Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Kwasababu ya maneno ya nje (ndugu, marafiki, majirani) ,pia mwanaume kutaka kuonyesha kwamba sio yeye mwenye matatizo. Kwenye jamii yetu bado wapo wanaume na ndugu zao wanaoamini kwamba wasipojaaliwa mtoto kosa ni la mke. . tatizo ni la mke na haiwezekani likawa la mwanaume. Kama vile tu wengine wanapoendaga kuzaa nje eti "natafuta mtoto wa kiume/wa kike" akidhani mwanamke ndie anaeleta tofauti kumbe yeye ndio hana kinachotakiwa kusababisha mtoto wa kike/wa kiume.Sijui hawakusoma bailojia, maana watu wenyewe utakuta wamesoma.
a) Ndio inawezekana ila inategemea na malengo yao... na inabidi malengo yao yafanane au angalau kuwe na makubaliano kati yao.
b) Sidhani kama ni LAZIMA. . . ila sisi tumeshajizoesha kwamba ndivyo inavyotakiwa. Kwahiyo watu wakichelewa kwasababu yoyote ile tayari maneno yanaanza . . . na kama hao wanandoa ni watu wakuridhisha watu wa nje ya ndoa yao zaidi lazima wataanza kukorofishana ikiwa mmoja hatokua tayari/hawezi kufanikisha hilo takwa la ndugu/marafiki/majirani. Na hapo ndio huo ULAZIMA unakuja.
c) Kwanza kabisa inatokanana ego. . . .kila mmoja wao au mmoja wao tu utakuta anaamini kwamba mimi sio mwenye matatizo sasa kwanini nisiwe na damu yangu?Bora nitafute mtu mwingine nizae nae. Hayo mawazo ya "mimi niko fit" ni kimoja ya chanzo.Ila kingine ni kwamba bado kwenye jamii yetu hatujazoea swala la kuadopt. . . nadhani kuna siku hata hapa JF mtu aliweka thread akiulizia process kwasababu anataka kuadopt watu wakamuuliza kwanini asizae tu wakwake? Yani bado tuna yale mawazo ya "kwanini nimlee mtoto ambae sio wangu wa damu". . . tusubirie siku tukibadilika labda na baadhi ya ndoa zitasurvive.
Kama kuna wakati mgumu wakati mwingine kwa wanandoa wapya ni kuchelewa kupata mtoto. Wakati mwingine watu wanaamua kwa makusudi kutopata mtoto mara moja huku wakijitahidi kujipanga vizuri. Mgogoro mkubwa huanza mwaka mmoja baada ya ndoa kama hawaoni kile kinachoitwa "tunda la ndoa". Maswali yanabakia:
a. Je watu wanaweza kukaa pamoja na kuamua kuishi pamoja bila kutaka watoto?
b. Je ni lazima kupata mtoto mwaka wa kwanza wa ndoa? au hata mwaka wa pili?
c. Ni kwanini watu ambao hawajajaliwa mtoto huona bora kuachana kuliko kuchuka mtoto wa kuamua kulea (adoption)?
MMM
umenitonesha hapa, acha nikae kimya nisome comments tu
Wakuu ndoa yenye mtoto ina raha yake, acheni kabisaaa! Mimi nna jamaa yangu hadi leo hii, tar 28/11/2011 hana mtoto na hakuna dalili kabisa maana wamezunguka nadhani hospitali zote dar, ngoma bado bila bila.
Juzi kati nikakutana nae nilipomuuliza kama ana mtoto, alibaki kuangalia chini, wala sikuendelea kumuuliza nikajua it was not a good question.
'Mgonjwa' poleeeeeeee! Usijali 'utapona', hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
ni wachache sana, 10/1,000,000 ambao huwa wanaamua 'kupitisha siku' bila kuzaa baada ya ndoa. wengi wetu huwa tunataka immediate outcome coz kwa baadhi ya wanawake, mtoto ni security na ni 'strong bond' ya uhakika kwa familia ya mume!
Kwasababu ya maneno ya nje (ndugu, marafiki, majirani) ,pia mwanaume kutaka kuonyesha kwamba sio yeye mwenye matatizo. Kwenye jamii yetu bado wapo wanaume na ndugu zao wanaoamini kwamba wasipojaaliwa mtoto kosa ni la mke. . tatizo ni la mke na haiwezekani likawa la mwanaume. Kama vile tu wengine wanapoendaga kuzaa nje eti "natafuta mtoto wa kiume/wa kike" akidhani mwanamke ndie anaeleta tofauti kumbe yeye ndio hana kinachotakiwa kusababisha mtoto wa kike/wa kiume.Sijui hawakusoma bailojia, maana watu wenyewe utakuta wamesoma.
a) Ndio inawezekana ila inategemea na malengo yao... na inabidi malengo yao yafanane au angalau kuwe na makubaliano kati yao.
b) Sidhani kama ni LAZIMA. . . ila sisi tumeshajizoesha kwamba ndivyo inavyotakiwa. Kwahiyo watu wakichelewa kwasababu yoyote ile tayari maneno yanaanza . . . na kama hao wanandoa ni watu wakuridhisha watu wa nje ya ndoa yao zaidi lazima wataanza kukorofishana ikiwa mmoja hatokua tayari/hawezi kufanikisha hilo takwa la ndugu/marafiki/majirani. Na hapo ndio huo ULAZIMA unakuja.
c) Kwanza kabisa inatokanana ego. . . .kila mmoja wao au mmoja wao tu utakuta anaamini kwamba mimi sio mwenye matatizo sasa kwanini nisiwe na damu yangu?Bora nitafute mtu mwingine nizae nae. Hayo mawazo ya "mimi niko fit" ni kimoja ya chanzo.Ila kingine ni kwamba bado kwenye jamii yetu hatujazoea swala la kuadopt. . . nadhani kuna siku hata hapa JF mtu aliweka thread akiulizia process kwasababu anataka kuadopt watu wakamuuliza kwanini asizae tu wakwake? Yani bado tuna yale mawazo ya "kwanini nimlee mtoto ambae sio wangu wa damu". . . tusubirie siku tukibadilika labda na baadhi ya ndoa zitasurvive.
Nadhani kwa udadisi wa mwanakijiji lengo lake ni kupata mawazo kwa nini siku hizi vijana wanazaa kwanza halafu ndoa baadae au mabibi harusi wengi wa sasa wakiwa kwenye wedding na mimba ya miezi sita juu.