Kwanini kina Baba hatupongezwi kwa kupata mtoto?

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Habari za wakati huu wanajamii?

Ningependa kujua kuna sababu za msingi za kina baba kutopongezwa kwa kupapa mtoto na mama kupongezwa tu au ni ubaguzi tu, au ni mazoea tu?

Siku hizi hata baba hupata lizizo ya siku tatu (partenity leave) akipata mtoto ila kwanini huyu baba yeye pongezi hapati bali ni kwa mama tu? Kwani bila baba huyu mama angempata huyo mtoto?

Kuna stori moja hivi nilishuhudia kwenye kiosk kimoja, walikuja baba na mama wametoka hospitali mama kapakata mtoto alitoka kujifungua. Walipofika pale kwa kiosk wakaja kina mama wanampa yule mama hongera na vigelegele juu halafu yule baba anaulizwa za saa hizi shem.

Baba alipoona hamna anayemwambia hongera akaamua akatangulia zake. Kama vile alichukia maana nilimsikia akisema yaani kina mama watu wa ajabu sana wanampongeza tu maana ina maana mimi sistahili?

Anyway, tunastahili pongezi sawa na wao au hapana? Maana hata zawadi wanapewa kina mama, pia kuna vyama vya wanawake vya kuzawadiana mmojawapo anapojifungua, vipi sisi kina baba tupatapo mtoto?
 
sababu anaweza asiwe wake kweli, tofauti na mama
 
Aliepata mtoto ni mama. Wewe kama mme umejaaliwa. Na hatukupongezi sababu wakati mkeo akizaa kwa uchungu,wewe waweza kaa pale vigrosari vya nje ya hospital ukisubiria huku ukigonga baridiiii mbili tatu.
 
Pongezi alishapata utamu, nyingine atapewa mtoto akimaliza chuo kikuu, na pia atakapooa au kuolewa kama hajazalia home
 
Habari za wakati huu wanajamii?
Ningependa kujua kuna sababu za msingi za kina baba kutopongezwa kwa kupapa mtoto na mama kupongezwa tu au ni ubaguzi tu, au ni mazoea tu?

Siku hizi hata baba hupata lizizo ya siku tatu (partenity leave) akipata mtoto ila kwanini huyu baba yeye pongezi hapati bali ni kwa mama tu? Kwani bila baba huyu mama angempata huyo mtoto?

Kuna stori moja hivi nilishuhudia kwenye kiosk kimoja, walikuja baba na mama wametoka hospitali mama kapakata mtoto alitoka kujifungua. Walipofika pale kwa kiosk wakaja kina mama wanampa yule mama hongera na vigelegele juu halafu yule baba anaulizwa za saa hizi shem. Baba alipoona hamna anayemwambia hongera akaamua akatangulia zake. Kama vile alichukia maana nilimsikia akisema yaani kina mama watu wa ajabu sana wanampongeza tu maana ina maana mimi sistahili?

Anyway, tunastahili pongezi sawa na wao au hapana? Maana hata zawadi wanapewa kina mama, pia kuna vyama vya wanawake vya kuzawadiana mmojawapo anapojifungua, vipi sisi kina baba tupatapo mtoto?

Anayepanda Mbegu Katika Bustani au Shamba Huwa Hasifiwi Sana Kama Yule Anayehakikisha Kila Siku Anamwagilia, Anapalilia Na Kuweka Mbolea Kila Inapobidi Na Kuhakikisha Ustawi Mzima Wa Shamba Husika.
 
Aliepata mtoto ni mama. Wewe kama mme umejaaliwa. Na hatukupongezi sababu wakati mkeo akizaa kwa uchungu,wewe waweza kaa pale vigrosari vya nje ya hospital ukisubiria huku ukigonga baridiiii mbili tatu.

hata kama, hata mbona unamtunza akiwa mjamzito?
 
Pongezi alishapata utamu, nyingine atapewa mtoto akimaliza chuo kikuu, na pia atakapooa au kuolewa kama hajazalia home

hapana bhana, mbona yeye mama asisubiri hayo? Je asipofika chuo ama asipooa na kuolewa?
 
Anayepanda Mbegu Katika Bustani au Shamba Huwa Hasifiwi Sana Kama Yule Anayehakikisha Kila Siku Anamwagilia, Anapalilia Na Kuweka Mbolea Kila Inapobidi Na Kuhakikisha Ustawi Mzima Wa Shamba Husika.

hivi mtoa mbegu, mbolea, maji, dawa, n.k na mwekaji wa hizo mbolea, dawa, maji, n.k yupi mpalizi mkuu?
 
kwa sababu nyie mlitoa maligafi tu na wakati mnatoa huwa mkimaliaza tuna waambiaga pole baby au pole honey au majina mengine fake yote...sasa ile pole pale kitandani wakati mnatoa mbegu inatosha .. halafu sisi tunaanza kutengeneza mtoto (kiwanda) baada ya kumaliza kutengeneza lazima tupewe pole kwa kazi nzito ya kubadili maligafi kuwa bidhaa na ikaingia duniani..... tunahitaji pongezi na pole nyingi
 
Kina baba hamjui uchugu wa kupush mtoto.mmeshiriki kupata mtoto tuu kama starehe.
 
kwa sababu nyie mlitoa maligafi tu na wakati mnatoa huwa mkimaliaza tuna waambiaga pole baby au pole honey au majina mengine fake yote...sasa ile pole pale kitandani wakati mnatoa mbegu inatosha .. halafu sisi tunaanza kutengeneza mtoto (kiwanda) baada ya kumaliza kutengeneza lazima tupewe pole kwa kazi nzito ya kubadili maligafi kuwa bidhaa na ikaingia duniani..... tunahitaji pongezi na pole nyingi

mkuu upo? Thatha, mbona mwatuamsha hadi usiku wa manane tuwaletee mkaa mtafune? Huoni kwamba sisi pia twahangaika na nyie kuwahudumia hadi kupanua njia kuna starehe hapo kweli?
 
kiwanda kipo kinafanya kazi mda wote kinahitaji maji, umeme na wakati mwingine hata marekebisho hiyo ni part ya kuhudumia kiwanda
 
Kwani kupasuliwa utamu?

aseeeeeiiii kubeba mimba miezi tisa siyo
mchezo bana robo tatu mwaka
uko na kitumbo mara kutapika
mara miguu kuvimba na vyinginevyo
nyie kina baba mnastarehe tuu
wala hupati kero ya kichefuchefu
kina mama wanastahili pongezi
loveeee u mama mungu
akubariki kwa kuvumilia yote mpaka
kunileta duniani
saluteeeeee......
 
kiwanda kipo kinafanya kazi mda wote kinahitaji maji, umeme na wakati mwingine hata marekebisho hiyo ni part ya kuhudumia kiwanda

mgodi ukitema huwa tunapongezana ila mwenye mgodi hupewa kofia. Kwani team ikichukua kombe hupongezwa kocha pekee?
 
Back
Top Bottom