Kabla ya miezi 6 mfumo wa umeng'enyaji wa chakula unakuwa haujakomaa. Kumpa mtoto chakula kabla ya miezi 6 inaweza kupelekea kuongezeka uzito kupita kiasi, kupaliwa, kukosa choo, kutapika, kuharisha, n.k. na hii yote ni hatari kwa afya ya mtoto.
Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji wa mtoto, kuanza kumpa vyakula vigumu ni kumharakisha mtoto.
Na siyo chakula tu, hata maji ya kunywa mtoto anapaswa kuanza kupewa baada ya miezi 6. Yaani, maziwa yanajitosheleza kwa 100%.