekuwa sehemu ya utaratibu wao

Na kuna takwimu za vifo vya wagonjwa ambao wanakufa kutokana na ama kupewa dawa ambazo sio sahihi kuongezewa dozi kwasababu wafamasia wanashindwa kuisoma vizuri
 
According to my experience, mwandiko wangu hua unabadilika kutokana na muda. Asubuh ninavoanza kazi hua nipo kistaarabu kabisa tena mwandiko mzuri, lakini muda unavozid kwenda hali inakua mbaya. Sababu kuu mostly ni wingi wa wateja. Per day unakuta unahudumia watu wengi sana na hapo kila mtu ana shida yake. Sometimes ukiangalia foleni uliyonayo unakuta ni kubwa inabidi tu ucharange ili kukimbizana na jam maana ukiremba utakesha.
 
Umeenda mbali angalia wanafunzi waliosoma sayansi miandiko yao na waliosoma arts miandiko yao halafu utapata jibu .
 
Zamani ndo ilikuwa shida zaidi, miandiko mibaya, wanaosoma udr sasa--wale wasichana rafu na sura mbaya ndo wanaosomea udr. Ila siku hizi wanandika vizuri na watoto wakali kali ndo wanasoma udr.
 
Wakuu,
Umofia kwenu.
Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya isioweza kusomeka vizuri?
1. Je wanafundishwa chuoni?
2. Wanakuwa na haraka ili kuwahi wagonjwa?
Madaktari karibuni
Wengi miandiko inakuwa hivyo baada ya kuanza kazi. Mambo ya kuandika ni mengi na wagonjwa wengi pia, hivyo kurembesha kunapotea.
 
Sababu Toka nasoma mwandiko ilimradi usomeke ila mambo ya kuremba muandiko muda unaona huna
 
kinachofurahisha wewe hata uwe na phd ya fani nyingine huelewi ila hata mhudumu wa pharmacy anaelewa kilichoandikwa.
 
Wakuu,
Umofia kwenu.
Kwanini Madaktari wana miandiko mibaya isioweza kusomeka vizuri?
1. Je wanafundishwa chuoni?
2. Wanakuwa na haraka ili kuwahi wagonjwa?
Madaktari karibuni
... miongoni mwa courses za madaktari ni pathology ambapo maiti zinahusika sana. Hii inawaathiri kisaikolojia hadi miandiko yao.
 
Wanapokuwa masomoni huwa wanachukua notes kutoka kwa anaewafunza
Sasa inabidi waandike haraka haraka ili waendane nae

Nakumbuka nilipokuwa mkalimani kama mtu anahojiwa lazima nichukue notes haraka haraka tena kwa ufupisho sana
Kama akiilizwa ana watoto wangapi ntaandika b4 g2 na hapo nikitoka baada ya dakika 5 tu mimi mwenyewe siwezi kusoma nilichoandika kwani yanabaki pale pale

Ila kwa Doctors ni tofauti wao wamesoma miaka mingi na wana kumbuka sana wanachoandika

Kwa hiyo sababu ndio hizo kuchukua Notes haraka kwa kuandika
 
Back
Top Bottom