Kwanini linapokuja suala la kutumbua wabunge wetu watendewe tofauti. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini linapokuja suala la kutumbua wabunge wetu watendewe tofauti.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Feb 16, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania kwa pamoja tumekubaliana kwamba kutokana na majukumu makubwa waliyonayo Viongozi na watendaji waandamizi serikalini, ambayo yanahitaji akili iliyotulia, kuna umuimu mkubwa kutumia rasilimali kidogo tuliyo nayo ili kuhakikisha watu hao wanaishi peponi; hata kama kwa kufanya hivyo italazimu wananchi wa kawaida/wadogo waishi kwa kula majani. Wabunge wetu wako katika kundi hilo adimu. Kinachonishangaza, ni kwanini wabunge hao wamepewa shs.90 milioni tu kwaajili ya kununua gari, wakati magari iliyopewa mihimili mingine ya dola yana thamani ya shs. 200 milioni na kuendelea!
   
Loading...