Kwanini Lowassa alipougua alikwepa kwenda India lakini alikwenda 'kwa babu' Loliondo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa alipougua alikwepa kwenda India lakini alikwenda 'kwa babu' Loliondo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwamakula, Oct 29, 2011.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sakata la viongozi wetu kuugua magonjwa limeshika kasi na kila anaye ugua anachukua hatua za kujitibu kwa nafasi yake.


  Wapo watu wanao singizia kuwa magonjwa yanayo wakabili mwakyembe na mwandosya ni kutokana na sumu au mambo ya kisiasa.

  Mbana jakaya kikwete alipoanguka jangwani wakati wa kampeni za siasa watu hawakuhusisha sumu wakati wabaya wake wote waliukuwepo hapo????


  Ukwewli ni kwamba viongozi wetu ni wagonjwa wa magonjwa sugu na ugonjwa hauchagui fisadi au mpambanaji wa ufisadi !!!
  Wote wanaugua tu!!!

  Ni fikira za kukosa ukweli kusingizia sumu.!!!!!

  Nyerere aliugua ugonjwa wa ajabu sana na kila siku madaktari walikuwa wanagua magonjwa mapya !!!!
  Je nina katika viongozi waliopo anaweza kumufikia nyerere???
  Wakati wa tiba ya babu vigogo wote walikwenda loliondo na wakaficha magonjwa yao!!!!


  Lowasa alikwenda loliondo kutibiwa na amekuwa akihaha kwenye maombi nigeria wa nabii joshua , juzi ameonekana uk kwenye matibabu, kwa nini wasisemi ni sumu???
  Lowasa anahekima alipo ona mwandosya yupo india yeye akakwepa kwenda uk .


  Huko loliondo mafisadi wote walikuwa wanatibia sehemu moja na wabambanaji wa ufisadi bila kujali wate walipanaga foleni!!!!.
  Ni bora tuakaondoa fikra za imani potofu na kufikria matendo yetu kabla ya kuugua!!!  Wakati wa vikao vya bunge machangudoa wanajazana dodoma sasa matunda yake ndio hayo!!!
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=2]90 % ya viongozi wetu wenaugua magonjwa sugu , wanashindwa kufanya maamuzi[/h]
  Mapema mwaka huu viongozi wetu wa juu wakiwemo wabunge,mawaziri, majaji , wakuu wa mikoa, watendaji wakuu wa serikali walimiminika loliondo wakitaka kutibiwa magonjwa sugu ukiwemo ukimwi.mch ambilikile mwasapila (babu) aliwalaghai vigogo wa serikali na serikali yote kuamua kuelekea huko.
  Magonjwa sugu yaliyotajwa ni:
  1.ukimwi
  2.kisukali
  3.pressure
  4.
  5.
  Taarifa za daktari zinaonyesha kuwa watu wenye magonjwa sugu huwa wanhasira kali na kushinda kufanya maamuzi magumu na kukosa mipango endelevu. Wanauza mali hovyo na kutapanya rasilimali

  pamoja na kwamba dawa ya babu haitibu ukimwi lakini amefanikiwa kutupatia takwimu za ukweli kuhusu mtandao wa magonjwa sugu kwa viongozi wetu ambapo wametumia ndege kwenda loliondo na magari ya serikali.
  Ni dhahili kuwa viongozi wetu wanao tuongoza ni wagonjwa wa magonjwa sugu kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi mazito na mipango ya maendeleo y mda mrefu.

  Viongozi wetu wanahofu ya kufa kutokana na magonjwa yao na ndio maana wanauza madini, wanauza ardhi, wanauza wanyama hai mapema ili kukusanya pesa mapema.
  Wengi tunajua mtu akiwa na hofu ya kufa kutokana na ukimwi huwa anauza mali hovyo hovyo na maamuzi yake siyo mazuri.

  Mfano mzuri ni maamuzi ya kulipa dowans , jambo ambalo ni dhahili kwamba wanaofanya hivyo hawana mipango mirefu ya maisha katika taifa hili.
  Viongozi wa ccm wanakata kuachia madaraka kwa watu wengine wakihofia hatima yao baada ya kuuza nchi na wanyama nje ya nchi. Wametapanya mali hovyo kwasababu hawana mawazo mazuri, wanang'ang'ia madaraka na kutaka watoto wao walithishwe urais , ubunge, na uwaziri ili kulinda uhalifu waliofanya.wanahaha kuiba kura ili waonekane wanapendwa na wananchi.


  Mgogoro uliotokea libya ni sawa na mgogoro utao tokea tanzania 2015.
  Huko libya gadafi alitaka kuachia madaraka mikononi mwa watoto wake ambao nao wamejilimbikizia mali lakini raia wema wakamuonya lakini hakusikia.


  Hapa tanzania kuna juhudi kubwa za watawala wetu kutaka kurithisha madaraka kwa watoto wao ambao wamejirimbikizia mali katika vituo vya mafuta, migodi , maliasili, wameuza ardhi na sasa wanahaha kuiba kura.!!!!

  Kuna harakati kubwa kwa watu ambao wametuhujumu , wametuibia , wametunyonya na sasa haohao ndio wameunda mitandao ya urais 2015. Wanatumia fedha walizotuibia kutuhonga ili tuwape kura. Wanatumia pesa hizo kuwahonga wachungaji, wamewanunua wachungaji na kufanya kampeni makanisani.


  Watu hawa wakiugua tu utasikia walalahoi wanalalamika na kupiga kelele kuwa wamepewa sumu lakini safari ya loliondo walikwenda bila mtu kulalamika.wanasafiri kwenda india kutibiwa baada ya loliondi kupoteza umarufu lakini wanapo ondoka hawasemi wanaumwa nini !!!!!! Mauaji ya albino yanaongezeka ushirikina huku serikali ikiongeza kasi ya kutoa vibali kwa waganga .waliopo kwenda loliondo hawakusema wanaumwa nini!!! Lakini safari ya india ina maneno mengi


  ni bora mbunge ,waziri, vigogo wanapougua waangalie ukweli wa afya yake sio kusingizia sumu .

  Pia hapa kuna ubaguzi mpiga kura akiugua anafia nyumbani bila kufika hata dispensary, na hata akienda huko anakosa dawa.

  Wajawazito wametengewa bajaji ambazo bado zinasuasua.

  Waziri akiugua anakimbizwa haraka kwenda india na anagharimiwa fedha nyingi inayo weza kutibua zaidi ya walalahoi 100 hapa!!!

  Wakati wa kupiga kura wabunge wanapiga magoti kuomba kura, wakimunyima anachakachua!!! Je, ni haki????​
   
 3. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwamakula, umesema kweli, ingawa ni kweli ngumu kuitafuna. Ndiyo maana uchangiaji wa thread yako, umedorora.
  Umedorora, kwa sababu katika mila na desturi za Watanzania; ni ajabu kwa wanasiasa maarufu kuugua; na hata wakiugua,
  basi siyo magonjwa sugu kama UKIMWI. Ndiyo maana wakiugua, basi tunawaza haraka kwamba, huenda "wamepewa sumu".


  Ingawa Watanzania wengi hatutaki kukubali hadharani, lakini ni dhahiri kwamba, wanasiasa wengi maarufu, wanaumwa magonjwa sugu; hususan UKIMWI. Jambo hili lilidhihirika, kutokana na jinsi wanasiasa hawa, kwa wingi wao; walivyomiminika kwenda Loliondo kwa Babu. Asikudanganye mtu! Watu wengi waliokwenda kwa Babu, kilichowavutia kwenda huko, ilikuwa tiba ya UKIMWI; na magonjwa yale mengine yaliyokuwa yanatajwa, yalikuwa ni danganya toto tu. Sasa tujiulize, kwa nini tunashindwa kuwa wazi kuhusu magonjwa ya wanasiasa maarufu?


  Kama tunalipenda taifa letu, hatuna budi kuuacha utamaduni wetu huu. Tabia hii ya wanasiasa maarufu, kushindwa kuwa wazi kuhusu magonjwa yao, siyo tabia njema; itakuja kuliangamiza Taifa letu lote. Wanasiasa hawa, ni kioo cha jamii. Wakishindwa kuonesha mfano, ni vigumu kutarajia kwamba watu wengine, watamudu kuwa wazi kuhusu magonjwa yao.


  Tujifunze kwa wenzetu, katika nchi ya Zimbabwe. Mwezi wa Juni, mwaka huu wa 2011; Makamu wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Thokozani Khupe, alitangaza hadharani kwamba, ingawa bado ana nguvu ya kufanya kazi; hata hivyo anaumwa Saratani (Kansa) ya Matiti. Baada ya kauli hii, Spika wa Bunge la Zimbabwe, Lovemore Moyo; alimpongeza hadharani mwanamke huyu, na kumtaja kuwa ni mwanasiasa wa kuigwa; kwa jinsi alivyokuwa wazi, kuhusiana na ugonjwa unaomsibu.


  Gazeti la Zimbabwe Standard la Oktoba 2 mwaka huu wa 2011; pia lilimnukuu Spika wa Bunge Moyo, akisema jana yake
  hadharani kwamba, wabunge wengi wa Bunge la Zimbabwe, wana UKIMWI, na baadhi yao wamefiwa na wenzi wao (waume/wake zao); kutokana na UKIMWI.


  Kabla ya hapo, mwezi wa Septemba, mwaka huu wa 2011; Rais Robert Mugabe, yeye naye; alisema kwamba anawajua
  Viongozi wengi wa juu wa Serikali, wenye virusi vya HIV, ambao wanatumia ARV's (dawa za kurefusha maisha). Akasema
  kwamba, pamoja na kwamba viongozi hawa wameathirika, bado wanawaambukiza UKIMWI, watu wengine; bila kujali. Akawaonya wasifanye hivyo, ili kulinusuru taifa hilo lenye waathirika wengi wa UKIMWI.


  Katika hatua nyingine, mwezi wa Juni, mwaka huu wa 2011; Mwandishi wa kike wa Gazeti la B-Metro, Simiso Mlevu; alimpeleka mahakamani, Mbunge wa Bulawayo-Insiza, Siyabonga Ncube (MDC-N); kwa kumwambukiza UKIMWI, huku akijua kwamba anao. Simiso alidai kwamba, amekuwa ni rafiki yake Ncube, kwa miaka miwili; baada ya mkewe kufariki. Aliendelea kusema kwamba ingawa Ncube alimficha, hata hivyo, alikuja kuthibitisha baadaye kwamba; mkewe Ncube alifariki kutokana na UKIMWI.


  Huo ndiyo uwazi uliopo kwa watu wa nchi ya Zimbabwe, wanajua kwamba hata wanasiasa maarufu wanaweza kuugua
  magonjwa sugu, na hata UKIMWI. Hivyo sivyo ilivyo kwetu Watanzania. Kwetu sisi, wanasiasa maarufu wakiugua, wanakuwa "wamepewa sumu". Tumefikia mahali pa kudanganyana kwamba, mwanasiasa fulani amepelekwa India, kwa sababu ya vijidudu 150 vya Malaria. Je, uongo huu ni kwa faida ya Taifa letu? Na je, wanasiasa wanaposhindwa kuwa wazi juu ya magonjwa yanayowasibu; TANZANIA ISIYO NA UKIMWI, KWELI INAWEZEKANA? Katika nchi yetu, eti UKIMWI ni maradhi ya walalahoi tu, lakini wanasiasa maarufu, wao, hawawezi kuwa nao. Tunamdanganya nani? TUTAFAKARI!

   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wanasiasa wengi niseme karibuni wote sio wakweli. Leo hii ukisema uende pale bungeni ili waheshimiwa wakapime afya zao [UKIMWI] ,sintashangaa kuwa asili mia kubwa ya waheshimiwa hawa wanaweza hata kukimbia kuhudhulia vikao kwa kuogopa kupima; na hili ni kwa wote wanaume na wanawake!! Halafu wakiwa majimboni wanapanda kwenye majukwaa kuwahamasisha wananchi juu ya matumizi ya condom wakati wao wenyewe pengine hata hawazitumii!! Si mnakumbuka mambo yaliyomkuta mzee mzima Jacob Zuma huko bondeni halafu akaenda kupata shower!!
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Je wewe umepima?
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwaka 2007 rasi jakaya mrisho kikwete aliwahi kukemea viongozi wa serikali ambao wana virus vya ukimwi lakini wanatumia pesa zao kusambaza. Lakini baada ya hapo hakuna kiongozi yoyote aliye chukuliwa hatua zaidi ya kumufunga amatusi lyihumba wa bot ambaye anatajwa kufanya ngono na vick kamata (viti maalum ccm).hapo inatupa kujua kwamba kauli yake ilikuwa si ya kiserikali bali kifamilia.
  Pia mwaka 1999 na 2000 kulitokea malumbano makali kati ya mkapa na augustino mrema kuhusu mkapa na wabunge wote kupima ukimwi.

  Wabunge wenge walipinga hoja hiyo na wengine wakakimbilia nje ya nchi kupima ukimwi ili wasijulikane. Na hii ndo sababu kubwa wabunge wanakimbizwa kutibiwa india ilikuficha ukimwi.  Wapo wanasiasa walioshauli , wanafunzi wa vyuo vikuu wapimwi ukimwi kama kigezo cha kujua afya ya mtu ili wanapopata mkopo serikali ijue hatima ya malipo.
  Katika form ya afya vyuo vikuu , ukimwi haupimwi , wanapima kifua tu!!!
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mwamakula maneno yako ni ya kweli,ila mfumo wetu [system] ndiyo imetufikisha hapa,Kwa kuwa viongozi wengi kweli ni wagaonjwa.Na kwa wataalamu wagonjwa wengi wa ugonjwa wa UKIMWI wanamaamuzi ya ghadhabu [hasira na hamaki].Yaani maamuzi yao mengi yamekaa kwa upande wa kuona kama amenyenyapalia na kuwa watu wanajua yeye ni mfu mtarajiwa.Na wengi wameshajiwekea kuwa ukiwa Mgonjwa wa UKIMWI basi pona yako ni kujilimbikizia Mali kwa kuwa utaweza kujitibu kwa gharama yoyote hile.Basi walichofanya ni kujilimbikizia mali kwa namna yoyote ile na kwa gharama yoyote ile ya Watanzania.

  Na kwa kuwa wengi wako kwenye mfumo kwa kujua nini kinaendelea juu ya Nchi tofaouti na watanzania walio wengi [Majority] wamejilimbikizia wao kupitia wahindi na waarabu kwa kujua wanatunziwa siri za uovu wao.

  Hakika matendo ya uovu gharama zake ni hapa hapa duniani, wengi wameshaanza kudhulumiwa na wahindi na waarabu hao, wakiwa bado hai,na pindi wakifa kabla ya Tanzania kupambazuka watoto wao wengi watadhulumiwa na watu hao kwa kuwa watu hao wanajua mabenki na miladi yao mingi inamilkiwa nao iko wapi na nani anahusika nayo.

  Kibaya ni kuwa wanamsemo wa PONDA MALI KUFA KWAJA.Ponda mali hiyo imekuwa ni gharama ya Watanzania kula mlo mmoja na shida kwenye mahospitali yao.

  Na kikubwa zaidi wahindi na waarabu wachache wameshajiundia kikosi kazi kikiwa na kiongozi mwenye kusimamia mikakati ya kutumia udhaifu wa kuwafanya mateka [slave] viongozi walioiba kwenye Taifa kwa kuwa wanajua madhambi yao,na hao wahindi na waarabu wamefikia kuwa wanamilki viongozi sehemu hatari, ukiondoa jeshini.Wamepachika watu wao kufanya kazi kwa niaba yao wakiunda ufalme [Empire] ya kulinda na kuchuma zaidi uku wakiwa na walinzi na watekelazaji waliowafikisha hapo walipo.

  Pata picha kiongozi wa idala anatafuta mtu wa kusimamia sehemu [section] kama msimamizi [foreman] kisha mtu Nje ya Ofisi, asiye mfanyakazi wa ofisi kisa tu ni rafiki ya mkuu wa idala, hivyo anachukua nafasi ya kumtafutia kiongozi wa idala mtu huyo na kumwambia kuwa Mkuu huyu anakufaa hapa unapotaka mtendaji.Swali liko je huyu foreman atawajibika kwa nani Je ni kwa mkuu wa Idala ambae hamjui au ni kwa Rafiki ya Mkuu wa Idala ambae anajua aliko mtoa huyo foreman.

  Basi matendo mengi yetu yako kwenye hali hiyo ya wakubwa wengi wako vifungoni [slave] mwa wahindi na waarabu wengi kwa kuwa wengine wamefika ngazi kubwa kwa kupitia connection za hao wahindi na waarabu.Hivyo awawajibiki mahusisi kwa viongozi walio juu yao bali kwa wale waliosababisha wao kuonekana na kupewa uongozi.

  Ila uzuri wa asilia [Nature] kwa kuwa matendo yao ni kinyume na mapenzi ya Mungu, basi wasubilie kuumbuka na kuacha laana ya kwa vizazi vyao mfanno wameuona kwa gadhafi na wanae.Na hao waarabu na wahindi watatafutwa popote pale watakapokimbilia dunia hii.Ni swala la Muda kwa kuwa Muda ukifika hakuna wa kulizuia.

  Hata Rais wetu hili muda analijua kuwa muda ukifika hakuna cha kuzuia hili analijua kwa kuwa maneno haya haya alipata kuamba na Mzee Thabit Kombo, wakati amepigwa zengwe,mzee yule alimwambia atulie tuli kwa kuwa "Mungu akipanga na muda ukafika basi hakuna wa kuzuia", na kweli muda wake ulipofika waliajaribu kumzuia lakini walio wengi waliona kishindo chake. Basi usemi huo huo mali ya watanzania kuwaludi watanzania na kuludisha heshima yao muda ukifika haitakuwa na shida itakuwa lahisi kama kumsukuma mlevi kwenye kolongo.

  Time will tell.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Thread yako imeeleweka kwako tu!
   
 9. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tanzania inawezekana bila ukimwi kama wabunge wataongoza harakati za kutoa elimu kivitendo. Rais kikwete alisha fungua kampeni ya kupima ukimwi lakimu majibu yanabaki siri, ila mtu wa manzense akifa wanasema ni ukimwi, lakini mtu wa upanga akifa wasema sumu au pressure.
   
 10. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wetu ni wagonjwa wanahitaji maombi, zote tumewashuhudia wakianguka wakati wa kuomba kura.

  Nawashauli kitu kimoja , wawe wakweli na wasikimbilie kwa waganga wa kienyeji , maana mauaji ya albino yanarejea kwa kasi sana
   
 11. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Shida kubwa ya watanzania hatufanyi body check up.. matatizo ya zitto amekuwa nayo for the last 12yrs.....

  Na shida nyingine kubwa ni kwamba Hospitali yenye vipimo sahihi kwa sasa ni Muhimbili... Sasa watanzania milioni 47 tunaweza kupata matibabu wote pale kweli... na kupona kweli kwa masikini ni shida sana......
   
 12. o

  onchoseciasis Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona mnaandikia mate wakati wino upo? kwa nini msiwataje hapahapa JF hao waheshimiwa ambao mnauhakika kuwa wana viruirui? hii itasadia kubadili tabia zao; pia kutambaa kwenye maneno wanayohubiri majukwaani kila siku!
   
Loading...