TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,743
Mbowe alisema Lowassa aliletwa na Dr Slaa, Dr Slaa alisema Lowasa ameletwa na Gwajima na Mbowe, Gwajima alisema Lowassa aliletwa na Slaa akishirikiana na yeye Gwajima, Lipumba anasema Lowassa ameletwa na Mbatia, Mbatia alisema Lowasa ameletwa na Lipumba, Maalim anasema Lowassa aliletwa na Lipumba. Lowasa yeye alisema alifuatwa na viongozi wa CHADEMA.
Je, Lowassa alikuwa ni haramu kwenda UKAWA. Mbona kila mpinzani anajisikia AIBU kukiri kuhusika kumleta Lowassa UKAWA? Je Lowassa ni mzigo mpaka wote wakane kuhusika kumleta CHADEMA?
Hivi kama CHADEMA na UKAWA imeanza kumpiga mpira Ndugu Lowassa leo. Ikifika 2020 hali itakuweje? Basi kama alinunua tiketi na chama ili agombee urais tuambieni. Vita vina mbinu nyingi ilimradi tu ushinde vita.
Niwakumbushe swali la msingi la Dr. Slaa ambalo hamjamjibu hadi leo " Je Lowassa ni Asset au ni liability (mzigo)?
I rest my case.
Remy Cameroon