Kwanini kusiwekwe sheria inayodhibiti matumizi ya simu kwa mtoto chini ya umri wa miaka 18?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,856
Maswala ya watoto naona hayazungumuziwi sana humu,kuna sheria nyingi zinazomtetea mtoto lakini zinazomkemea mtoto pia ni chache sana. kwa kuanza,nashauri kuwe na sheria inayomkataza mtoto kutumia simu akiwa chini ya umri wa miaka 18!!
Nawasilisha
 
Kuna logic kwenye pendekezo lako kwa sababu kisheria mtoto wa miaka chini ya 18 anaitwa 'minor' na haruhusiwi kuingia mkataba wowote wa kisheria na pia kwa hapa tz hawezi kuomba wala kuruhusiwa kumiliki silaha (bunduki, bastola)

Sababu ni kwamba umri huu huhesabika kama umri usiokuwa na maamuzi timamu.

Ni vizuri pia sheria ikatamka wazi kwamba umri huu haruhusiwi kumiliki simu kwani hawezi kufanya maamuzi timamu ya mawasiliano, anaweza kulaghaiwa ikaleta maafa.
 
nadhani ipo lakini kwa wanafunzi...ila kwa kifupi sheria za watoto bongo bado sana yaani hizi zilizopo bado zinautata sana hazimlindi mtoto kivile na pia nyingi ni copy pest na international conventions ambazo sio sheria ni maazimio tu
 
Asishike simu ili iweje, Wabongo hatuendelei kwa sababu ya fikra zenye giza kama hizi,

Unaona upande wa negative tu, tangia ukue hujaona umuhimu wa simu?

Mimi nashauri akizaliwa tu apewe simu baada ya maziwa.

Ila sio goroka.

Maana yangu ni (internet access) tangu akiwa mdogo
 
Ikiwa lengo ya matumizi mazuri na chini ya usimamizi wa wazazi hakuna shida tofauti na hapo hatua zichukuliwe.
 
Back
Top Bottom