Kwanini Lowassa hawasaidii hawa kwanza kabla ya makanisa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa hawasaidii hawa kwanza kabla ya makanisa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Feb 20, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Edward Lowassa amepata umaarufu kwa kumwaga mapesa kwenye miradi mbali mbali hasa makanisani. Ajabu kuna wale wanaoitwa ndugu zake-wamasai, ambao hawasaidii! Je anachofanya Lowassa hakikaribii unafiki?

  Yesuanasema kuwa ndugu yetu wa kwanza ni majirani wenye shida
  Usipompendajirani unayemjua inakuwaje umpende wa mbali kama siyo kumtumia kwa malengo yasiri?

  Lowassaamekuwa akizunguka mikoani kutoa misaada ya pesa nyingi lakini hajiuliziwanafunzi wa Moita Sekondari wanakunywa na kufulia maji ya aina gani? Achiliambali wanafunzi wa Nanja Sekondari ambayo ilizinduliwa na Jakaya M.Kikwete nakutoa ahadi kibao lakini mpaka leo watoto wale wanasoma kwa kutumia chemli.
  Lowassa hajui wako wapi wakinamama wakijiji cha Arkatan ambao wanaishi kwa kutengeneza kokoto kwa mikono.Wala hajuiwako wapi leo Morani ambao wanaishi kwa kulinda wanaume na wake zao kwa kutumiasime na rungu usiku na mchana kuuza ugoro.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Nothing goes for nothing mkuu
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Kamanda.Lakini Lowassa anajisumbua na kujifilisi bure....hapati kitu mwisho wa mchezo wake huu
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli kabisa kwenye jimbo lake kuna shida sana ya maji, maeneo ya makuyuni wamasai wanapata shida sana na hata maeneo ya katikati ya makuyuni na mto wa mbu,
  Monduli kwa ujumla kuna shida ya maji na maeneo yenye maji ni Mto wa mbu kutokana na nature yake na Monduli mjini,
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  serikali haipo mpaka misaada yote unataka atoe Lowassa?

  Harambee, Minada na mavuno ni sehemu ya kutunisha mifuko ya kanisa inafanyika makanisa yote nchini na duniani kote sio lowassa aliyeanzisha ni kanisa lenyewe kwa maendeleo yake na waumini wake. Kama Lowassa anafanya hivyo anafanya kama muumini yoyote wa kikristo na naamini alikuwa anashiriki harambee hizo hata kabla ya kuwa kiongozi kwa sababu zipo siku zote na zitakuwepo hata Lowassa akiondoka dunia hii.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Harambee ni kisehemu kidogo tu cha njia zinazotumiwa na kanisa kutafuta fedha, Lowassa ni mkristo kutumika kwake sijaona kama ni makosa. zipo harambee ndogo ndogo zinazoendeshwa makanisani na huwa hazitangazwi naamini pia Lowassa ni mshiriki mzuri.

  Mara nyingi minada kanisani ni karibu kila jumapili lakini harambee hujitokeza pale kanisa linapotaka kufanya uwekezaji mkubwa kama mashule, hospitali, maji, umeme na miundombinu yenye gharama kubwa.

  Harambee kwa wakristo imeanza kuwa kama sehemu ya ibada kumzuia Lowassa ni sawa sawa na kusema viongozi wasionekane Ijumaa misikitini kwa kufanya hivyo wanachochea udini.

  Hata hivyo, lowassa amefanya Harambee misikitini na kutoa misaada kwa waislamu japo sio jadi yao.
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi huwa anaalikwa au hujialika mwenyewe, make kuna wanao dai kuwa huwa anaalikwa na kuna wanao dai kuwa huwa najialika, na hii ya kujialika inaweza kuwa na ukweli kwa sababu hata kipindi amejiuzulu Uwaziri mkuu alijiandalia mapokezi ya kufa mtu jimboni mwake,ni kama rafiki yake alivyo jiandalia watu wa kulia siku ile anatangaza kuachana na siasa za majitaka
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa mantiki hiyo unataka kusema Lowassa atatue shida zote kwao kusiwe na shida hata moja. Hakuna jambo kama hilo duniani kote ambako shida za binadamu zimekwisha
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Napata wasiwasi kama mleta mada ni great thinker kweli!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Harambee ni tukio na mara nyingi linakuwa na mgeni Rasmi hivyo kujiarika si jambo rahisi na mara zote kanisa husika lazima lipate kibali kutoka ngazi za juu kuhusiana tukio na wahusika.

  Rostam Aziz aliwahi kwendesha Harambee ya kanisa la KKKT usharika wa kinondoni kwa nia ya kutafuta fedha za kununua vyombo ya muziki lakini baadaye ikaonekana kanisa husika hawakupata kibali cha makao makuu. Mtafaruku ukatokea na kanisa husika liliambiwa na makao makuu kurudisha fedha ya Rostam Aziz.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lakimi pia mazoea yanaonyesha kwamba Harambee nyingi za kanisa zinatumia viongozi au watu maarufu kama Regnard Mengi kwa nia ya kupata mwitikio mkubwa wa wachangiaji.

  Ni hivi majuzi nilisikia waziri Agrey Mwanri alikuwa anaendesha harambee ya kanisa mara akatokea nyoka kwenye meza aliokuwa amekaa.

  Jambo hili linakuzwa pengine na watu wanaodhani kuwa mwanzilishi wa harambee makanisani ni Lowassa wakati kiukweli na yeye kazikuta na anaziendeleza akiwa sehemu ya waumini wa kanisa,
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli alizukuta, ila cha ajabu tangia ajulizulu ndo mialiko imezidi,
   
 13. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great thinkers mie naanza kwa kukiri kwamba hayo maeneo yalotajwa hapo awali siyajui yanahucka na Jimbo gani na kama yanahucka ndani ya jimbo lake la Monduli je wananchi wake, ikiwemo ngazi za chini za uongozi jimboni hapo washapeleka maombi yao kwa Mbunge wao au ni jitihada zipi wamezifanya ili kufikisha kero zao kwa mkulu wao? Ni mara nyingi huenda huko kwake monduli; kama aalikwavyo na hayo makanisa na kufanya harambee kwa maendeleo ya kanisa basi nao wanapaswa waangalie namna ya kuzfikisha kero zao"
   
 14. b

  braza makaptula Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu ni wapi umewahi kuona Mtu mmoja anatatua matatizo ya eneo lake bila kuwa hata na tatizo moja? tuache nadharia hata hayo makanisa anayoenda kuchangia anachangia yote? hayo makanisa yamemaliza matatizo yao yote?
  kuna mgombea mmoja Bw Patrick Quoro alikosa kura kwa kuwajibu hovyo wapiga kura wake wakati wa kampeni pale walipolalamikia kero ya maji, aliwajibu sasa mnataka mimi niweke mkojo wangu? hili gamba halikutumia Busara kwani lazimaangekuwa najibu lenye sababu za maana, KWANINI nimeanza na hiki kistory; Eneo kubwa la Monduli lina shida kubwa sana ya maji, maeneo yenye maji ni Mto wa mbu, Selela, Monduli juu na Engaruka, hii ni kutokana na vyanzo vya maji vya kutosha ambavyo ni vijito na maji toka kwenye mwamba kwa Mto wa mbu, maeneo yaliyobaki hayana vyanzo vya karibu zaidi ya kuchimba visima Virefu (Bore holes), sasa kitaalam maji yanayopatikana katika hizi bore holes hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na aina ya chumvichumvi zilizopo katika maji hayo hivyo ni vigumu watu hawa kuwa na maji ya kutosha, na hata vyanzo vilivyopo haviwezi kusafirisha maji ya kutosha kwenda maeneo haya yenye shida . Sasa unataka yeye afanye nini? awanyweshe mkojo wake? na ukumbuke kuwa ni jukumu la serikali kuleta huduma hii ya maji kwa wananchi kazi yake El ni kufuatilia serikalini, alichoweza kukifanya ni kutumia mabwawa ya maji ya mvua ambayo nayo si salama lakini angalau yanaokoa maisha ya watu

  lakini mbali na huduma ya maji ulitakiwa ufanye utafiti wa kutosha kuwa amefanya mambo mangapi ya maendeleo kwa wananchi wa jimbo lake, kwa jinsi anavyosaidia watu wake; maelezo yako uliyoyatoa hapo wananchi hawa hawatakuelewa na wanaweza kukuzomea. Lakini Kumbuka hakuna kiongozi aliye perfect kwa asilimia 100 ambaye amesaidia watu wake kwa kila kitu; na kama utakubaliana na kauli hii basi naomba umchukulie EL kama hao viongozi wengine
  naomba kuwasilisha
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Binafsi siwezi kupinga LOWASA kufanya harambee katika Nyumba za Ibada.

  Lakini turudi katika mtoa mada, kwani yeye ameainisha kuwa " KWA NINI ASISAIDIE NA MATATIZO YALIYOPO KATIAK JIMBO LAKE NA JAMII YA WAMASAI"
  Kama ilivyochangiwa ni kwamba jimbo lake lina matatizop ya kila aina ya kijamii lakini haendi kutatua hizo shida na badala yake anatumia pesa nyingi kusaidia makanisa au ndio kutimiza msemo wa kishwahili kuwa "HAKUNA MSAADA USIO NA MALENGO?"

  Aache kujionyesha kuwa ni mwema kwa majirani ikiwa nyumbani kwake haonyeshi wema wowote. Je ni busara kwa baba wa familiya kutoa misaada ya chakula kwa majirani na ikiwa watoto wake hawana hata unga wa kupika uji?
  TAFAKARIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lowasa anavunja ngome ya CHADEMA kanisani! Hii ni strategy nzuri kama akichaguliwa kuwa mgombea wa CCM 2015. Akijihakikishia 50% ya kura za kanisa tayari ni ushindi wa kishindo kwake, CDM wanaweza kuchukua hizo zinazobaki.
   
 17. l

  landiis Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu yaelekea huna upeo na mambo ya Kanisa, hivyo uwaache watu watende kazi ya Mungu ili nawe unufaike na rasilimali za Kanisa katika kada mbalimbali. Mhe, Lowasa anatumiwa na Kanisa akiwa ni mtu mwenye uwezo wa kuchochea na watu wakajitokeza kuchangia Kanisa ili ijiendeshe. Pili kwa mawazo yako unataka hata Mheshimiwa afanye kila kitu, kugonga kokote ni sehemu ya ajira aliyochagua mtu na hawezi kumsaidia mtu mmoja mmoja ndio maana anafanya hivyo kupitia vikundi halali.
   
 18. a

  adobe JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  friend kuwa mwelewa,lowasa hasaidii makanisa bali anaombwa na kanisa aongoze harambee,pia kusaidia kanisa ni kusaidia jamii nzima kwa kuwa huduma za kanisa hazibagui hata kawa we ni gaidi utatibiwa peramiho,kcmc na bugando kama mgalatia anavyotibiwa
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  wakati umefika sasa wa kutafuta Rais kwa kuangalia vigezo kwamba tangu aongoze kawatendea nini wananchi wake, kafanya nini cha kuwaondoa kwenye umaskini hasa miradi yasije yakawa kama ya Mzee Rostam Aziz Igunga
   
 20. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Kumbe Monduli ndo zao la hawa wasuka rasta na wauza madawa ya kienyeji wanashinda machinjioni usiku wanalinda wanaume wenzao hii kali....mie nilidhani kulingana na juhudi za huyu jamaa hawa ndugu zake waMasai watakua wamehamasishwa tosha na huyu jamaa kusoma na sio ****** wanaofanya mikoani yani ni kelo utadhani tunaishi polini wengine hatujazoea masime,mikuki wala marungu utadhani wanaenda kupigana.....always charity begins at home......LOWASSA ukitaka uonekane wa maana anza na watu wako kwani wamepotea na wanazagaa mitaani utadhani mbuzi aliye kata kamba
   
Loading...