Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Kama Lowassa alikuwa na nia njema ya kuwatumikia wananchi wa Tanzania na sio maslahi binafsi/kifisadi basi:-
1. Alipaswa kwenda UKAWA kabla ya kushindwa CCM.
2. Alipaswa kutubu/kuungama juu ya ufisadi na uonevu wote alioshiriki na anaoufahamu (kufanywa na CCM) dhidi ya Taifa hili.
3. Alipaswa ajitenge na kuonekana hivyo kuwa SASA anachukia rushwa, ufisadi na uonevu.

NB: Kwa wale wasio jua (wengine wamesahau), Lowassa ni katili sana. Jimbo lake la Monduli wapinzani wameuawa, wameumizwa na wengine wengi kupoteza mali zao na hata kulazimika kukimbia. Iweje leo hayo yote yasahaulike na ghafla tu mumfanye mmoja wa UKAWA?
 
John Komba angekua anatupa burudani saa hvi.

Daah maisha hayaa.
 
UKAWA wanaweza wakampa tu maana ataongoza kwa misingi na itikadi za chadema na cio tena ccm so wanaweza wakampa namba kama ktk kikosi chao kuna chance .
 
UKaWa unaouona moyoni mwako, unaundwa na vyama vya siasa ambavyo vimekoma kuandikisha wanachama wapya?

Bila kuwapenda na kuwabadilisha Watanzania, wawe na mitazamo na itikadi za UKAWA, tunajenga nchi namna gani? Magereza hayatoshi kuhifadhi mafirauni wote. Ni vizuri wakibadilika na kuwa raia wema wakashiriki katika ujenzi wa taifa ambalo ni letu sote japo sisi tunaongoza kwa kutoa dira na miongozo.

Kuna watu huwezi wabadili bila ya wewe kujibadili kwanza na kuathiri mfumo wako wa maisha, kimtazamo na kisera...
Njia pekee ya kumbadili Mzee ni kumshauri aache siasa na akapumzike na si kumpatie platform ya siasa.....
 
Mkuu mawazoyako mazuri Urais asigombee ila agombee ubunge kwa tiketi ya chama kimojawapo kinachounda UKAWA bungeni tuwe na majimbo menge
 
Kinachosumbua Lowasa nikurudisha zile hela alizotumia,mambo mengine ya mapenzi baadaye....UKAWA kuna upenyo huo kweli?
 
Na haijajulikana kama analilia ukawa ili awe raisi, au analilia kuwa mwanachama katika vyama vya ukawa ili atumikie taifa katila hali nyingine tulivu na yenye amani. Kuna Watanzania wengi tu wanavyama vya siasa lakini hawagombanii uongozi.




Kuna watu huwezi wabadili bila ya wewe kujibadili kwanza na kuathiri mfumo wako wa maisha, kimtazamo na kisera...
Njia pekee ya kumbadili Mzee ni kumshauri aache siasa na akapumzike na si kumpatie platform ya siasa.....
 
Back
Top Bottom