Kwanini kujadili spika wa kwanza mwanamke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kujadili spika wa kwanza mwanamke?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Nov 19, 2010.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanadamu wapo katika jinsi ya kike na kiume. Utambulisho wa jisi hizo upo katika maumbile (uke na uume -maumbile yanayotoa tofauti za msingi). Hivyo ndivyo walivyoumbwa. Ili kuendeleza uumbaji huo lazima jinsi (wakati mwingine tunatumia neno jinsia) hizi mbili zishirikiane ili kumpata mwanadamu mwingine.

  Juzi juzi amechaguliwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kuwa spika wa Bunge la Tanzania. Kitu kinachonishangaza ni kuwa wengi wanampongeza tu kwa sababu ametengeneza historia ya kuwa spika wa kwanza mwanamke. Hilo la jinsia ya spika aliyechaguliwa limepewa umuhimu. Wakati wanaume wanapata nafasi ya kuwa spika wa kwanza halikupewa umuhimu.kama kuna waliojitokeza kumpongeza kwa sababu ya uwezo wake ni wachache na kama wapo walilitaja hilo la uwezo baada ya kutanguliza pongezi kwa sababu ya kuwa mwanamke.

  Nafasi za uongozi zinapoombwa mtu anataja uwezo wake na uzoefu katika nafasi anayoiomba. Kama kuna suala la kutaja jinsi (me au Ke) ni katika hali ya kujitambulisha tu lakini siyo katika suala la kustahili au kufaa kwa ajili ya nafasi fulani.

  Kama kuna suala la mtu kutanguliza na kutumia kigezo cha jinsi kama sifa na uwezo wa kupata nafasi linahusika katika suala la uumbaji tu(kuzaa). Kama mwanaume anataka kumpata mtu wa kuzaa naye basi ni fursa ya mwanamke kujitokeza kupata nafasi ya kugombea kupata fursa hiyo.

  Anne Makinda aligombea nafasi ya kuongoza bunge. Hilo halikuhitaji spika awe na sifa ya kuwa mwanamke, hata kama atakayepata nafasi hiyo angekuwa mwanamke. Je, alipoanza kuongoza bunge kuna kitu chochote chenye uhusiano na jinsi yake?
   
Loading...