Kwanini kinyesi cha binadamu hakitumiki kama mbolea?

Kwanini kinyesi cha binadamu hakitumiki kama mbolea?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,863
Inasemekana yanaweza kuzalisha nishati mbadala

Lakini kwanini hayatumiki kwa mbolea kama wanyama wengine?
 
Kwa sababu tunatumia ya wanyama. Supply ikipungua, tutatumia mbolea ya binadam
 
Kwanza jiulize kwa nini yanafichwa kwenye mashimo yaani choo
 
Inasemekana yanaweza kuzalisha nishati mbadala

Lakini kwanini hayatumiki kwa mbolea kama wanyama wengine?

Ni kweli kuwa kinyesi chetu kinaweza kutumika kuzalisha nishati na nimeshudia baadhi ya maeneo wakikitumia kuzalisha nishati,kuhusu kutumika km mbolea ni kwamba inawezekana isipokuwa hadi ki- decompose,Sema wengi hawakitumii kutokana na changamoto mbalimbali km vile harufu,Usafirishaji hadi shambani,n.k.
 
Inasemekana yanaweza kuzalisha nishati mbadala

Lakini kwanini hayatumiki kwa mbolea kama wanyama wengine?

Kakuambia nani hakitumiki kama mbolea? Kutokuona kitu fulani au kutosikia haimaanishi hakipo.

Unajua biosolids ni nini? Jaribu kutafiti!

300px-Biosolid.pumpkin.row.jpg
 
Nimeshuhudia wamisionary songea wakikomwaga mashambani baada ya mavuno. Ila kinakuwa haina harufu huwekwa sawa na maji mengi kisasagika then wanamwaga shambani.
 
Kinyesi cha biandamu kina mbole yenyerutba sana, cha kuzingatia wakati wa maandalizi kisiwe kimechanganyika na mkojo, China katika kilimo cha mpunga wanatumia sana kinyesi cha binaadam
 
Akitokea mwekezaji tutafanya upembuzi yakinifu utakaopelekea mpango mkakati wa kuratibu mchakato wa kuwekeza katika hii sekta ila inabidi tujaribu kuwafanyia utafiti binadamu kadhaa na vyakula wanavyokula ili tuone ni vyakula gani mtu akila raw material anazotoa zina nishati kubwa ya gesi...asante!
 
Ni kweli kuwa kinyesi chetu kinaweza kutumika kuzalisha nishati na nimeshudia baadhi ya maeneo wakikitumia kuzalisha nishati,kuhusu kutumika km mbolea ni kwamba inawezekana isipokuwa hadi ki- decompose,Sema wengi hawakitumii kutokana na changamoto mbalimbali km vile harufu,Usafirishaji hadi shambani,n.k.

Mkuu ila prosess yake ya kuandaa mbolea ya mavi sisi tumekitumia sana na mazao yanastawi hadi kero sijasimuliwa ila hvi vioo vya maji ni shida! kama choo siyo cha maji kikishajaa una stop kukitumia kwa mda halafu baada ya mda unachimba pembeni ya choo kwa nje unachota halafu unaendaa kumwanga mahali kama kifusi kikikauka unakiponda hadi kinasagika hakina harufu wala nini! karibu mbeya
 
Akitokea mwekezaji tutafanya upembuzi yakinifu utakaopelekea mpango mkakati wa kuratibu mchakato wa kuwekeza katika hii sekta ila inabidi tujaribu kuwafanyia utafiti binadamu kadhaa na vyakula wanavyokula ili tuone ni vyakula gani mtu akila row material anazotoa zina nishati kubwa ya gesi...asante!

Hapa inakubidi uende kijijini maana hapa mjini chips yai mavi yake hayawezi kutengeneza nishati hata mbolea yake haina rutuba!
 
Inasemekana yanaweza kuzalisha nishati mbadala

Lakini kwanini hayatumiki kwa mbolea kama wanyama wengine?

MKUUKinatumika sana sema tu hujui uliza wale wanaoka kandokando ya bwawa la mavi watakuambia sifa ya mbolea hiyo
 
Hapa inakubidi uende kijijini maana hapa mjini chips yai mavi yake hayawezi kutengeneza nishati hata mbolea yake haina rutuba!

Tena vijiji vyenyewe tunavifanyia utafiti pia,mfano kwa kuwa ndani ya mkoa mpya wa Songwe kuna mtambo wa kuzalisha hewa ukaa ya asili na kwamba Kiwira iliyo kwenye mkoa huo huo kuna makaa ya mawe ambayo vyote ni nishati basi wakazi wa Mwakaleli,Kandete,Mwatisi,Busokelo,Kiwira na vijiji vinavyopakana na hivi utafiti uwahusu!
 
Kwa wachina mbolea ya binadamu ni nzuri zaidi ya wanyama. Tena kinyesi cha binadamu kinatokana na vitu tunavyokula na vinavyoeleweka tofauti na vya wanyama ambao wanakula hovyo tu.
 
Inasemekana yanaweza kuzalisha nishati mbadala

Lakini kwanini hayatumiki kwa mbolea kama wanyama wengine?

Kinyesi cha binadamu kama mbolea kinaweza kusababisha magonywa hatari sana na mengi sana, hivyo utumiaji wake unapaswa kuwa makini sana. Hatari ni nyingi kuliko faida. Orodha ya magonjwa unayoweza kupata kutokana na kinyesi cha binadamu ni kama ifuatavyo, na baadhi ya haya magonjwa utakufa haraka sana;

Polio Hepatitis A, E
Viral diarrhoeas such as rotavirus and adenovirus
Typhoid and paratyphoid
Cholera
Bacillary dysentery
Anthrax
Bacteria diarrhoeassuch as Yersinia, Campylobacter, E. coli
Amoebiasis
Giardiasis
Ascariasis
Enterobiasis
Trichuriasis
Taeniasis
Hydatidosis
Botulism
Staphylococcal food poisoning
Enterotoxigenic coli diarrhea
 
Back
Top Bottom