Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Kwanini Lowassa sasa analilia UKAWA?

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Nimesoma mabandiko mengi hapa yakiongelea Lowassa sasa amegeuza majeshi analilia kwenda UKAWA.

Kwa nini anatumia nguvu zake kwenda UKAWA katika kipindi hiki baada ya kumwagwa CCM?

Ninashauri asikilizwe bila hata juhudi za Apson kukusanya fedha za rushwa. Lowassa na watu wako mfahamu kwamba si kila siku fedha itafanya kazi mahala pote, hilo suala la fedha acheni.

Kama Lowassa anataka kuhamia CHADEMA, asizuiliwe kwa sababu CHADEMA ni sehemu ya UKAWA ambao lengo lake ni kujenga nchi ya Wtanzania isiyokuwa na ufisadi wala ufirauni wowote wa kiccm iliyoshindwa. Na nchi hii mpya itajengwa na Watanzania walio ndani na nje ya vyama vyote vya siasa, kwa uongozi wa UKAWA.

UKAWA itakuwa na jukumu la kuwabadilisha Watanzania fisadi wawe watanzania bora kwa njia zote ngumu na nyepesi, kwa hiyari zao ama bila hiyari zao. Tunahitaji taifa lenye mtazamo na mwelekeo sahihi at all costs.

Kama ndivyo, Lowassa akiwa kama Mtanzania, na anatamani kuingia UKAWA, asizuiliwe ila Asipewe uongozi na yeye asilazimishe uongozi kwa sababu UKAWA ni imani mpya kwake.

Anahitaji kufundishwa kama vile muumini wa dini mpya afundishwavyo amani mpya kabla hajaanza ku3nda kwenye utumishi.

Ushauri waneu narudia, kwa kuwa analilia sana, apokelewe kama mwanachama wa kawaida, afundishwe uzalendo sahihi, ajenge nchi yake kwa njia sahihi zisizo za ufirauni chini ya uongozi wa UKAWA na aache ubabe wa kulazimisha kwamba awe raisi.

Kwa UKAWA hana sifa, lakini anaweza kuwa mwanachama akafundishwa uzalendo wa kweli na akaishi kwa kujenga nchi kama ambavyo tunategemea kuwa tunakwenda kubadili taifa na kulifanya la wazalendo wajenzi wa nchi kwa kuwapa sera na miongozo sahihi, kuwalinda na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kwa ustawi wao na ustawi wa taifa.

Lowassa apokelewe lakini asipewe uongozi kwa kumpa ongozi ni kuhamisha ufisadi toka CCM kwenda UKAWA na hivyo kupoteza muelekeo wa UKAWA.

Yeye awe raia ajifunze itikadi za chama na abadilishwe kutoka ufisadi kwenda uzalendo na kukimbilia uraisi kama anavyotaka.
 
Kama anaipenda zaidi ukawa basi afute AcT yake aliyoianzisha.
 
Tabby

Lowasa akijiunga na CDM jua kwamba CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi huu, kumbuka Lowasa ni ktk magamba yaliyoshindwa kuvuka wakati ule kama wamevua sasa thamani yake inatoka wapi hata CDM wamsafishe.
Huyu hafai hata kua nwanachama wa kawaida labda kama mnataka pesa zake.
Mtadharauliwa sasa mpaka kizazi cha tano.
 
Last edited by a moderator:
Kama anaipenda zaidi ukawa basi afute AcT yake aliyoianzisha.

Mkuu ukawa anajua kule hataambulia anachokitarajia,anaweza akaupata urais lkn hasipate wabunge kwani act ni chama kichanga bado kinahitaji kujitangaza sana hata kwa miaka kumi ijayo ndio kiwe kama taasisi kamili kama ilivyo cdm,ccm,cuf,nccr
 
Umesema sahihi. Na ndiyo sababu ninasema akaribishwe kama muumini mpya ajifunze abadilike awe raia mwema na ajenge taifa bila ufirauni wa ccm wala tamaa yake ya madaraka na ulaghai, kwa kuwa kwa wakati mmoja au mwingine, wakati UKaWA itakapokuwa madarakani kuanzia October, Si Lowasa wala Fisadi yeyote atabaki na shombo za ufirauni awe ndani ama nje ya ccm.

Kwa kumkaribisha UKaWa na kumbadilisha awe kiumbe kipya, ni kwamba tu atakuwa fisadi wa kwanza kusalimu amuri na kugeuka kuwa raia bora, lakini Watanzania wote tunalengo la kuwabadiisha wawe wajenzi wa taifa badala ya mumiani nyonya damu za wanyonge.

Ninachokataa ni kumpa uongozi kwa sababu ni kusambaza kansa ya ufirauni wa ccm , na kuua lengo na madhumuni ya UKAWA na kuufanya ukawa kiota cha mafisadi mafirauni wahuni.

Sumu ya CCM bado ni ile ile! Ni chupa tu imebadilishwa! Mwananchi zinduka, chukua tahadhari mapema!
 
NI NANI ALIYEKUDANGANYA?/ii

Tunaposema tunakwenda kuikomboa nchi, tunamaanisha tunakwenda kuogoza mabadiliko halisi kwa kutumia kila raslimali iliyopo nchini kwa maslahi ya taifa. Lowasa ni moja ya raslimali za taifa ambaye anatakiwa atumike vizuri kwa ustawi wa taifa kama vile madini, gesi, mafuta, misitu, wewe, mimi na ritz1.

Hatutakuwa viongozi wazuri kama tutashindwa kutumia raslimalli za taifa kwa maendeleo ya taifa kwa sababu yoyote ile.

Kwa mantikihiyo, watanzania wote, watalazimika kuwa wazalendo hata kama hawataki kwa sababu hiyo itakuwa ndiyo dira ya maendeleo ya taifa. Kuna ubaya gani kumkubalia Lowasa kujiunga na UKaWA akaanza kubadilishwa na kuwa Mtanzania safi sasa kama tu HAACHWI AKAINFLUENCE CHAMA KWA KUPANDIKISZA UFIRAUNI WA CCM TUNAOUKATAA AUA KAMA HAPEWI UONGOZI?
 
Sina uhakika na unalosema kama ni maoni ya Lowasa mwenyewe au ni hisia za watu tu.
 
Uraisi hawezi kupata hata aende wapi!. Hatukubali kuwa chini ya fisadi. Ila kama kajuitia makosa na anataka kulitumikia taifa kwamba kajua ccm hakuna uwezekano wa kuijenga nchi anayolilia kuipenda sana sasa, atambue kwamba anauwezo wa kufanya hivyo hata bila kuwa raisi. Na kwa kuwa mfumo wa ccm anauchukia na akijua ndio mfumo aliouasisi wa kifisadi wakati akiwa waziri kule, na sasa anajuta, akae chini, ajifunze njia mpya chini ya UKAWA, abadilike awe mwema aktika siku zake za mwisho lakini ASITHUBUTU KUENDELEA NA SHINIKIZO LAKE LA URAISI WAKATI HAFAI NA WALA ASITEGEMEE KUPEWA URAISI KWA SABABU ANAPASWA KWANZA KUJIFUNZA UZALENDO CHINI YA MFUMO MPYA.

Mkuu ukawa anajua kule hataambulia anachokitarajia,anaweza akaupata urais lkn hasipate wabunge kwani act ni chama kichanga bado kinahitaji kujitangaza sana hata kwa miaka kumi ijayo ndio kiwe kama taasisi kamili kama ilivyo cdm,ccm,cuf,nccr
 
Hamtumtaki fisadi nani alokwambia ukawa kua wanamuhitaji fisadi mgombea ni slaa mwenza ni musa haji aminini ninayo sema
 
Uraisi hawezi kupata hata aende wapi!. Hatukubali kuwa chini ya fisadi. Ila kama kajuitia makosa na anataka kulitumikia taifa kwamba kajua ccm hakuna uwezekano wa kuijenga nchi anayolilia kuipenda sana sasa, atambue kwamba anauwezo wa kufanya hivyo hata bila kuwa raisi. Na kwa kuwa mfumo wa ccm anauchukia na akijua ndio mfumo aliouasisi wa kifisadi wakati akiwa waziri kule, na sasa anajuta, akae chini, ajifunze njia mpya chini ya UKAWA, abadilike awe mwema aktika siku zake za mwisho lakini ASITHUBUTU KUENDELEA NA SHINIKIZO LAKE LA URAISI WAKATI HAFAI NA WALA ASITEGEMEE KUPEWA URAISI KWA SABABU ANAPASWA KWANZA KUJIFUNZA UZALENDO CHINI YA MFUMO MPYA.

Mkuu juzi kuna member aliweka bandiko hapa kuwa lowasa ajiunge cdm,lkn ajitokeze hadharani kukana na kuhusika na Richmond na awaombe radhi watanzania kwa kuwamo ktk kashifa hizo na watu wa mungu wamwombee atakuwa mpya
 
Kwa maana hiyo Lowasa hatakiwi tena kuhesabiwa ni Mtanzania? Amepoteza haki zake za uraia wa kushiriki maendeleo ya nchi kama raia wa kawaida? Kwamba CHADEMA NI CHAMA DHAIFU SANA HAKIWEZI KUMLEA NA KUMFANYA ABADILIKE KUTOKA UFISADI KWENDA UTANZANIA? Au kwa vile ccm imeshindwa unadhan Watanzania wote hawana uwezo wa kuwabadilisha watu?

Kwa sababu baada ya October, mafirauni wote walioko ndani na nje ya ccm watalazimika kubadilika na kutii sera na kanuni za UKaWA wapende wasipende. Watalazimika kuwa raia wema na hawatapata nafasi ya kutamba na ufirauni wanaodhani unatamalaki milele.

Ccm kwa kuwa hiawezi kubadilisha lolote huwa inawaua wanaokwenda kinyume nayo, lakini UKAWA, ninaamini hawana imani hiyo, wao ni watengenezaji nawarekebishaji wa watu kwa maslahi ya taifa.

Lowasa akijiunga na CDM jua kwamba CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi huu, kumbuka Lowasa ni ktk magamba yaliyoshindwa kuvuka wakati ule kama wamevua sasa thamani yake inatoka wapi hata CDM wamsafishe.
Huyu hafai hata kua nwanachama wa kawaida labda kama mnataka pesa zake.
Mtadharauliwa sasa mpaka kizazi cha tano.
 
Kusema akane Richmond wakati ni ya kwake, ni kuendeleza uharamia na ulaghai wa mafisadi. Hilo halikubaliki. Yeye kwanza kama ameona UKaWA ni njia sahihi, ajiunge na UKaWA kwa kukubali kwamba alikosea, akiri makosa na kukubali kukaa chini kama raia mwema. Asubiri UKAWA wamejipangaje kushughulikia wezi wa mali ya umma. Wakati huo ukifika, atashughulikiwa tu kulingana na ufirauni wake, namna anayoshirikiana au kutokushirikiana katika kurejesha mali za umma, kiwango cha ufirani wake n.k. sawa na mafisadi wengine bila kujali wako ndani ama nje ya ccm.

Ninaimani UKaWA si walipa visasi. Hawatakuwa na kisasi na mtu lakini wanakwenda kujeng amfumo wa kuliokoa taifa na mali zake.

Mkuu juzi kuna member aliweka bandiko hapa kuwa lowasa ajiunge cdm,lkn ajitokeze hadharani kukana na kuhusika na Richmond na awaombe radhi watanzania kwa kuwamo ktk kashifa hizo na watu wa mungu wamwombee atakuwa mpya
 
Mbowe anavyopenda pesa hawezi uziacha za Lowasa.
 
Kusema akane Richmond wakati ni ya kwake, ni kuendeleza uharamia na ulaghai wa mafisadi. Hilo halikubaliki. Yeye kwanza kama ameona UKaWA ni njia sahihi, ajiunge na UKaWA kwa kukubali kwamba alikosea, akiri makosa na kukubali kukaa chini kama raia mwema. Asubiri UKAWA wamejipangaje kushughulikia wezi wa mali ya umma. Wakati huo ukifika, atashughulikiwa tu kulingana na ufirauni wake, namna anayoshirikiana au kutokushirikiana katika kurejesha mali za umma, kiwango cha ufirani wake n.k. sawa na mafisadi wengine bila kujali wako ndani ama nje ya ccm.

Ninaimani UKaWA si walipa visasi. Hawatakuwa na kisasi na mtu lakini wanakwenda kujeng amfumo wa kuliokoa taifa na mali zake.

Upo sawa mkuu Tabby
 
Mkuu sijasema CDM wamsafishe na kumfanya mgombea wao. NINASEMA WAMPOKEE KAMA MWANACHAMA MCHAFU KAMA ALIVYO, WAMBADILISHE NA KUWA RAIA MWEMA!.

Hope umenielewa.

Lowasa akijiunga na CDM jua kwamba CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi huu, kumbuka Lowasa ni ktk magamba yaliyoshindwa kuvuka wakati ule kama wamevua sasa thamani yake inatoka wapi hata CDM wamsafishe.
Huyu hafai hata kua nwanachama wa kawaida labda kama mnataka pesa zake.
Mtadharauliwa sasa mpaka kizazi cha tano.
 
Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo. Pia unaweza kupewa fursa ya kutunga mtihani lakini usiusahihishe. Lowasa anataka kutunga mtihani na ausahihishe mwenyewe kwa haki bila upendeleo.Anataka kuhakikisha kuwa anaingia ikulu ili apambane na mafisadi anaowajua jicho kwa jicho ndio maana CCM wanamuogopa sana. Kuna siri kubwa sana anayoijua ndio maana wanaogopa akiingia madarakani itafichuka na atawaumbua na kutaifisha mali hizo
 
Japo kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa Lowassa ndiye anayetaka kwenda UKAWA au ni wafuasi wake ndio wanaotaka Lowassa aende UKAWA lakini Lowassa anayohaki ya kujiunga na chama chochote Kati ya vile vinavyounda UKAWA kama mwananchi wa kawaida yeyote anavyo weza akajiunga na UKAWA.

Ila ana takiwa awaheshimu viongozi atakaowakuta UKAWA na asijiunge UKAWA kwa ajili ya kutaka uongozi bali kama mwanachama wa kawaida,awachie viongozi na wanachama wa UKAWA atakao wakuta huko ndio wamfikirie kumpa uongozi kama watamuona anafaa kutegemeana na vigezo vyao.
 
Kwanini anaamini Sana katika rushwa? UKAWA mkimpa nafasi Lowassa mtakuwa wehu na wapenda rushwa kuliko CCM. Thamani yenu itashuka na mtadharauliwa milele
 
Back
Top Bottom