Kama kuna wakati mgumu wakati mwingine kwa wanandoa wapya ni kuchelewa kupata mtoto. Wakati mwingine watu wanaamua kwa makusudi kutopata mtoto mara moja huku wakijitahidi kujipanga vizuri. Mgogoro mkubwa huanza mwaka mmoja baada ya ndoa kama hawaoni kile kinachoitwa "tunda la ndoa". Maswali yanabakia:
a. Je watu wanaweza kukaa pamoja na kuamua kuishi pamoja bila kutaka watoto?
b. Je ni lazima kupata mtoto mwaka wa kwanza wa ndoa? au hata mwaka wa pili?
c. Ni kwanini watu ambao hawajajaliwa mtoto huona bora kuachana kuliko kuchuka mtoto wa kuamua kulea (adoption)?
MMM
Mzee Mwanakijiji;2893710]Kama kuna wakati mgumu wakati mwingine kwa wanandoa wapya ni kuchelewa kupata mtoto. Wakati mwingine watu wanaamua kwa makusudi kutopata mtoto mara moja huku wakijitahidi kujipanga vizuri. Mgogoro mkubwa huanza mwaka mmoja baada ya ndoa kama hawaoni kile kinachoitwa "tunda la ndoa". Maswali yanabakia:
a. Je watu wanaweza kukaa pamoja na kuamua kuishi pamoja bila kutaka watoto?
b. Je ni lazima kupata mtoto mwaka wa kwanza wa ndoa? au hata mwaka wa pili?
c. Ni kwanini watu ambao hawajajaliwa mtoto huona bora kuachana kuliko kuchuka mtoto wa kuamua kulea (adoption)?
MKJJ wewe una mtoto?Kama kuna wakati mgumu wakati mwingine kwa wanandoa wapya ni kuchelewa kupata mtoto. Wakati mwingine watu wanaamua kwa makusudi kutopata mtoto mara moja huku wakijitahidi kujipanga vizuri. Mgogoro mkubwa huanza mwaka mmoja baada ya ndoa kama hawaoni kile kinachoitwa "tunda la ndoa". Maswali yanabakia:
a. Je watu wanaweza kukaa pamoja na kuamua kuishi pamoja bila kutaka watoto?
b. Je ni lazima kupata mtoto mwaka wa kwanza wa ndoa? au hata mwaka wa pili?
c. Ni kwanini watu ambao hawajajaliwa mtoto huona bora kuachana kuliko kuchuka mtoto wa kuamua kulea (adoption)?
MMM
Duh!Uislaam unatowa jibu zuri sana kwa hilo. "Ruksa" kuoa mpaka wanne. Hapo kama tatizo ni mwanamme litajulikana tu, hata kama hataki kwenda Hospital.
Na jibu la pili ni kuwa Uislaam unaruhusu mwanamke "kupewa talaka" ikiwa mumeo hana uwezo wa kukuzalisha.
Kwani akisema kwa watu ni adopted kuna ubaya gani?..........Hili ni jaribu lingine la ndoa, ujue kipindi cha uchumba watu mnakuwa na malengo kwa tuzae watoto kadhaa..........sasa mnaingia kwenye ndoa miaka inakatika bila mtoto, aisee ni jaribu gumu mno.
Mie naona bora watu wasiwe wanazungumzia idadi ya watoto wala kuzaa kipindi cha uchumba, watu waamue kuishi pamoja kama mke na mume na kufanya watoto ni majaaliwa.
.......Adoption ni nzuri, ila mtoto wa kumzaa ana raha yake, una adopt mtoto na bado atakuja tu kusema kwa watu kwamba yeye ni adopted.
[/QUOTE].......Adoption ni nzuri, ila mtoto wa kumzaa ana raha yake, una adopt mtoto na bado atakuja tu kusema kwa watu kwamba yeye ni adopted.
Kaaaazi kweli kweli.Nimeshakueleza sababu ambayo inaweza kupelekea kutokueleweka.
Yani mtu anapoulizwa swali ambalo unaonekana ku react kama ni wewe.
Ndiyo alimjibia, pia kumjibia kwa kuuliza swali dhidi ya swali, badala ya kumjibia kwa kujibu swali,mbona mnakuwa wagumu kuelewa issue ndogo tu?
Kaaaazi kweli kweli.
Na wewe pia,kazi gani?Kaaaazi kweli kweli.
Na wewe pia,kazi gani?Acheni Ufala
Just **** off...
Ikumbukwe kuwa kabla ya kuoana inabidi wanandoa wajue kuwa wanaoana kwa vile wanataka kuishi pamoja kama wenza lakini co kuwa na watoto. Watoto wanakuja tu kama zawadi ya ndoa na pia majaaliwa ya mwenyenzi mungu. Hapo ndo wanandoa wengi wanapokosea, wengi wanaoana kwa ajili ya kupata watoto na mara nyingi wanaishia kuachana kama hawatapata watoto.
Kwasababu ya maneno ya nje (ndugu, marafiki, majirani)
MMM kwa dhana ya sasa na suala la ugumba lilivyo hakuna kitu kinachoitwa eti kupanga. Mnaweza ndani ya nyumba mkawa na mipango yenu kuwa tutapata mtoto may be baada ya miaka miwili ya ndoa yetu ila ulimwengu wa nje hawatawaelewa
Kumbuka kuwa walimwengu bado wana ile dhana kuwa mwenye matatizo anaweza kuwa mwanamke zaidi ya mwanaume
Kusema tuu nyie ndani ya nyumba mnapanga kutokuwa na mtoto kwa kipindi fulani bado hamtaeleweka kwa dunia ya nje. Bado mtaonekana mna matatizo
So mpaka ulimwengu wa nje uelewe kuwa ni kweli mmepanga inachukua muda sana mkuu
Sometimes external forces huleta presha kwa wanandoa hasa upande wa mume na kama mna hamu ya mtoto na hamjampata kw mwaka au miwili basi mwanamke huathirika kisaikolojia akiwaona wenzie wajawazito au wana watoto wao (nimewahi kuwauliza kadhaa hii) na hujisikia vibaya zaidi kama mtu atauliza baada ya mwaka au miwili vp shosti una mtoto wa kike au wa kiume?
Ni mipango tu ya wanandoa maana wao ndio watakaohudumia hao watoto, sema ndugu wengi hasa wa mwanaume huwa wanaingilia wakati yote ni mipango ya wanandoa na Mungu pia maana ndoa ni ya watu wawili na siyo watatu na Mungu ndio msaada wao na kimbilio lao.
Kuachana ni kutokana na maneno ya wanandugu mara nyingi ndio yanachangia hayo na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu adoption hususan hapa tz
Wataanzia wapi kuignore maneno ya nje wakati wengine hao hata ndoani wanaingia kutokana na hayo maneno?Huku kwetu maneno ya watu yanaongoza maisha ya wengi. . . na mpaka hilo litakapopungua ndo watu wataanza kujali hisia na matakwa yao wenyewe pale wanapofanya mambtherwise tukubali tu kwamba ndoa nyingi zinazovunjika kwa ukosefu wa mtoto/watoto sio kwa mapenzi ya wenye ndoa bali maneno ya wanaowazunguka.Wakuu heshima kwenu!
Lakini mimi nina tofautiana na mitizamo yenu. Suala alilosema Mwanakijiji ni pana sana; hapo suala la upendo wa dhati kwa hao wanandoa lazima ufikiriwe; suala la maamuzi ya wanandoa wenyewe pia lazima lifikiriwe.
Kwanza lazima tujiulize, kuhusu chanzo na msingi wa hao watu kuwa wanandoa. Je, wanapendana kwa dhati? Je, walielewa mafundisho ya ndoa? Maana kama wanapendana kwa dhati, naamini wataweza kukabiliana na changamoto zozote ambazo zitatokea katika maisha yao ya ndoa (ukosefu wa mtoto ikiwa ni mojawapo). Pia mafundisho ya ndoa (kwa dini ya kikristo) yanazungumzia juu ya suala hili; na ukosefu wa mtoto katika ndoa sio suala la kuweza kutengana kwa wanandoa, labda iwe nje ya taratibu za kidini, ambapo husipotengana ndani ya taratibu za kidini na ukamwacha mkeo/mmeo, utakua ukizini unapofanya tendo la ndoa na mwanamke/mwanamume unaeamini mtapata nae mtoto.
Suala la external forces katika ndoa si lakuvumiliwa na kudekezwa hata kidogo. Watu wakishakuwa mume na mke, wanapaswa wasisikilize wala kujali hizo pressure toka nje. Ndio maana wenzetu (watu wa Ulaya na Marekani) hapa wanakua wanatuzidi sana (once they are husband and wife, they don't give a damn about outsiders' gossips). Kwetu sisi waafrika hizi outsiders' gossips zinatuamiza vichwa sana kiasi kwamba ndio sababu ya ndoa nyingi kuvunjika. Sasa tukiweza kuhimili na kuignore hizo pressure toka nje (pamoja na kuzingatia mafundisho ya dini/ndoa) nadhani kesi za kuachana kwa wanandoa kutokana ukosefu wa mtoto zitapungua sana.