Kwanini kila pakiboreshwa wateja wanakimbia?

Kwanini kila pakiboreshwa wateja wanakimbia?

Impimpi

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2019
Posts
468
Reaction score
971
Wakuu habari
Hii kitu imenitokea juzi juzi nilikuwa na kimgahawa changu kidogo tu ila kilikuwa kinalisha watu wengi sana na ilhali mazingira hayakuwa rafiki kiafya na kifupi haikuwa sehemu yenye hadhi na kuvutia kabisa.
Nikajipanga nikapaboresha nikapajenga ili watu wakae ndani full feni na viti vizuri ila bei ikabaki ile ile.
Kilichotokea wateja karibia wote wamekimbia hawaji tena
Maandazi yanavunda kabatini ..chapati ndio usiseme zinakuwa kavuuuuu wadau nifanyeje au nilikosea kuboresha?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mgahawa wako upo kwenye location ipi kwanza !?=
.
Usije kuwa umeipeleka Sheraton vingunguti halafu unaanza kujilaumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na hongera kwa changamoto
Ila inabidi uelewa kuwa kutokana na kipato katika jamii kuna makundi makuu matatu ya wateja kuna wateja wenye kipato kikubwa, kipato cha kawaida na kipato kidogo.
Hivyo basi katika biashara yako inakupasa uiposition katika mazingira na muonekano wa kuvutia aina ya wateja ulio watarget na kuwa ignore aina nyingine.
Kwa mfano umeshawahi jikuta unahofia kuingia duka flani la nguo au saluni kutokana na mwonekano wake tu yaani unajenga taswira katika akili yako kuwa lazima bei ya bidhaa au huduma itakua ghali.

Hivyo basi epukana na hilo kwa kuweka bango la menu lenye orodha ya vyakula pamoja na bei zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom