Kwanini mabasi yatokee stendi kuu ya Magufuli?

Kwanini mabasi yatokee stendi kuu ya Magufuli?

Huyu jamaa ukute ana kijifremu chake pale stand..
Yes na huenda ni wale watoza kiingilio pale getini kwasababu mabasi yakitoka mjiini yanaingia pale na kutoka hivyo wanakosa tozo za wale abiria walioko kwenye mabasi
 
Nashauri mabasi yote yabaki pale mbezi yasionekane mjini.

Kama Wana mizigo basi watafute vigari kubebwa hio mizigo.

Pale shekllango ni stendi bubu ya haya mabasi yaondoke
Naimani hijawahi kusafiri mikoani maana hujui ni adha kiasi gani wanapata wasafiri
 
Huu ujinga wa kungangania stand iwe moja sijui umetoka wapi Tz kuna upumbavu mwingii. Nenda dunia kote hata marekani kila mwenye mabasi yake ana terminal zake. sasa huu utaratibu wa kulazimisha wote tukusanyike sehemu moja kama ngombe ni tunaendelea au tunarudi nyuma?.

The way foward tukubaliane kuwe na public na private bus terminals tuweke vigezo na tozo zinazoeleweka kwa private terminals tuache huu ujinga unaonganganiwa sasa.
 
Yes na huenda ni wale watoza kiingilio pale getini kwasababu mabasi yakitoka mjiini yanaingia pale na kutoka hivyo wanakosa tozo za wale abiria walioko kwenye mabasi
Usafiri sio starehe ni huduma,kama lengo ni mapato kutoka kwa abiria basi mabus yaongeze miatano katika nauli ili yakifika mbezi yatoe ushuru ili watu wasipate usumbufu,pia haya mabus huwa yakitoka mbezi ni direct kwenye ofisi zao sasa shida nini hapo...[emoji1]watunga sheria hii hata foleni hawasimami wanatumia escort,mabus hawapandi waweke tozo tu [emoji1787][emoji1787]abiria watalipa
 
Stand kubwa ya kimataifa ila. Vyoo havina maji,Kwa nn wasikimbiwe
 
nchi ya kusadikika , huenda kuna mchumi mmoja mbebezi kawaambia basi likenda chanika mapato yatapungua, nchi ngumu sana hiyo
 
Kwa mtu anaye kaa Dar au Alisha wahi fika Dar hawezi andika ujinga huu ulio andika wewe shida yenu watu wa mkoa ambao Dar mnaiona kwenye TV na kusimuliwa unaweka fikra za kuona ni Kama wilaya yako ya Tanganyika iliyopo mkoa wa Katavi.

Huwezi jua adhaa na karaha za jiji la dar hasa kwenye usafiri Kama hauja wahi fika dar ndio maana Mara zote huwa nasema humu jiji Kama dar kuwa na bus terminal moja ni ujinga na uzwazwa (kwa wale walio wahi fika na wakaazi wa dar) wananielewa nini nacho sema hapa

Pia huwa nahoji Kuna sheria gani inatamka kwamba bus terminal lazima kujengwa nje ya mji au jiji ?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona watu wanaoenda airport kupanda ndege..wanenda bandarini kupanda azam marine...kwann hii ya basi inaleta poyoyo nyingi?
 
Mbona watu wanaoenda airport kupanda ndege..wanenda bandarini kupanda azam marine...kwann hii ya basi inaleta poyoyo nyingi?
Ulishawahi kwenda airport ukagombaniwa na wapiga debe au ukaanza kutafuta ndege unayoondoka nayo bila mafanikio alafu hakuna mtu anapanda ndege alishawahi kulalamika atafikaje airport?
 
Serikali yetu kuna sehemu haina Meno,

Hivi inakuwaje baadhi ya wanainchi kugomea agizo la serikali?

Duniani kote lazima kuwe na stand kuu za mabasi.

Mambo ya vituo vya uchochoroni yakomeshwe..

Hivi airport watu wanafikaje?
Au mtu anaishi vikindu na anafanya kazi katikati ya mji anafikaje?

Bus Terminal ya Magufuli itaweza kudhibiti Mambo mengi sn.
Uthibiti wa ukaguzi wa mabasi kabla ya safari.
Na hata baada ya safari.

Serikali itoe agizo la kufungia ofisi zote za mabasi vichochoroni.
 
Hizi sheria ni za Kikomunisti kila Kampuni ijenge sehemu ya kupakilia, hizo Stendi ziko mbali sana mfano Sumbawanga inabidi watu waamke saa nane za usiku ilikuwahi Mabasi Stendi, Stendi imejengwa kilometa salasini.

Tunateswa na IQ zetu ndogo.

Umenikumbusha igumbiro iringa, songea, yaani wanadai wanapanua miji ni ushamba tu Uganda na Zambia kuna kila kampuni ina bus park yake abiria atachagua huduma rahisi iko wapi, huku tukiona stand ni bigdeal kwa uwezo mdogo wa kufikiri ndio wakakurupuka kujenga masoko ambayo hayana kazi wakati maeneo yale ilitakiwa wapewe watu binafsi wajenge haya malls lakini wawekewe tu sheria kua bei ya bidhaa iwe affordable
 
Ulishawahi kwenda airport ukagombaniwa na wapiga debe au ukaanza kutafuta ndege unayoondoka nayo bila mafanikio alafu hakuna mtu anapanda ndege alishawahi kulalamika atafikaje airport?
Sijakuelewa...siku hzi mabasi yanamfumo wa kukata ticket online kama ndege tu...vp umewahi kwenda kukata ticket ya boti pale ferry ukaona shughuli yake?
 
Back
Top Bottom