Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,312
- 10,494
Nimeangalia tangu ile series ya mh Lowasa kutembelewa na wachungaji, mashehe na watu mbali mbali kushawishiwa kugombea urais sikuwaona hawa maparokia wakijiunga na safari ya matumaini. Nikaangalia pale Karume kwenye ufunguzi wa kutia nia sikuwaona maparoko au maaskofu wa Kikatoliki wakijitokeza waziwazi kumuunga mkonyo mheshimiwa. Je, hawa wapendwa tuseme hawapo ktk ile safari ya matumaini?
KWAYA
Imejitokeza tabia ya wasanii wa nyimbo za injili kuwaimbia watia nia na kuwanadi. Alianza Bahati Bukuku, niliyemheshimu kuanza kumuimbia Mh Lowasa huku akimfananisha na Mfalme Suleiman. Kabla, sijaishiwa mshangao nimeshuhudia Rose Mhando, Matha Mwaipaja, Njole, Bon Mwaitege na mama wa maadili nimpendae Upendo Nkone wakiimba eti wana imani na Mwigulu Nchemba. Hapa nikaona kweli injili inatumika kupiga mihela na hawa wanaotuimbia daima injili. Hawana tofauti na Diamond au Linux au Kiba au Mzee Yusufu.
Cha ajabu hawa wakatoliki na kwaya zao siwaoni wakimuimbia au kumnadi mtia nia wa CCM au UKAWA. Sasa najiuliza, wenyewe tuwaweke kundi gani?