Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Mkuu upepo umebadilika imewachukua muda mrefu CCM kumkabili Lowasa na kuweza kumvua Gamba.
CDM sio kanisa ni chama cha Siasa, Lowasa ni Fisadi tu hafai nimesema narudia tena kama mnataka Pesa zake mchukueni.
Kwa nini anatumia nguvu kubwa kutafuta lkulu?


Kwa maana hiyo Lowasa hatakiwi tena kuhesabiwa ni Mtanzania? Amepoteza haki zake za uraia wa kushiriki maendeleo ya nchi kama raia wa kawaida? Kwamba CHADEMA NI CHAMA DHAIFU SANA HAKIWEZI KUMLEA NA KUMFANYA ABADILIKE KUTOKA UFISADI KWENDA UTANZANIA? Au kwa vile ccm imeshindwa unadhan Watanzania wote hawana uwezo wa kuwabadilisha watu?

Kwa sababu baada ya October, mafirauni wote walioko ndani na nje ya ccm watalazimika kubadilika na kutii sera na kanuni za UKaWA wapende wasipende. Watalazimika kuwa raia wema na hawatapata nafasi ya kutamba na ufirauni wanaodhani unatamalaki milele.

Ccm kwa kuwa hiawezi kubadilisha lolote huwa inawaua wanaokwenda kinyume nayo, lakini UKAWA, ninaamini hawana imani hiyo, wao ni watengenezaji nawarekebishaji wa watu kwa maslahi ya taifa.
 
Tabby

khaaa,,,,! Eti mtu akihama anahama na ufisadi, nani aliyekuambia lowasa ni fisadi? Mbona kwenye ripoti ya mwakyembe hakutajwa? Ana uhuru wa kuamua aendako!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ukawa anajua kule hataambulia anachokitarajia,anaweza akaupata urais lkn hasipate wabunge kwani act ni chama kichanga bado kinahitaji kujitangaza sana hata kwa miaka kumi ijayo ndio kiwe kama taasisi kamili kama ilivyo cdm,ccm,cuf,nccr

Kwann alikianzisha wakati huu ambapo alijua kuna uchaguzi mkuu? Si alitaka kuivunja ukawa? Wamemgeuka sasa
 
Kwanini anaamini Sana katika rushwa? UKAWA mkimpa nafasi Lowassa mtakuwa wehu na wapenda rushwa kuliko CCM. Thamani yenu itashuka na mtadharauliwa milele

Kama unaidharau ccm sawa
 
Kwani UKAWA ni ideology au mkusanyiko wa Manyangau kutoka CHADEMA na CUF.
 
Akija ukawa nitakuwa wa kwanza rudisha kadi yangu..na nitawadharau sana viongozi wangu wa chadema.
Maana itabidi wawe wanafki ili wamwingize ukawa na sisi Sera zetu unafki ni mwikooo
 
Suala la kuhamia UKAWA ni vema likaachwa alisemee mwenyewe, inavyoelekea hivi sasa watu wanataka kugombana wakati mhusika mwenyewe Lowassa hajasema neno. Pia masuala ya Richmond mahali ambako walikuwa wanayafahamu kwa undani zaidi ni CCM, kwani wahusika wote (Lowassa, Kamati ya Mwakyembe na Wadau wengine wa skendo yote) wanatoka CCM na mpaka hivi sasa wanategeana kulizungumzia pamoja na ahadi nyingi za kuahidi kulisemea hadharani mpaka wamesambaratishana.
 
Lowasa anaakili kuliko mnavodhani.Amepata kibali mbinguni na duniani.Mlango 1 ukifungwa mwingine unafunguka.Endeleeni na majungu
 
Tunaposema tunakwenda kuikomboa nchi, tunamaanisha tunakwenda kuogoza mabadiliko halisi kwa kutumia kila raslimali iliyopo nchini kwa maslahi ya taifa. Lowasa ni moja ya raslimali za taifa ambaye anatakiwa atumike vizuri kwa ustawi wa taifa kama vile madini, gesi, mafuta, misitu, wewe, mimi na ritz1.

Hatutakuwa viongozi wazuri kama tutashindwa kutumia raslimalli za taifa kwa maendeleo ya taifa kwa sababu yoyote ile.

Kwa mantikihiyo, watanzania wote, watalazimika kuwa wazalendo hata kama hawataki kwa sababu hiyo itakuwa ndiyo dira ya maendeleo ya taifa. Kuna ubaya gani kumkubalia Lowasa kujiunga na UKaWA akaanza kubadilishwa na kuwa Mtanzania safi sasa kama tu HAACHWI AKAINFLUENCE CHAMA KWA KUPANDIKISZA UFIRAUNI WA CCM TUNAOUKATAA AUA KAMA HAPEWI UONGOZI?
Mawazo mazuri kutoka kwa mtu makini!
Mkuu jana nilipo pata hizi tarifa za el kwenda kuongeza petrol ya kuondoa ccm madarakani tulifunga safari adi makao makuu ya chadema kufuata card nilisikitika kuambiwa zimekwisha!
Kwa sababu nilikuwa na nia ya dhati ilibidi ninunuwe gwanda!
Ni muhimu sana kutumia rasilimali watu kama lowassa akija ana okoka anakuwa raia mwema kaulimbiu ya chadema vua gamba itakuwa imetimia na itifaki itakuwa imezingatiwa
 
Tabby

Lowasa akijiunga na CDM jua kwamba CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi huu, kumbuka Lowasa ni ktk magamba yaliyoshindwa kuvuka wakati ule kama wamevua sasa thamani yake inatoka wapi hata CDM wamsafishe.
Huyu hafai hata kua nwanachama wa kawaida labda kama mnataka pesa zake.
Mtadharauliwa sasa mpaka kizazi cha tano.

Unajamba na kujifunika shuka wewe mwenyewe halafu na wewe ni Great thinker!!
 
Last edited by a moderator:
Japo kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa Lowassa ndiye anayetaka kwenda UKAWA au ni wafuasi wake ndio wanaotaka Lowassa aende UKAWA lakini Lowassa anayohaki ya kujiunga na chama chochote Kati ya vile vinavyounda UKAWA kama mwananchi wa kawaida yeyote anavyo weza akajiunga na UKAWA.

Ila ana takiwa awaheshimu viongozi atakaowakuta UKAWA na asijiunge UKAWA kwa ajili ya kutaka uongozi bali kama mwanachama wa kawaida,awachie viongozi na wanachama wa UKAWA atakao wakuta huko ndio wamfikirie kumpa uongozi kama watamuona anafaa kutegemeana na vigezo vyao.

Ushahidi upo,maana ameshasema tena kwa kutisha chama chake kwamba wasipopata mabadiliko ndani ya ccm basi atayafuta nje ya ccm.sasa mabadiliko kayakosa ndani ya ccm ni wakati ayapate nje ya ccm ambako ni ukawa
 
Lowasa anaakili kuliko mnavodhani.Amepata kibali mbinguni na duniani.Mlango 1 ukifungwa mwingine unafunguka.Endeleeni na majungu

Mapenzi yaliyopitiliza hupofusha akili,bado una fikra hizi,hata mzee makamba aliwahi kumwambia nape kwamba amefungiwa duniani na mbinguni lakini DOGO anadunda na uenezi.
 
Tabby

khaaa,,,,! Eti mtu akihama anahama na ufisadi, nani aliyekuambia lowasa ni fisadi? Mbona kwenye ripoti ya mwakyembe hakutajwa? Ana uhuru wa kuamua aendako!

... Acha Kumtetea, Lowasa Ni Fisadi Tu. Fisadi Ni Fisadi Tu Hata Ahamie Mbinguni
 
Last edited by a moderator:
Hatuhitaji makapi ya CCM UKAWA, tena hasahasa huyo LOWASSA. Afadhali angekuwa mwingine.. hata kuwa mwanachama tu ni kujidhalilisha.. si ni yeye huyu huyu tuliyekuwa tunamuita fisadi? Yaani leo tumpokee sio kwa sababu ametubu na kurudisha mali za umma ila ni kwa sababu tu ya kuukosa urais? Hapana.. kama anataka kuhama CCM aende ACT au aanzishe chama kipya maana anamtaji mkubwa wa wale waliokuwa wanagaragara na kutambaa kule Dodoma
 
Akija ukawa nitakuwa wa kwanza rudisha kadi yangu..na nitawadharau sana viongozi wangu wa chadema.
Maana itabidi wawe wanafki ili wamwingize ukawa na sisi Sera zetu unafki ni mwikooo


UKaWa unaouona moyoni mwako, unaundwa na vyama vya siasa ambavyo vimekoma kuandikisha wanachama wapya?

Bila kuwapenda na kuwabadilisha Watanzania, wawe na mitazamo na itikadi za UKAWA, tunajenga nchi namna gani? Magereza hayatoshi kuhifadhi mafirauni wote. Ni vizuri wakibadilika na kuwa raia wema wakashiriki katika ujenzi wa taifa ambalo ni letu sote japo sisi tunaongoza kwa kutoa dira na miongozo.
 
Back
Top Bottom